Ewe mwenyezi Mungu, naamini wewe ndiye uliyetoa kibali cha kuanzishwa kwa mchakato wa uandishi wa katiba mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naamini uliruhusu hili baada ya kuona kwamba watu wako tunaishi katika nchi yenye kila aina ya neema pasipokuwa na mwangozo ufananao na neema uliyotukirimu. Tunakushukuru sana kwa kuruhusu jambo hili kwa kupitia mamlaka zetu za kidunia. Naamini kwamba ukamilifu wa jambo hili ni mwanzo mpya wa safari yenye matumaini ya kuelekea nchi ya ahadi, nchi iliyojaa asali na maziwa ambayo kila mtanzania, wa leo, kesho, na hata kesho kutwa ataifaidi kwa kadri ya mapenzi yako.
Umetupitisha kwenye vipindi mbalimbali vya mchakato huu. Tunashukuru kwa mamlaka zilizohusika mpaka kutuvusha huko kwa mafanikio japokuwa kila kipindi kimekuwa na manung'uniko. Na hata sasa tunapoingia katika bunge la katiba bado kuna manung'uniko. Sababu za manung'uniko haya zipo nyingi. Mojawapo ni ukosefu wa busara na hekima kwa mamlaka ulizozipa dhamana ya kulisimamia jambo hili. Badala ya kulisimamia jambo hili kwa kweli na haki yako, baadhi ya mamlaka ziliingiza unafiki na ubinafsi. Kuna zilizoshupaza shingo kiasi cha kutokugeukia upande mwingine na kuwatazama watu wako. Lakini kuna zilizogeuka nyuma kama "mke wa Lutu" ili kujikumbusha na julinda maslahi ya finyu ya jamii zao. Kwa ukuu wako, naamini uliyaona hayo lakini uliyaacha yafanyike kwa makusudi.
Umeruhusu tuingie katika bunge la katiba. Bunge hili linaundwa na wajumbe wenye sifa mbalimbali. Wapo wa kuchaguliwa na wananchi kutokea majimboni na wapo wa kuteuliwa na Muheshimiwa Rais. Wapo wenye taaluma na wasio na taaluma. Wapo wanaujua kitu gani kinawapeleka huko lakini pia huenda wapo wasiojua nini hasa wanatakiwa kufanya. Yawezekana pia lipo kundi la wajumbe walioingia kwa hisani ya "uncle" ili kulinda maslahi ya "mjomba" na "shangazi" au "adili na nduguze". Kuna wengine tuliambiwa wameteuliwa kwa sababu wana "malengo yanayofanana" lakini kwa kuangalia kwa macho ya kawaida mfanano huo una mashaka. Anyway, wewe wajua. Kimsingi bunge hili yawezekana limesheheni "wawakilishi" wa kila kundi katika jamii yetu. Japokuwa hatuna uhakika kama uwakilishi huu utakuwa ni ule "uliotukuka". Anyway, wewe Mungu wajua.
Tunakuomba mwenyezi Mungu umbariki hekima na busara mwenyekiti atakayechaguliwa kuongoza bunge hili ili aongoze vikao kwa kwa kuikiri kweli yako. Wajaaliye wajumbe wa bunge la katiba afya tele ili waweze kutimiza majukumu yao vema. Tunakuomba uwakumbushe majukumu yao ya msingi. Hii ikiwa ni pamoja na kukumbuka matakwa ya wananchi walio wengi. Wakumbushe wale wabunge wa kutoka majimboni kuwa hawawakilishi nafsi zao au vyama vyao vya siasa bali wao ni wawakilishi wa wananchi wao waliowachagua. Waepushe wajumbe na ROHO MTAKA PESA ilimwapinge endapo "mjomba" na "shangazi" na hasa uncle, ataamua kuwapa mihela ili hali kila kukicha kiguu na njia "tukitembeza bakuli" huku na kule ili kupata chochote kitu. Au la waikubali mihela hiyo lakini walijaze bakuli letu ambalo hulitembeza lakini halijawahi ili liweze kuwasaidia watanzania wanaoangamia kwa kukosa huduma muhimu kabisa kabisa za kijamii.
Waepushe wajumbe na pepo la usingizi. Waepushe na unafiki na utetezi wa maslahi binafsi au ya kikundi fulani cha watu wachache wasioitakia mema safari ya watanzania ya kuelekea nchi ya matamanio ya watanzania walio wengi. Waepushe na jazba, wape moyomwamsubra katika majadiliano. Waepushe na ubabaishaji. Wakumbushe kufuata taratibu na kanuni za mjadala. Wakumbushe kujadili mambo yote ya kijamii kwa uzito stahiki bila uchovu. Waondolee upofu ama wa kujilazimisha au wa iukosa maarifa au kiburi katika kuyaona mambo kwa upana wake.
Ewe mwenyezi Mungu, usisite kuwa LAANI wajumbe waongo, walafi, wanafiki, wabinafsi watakaotetea hoja kwa manufaa yao au ya kakikundi fulani cha wachache kisichokuwa na manufaa kwa watu wako tulio wengi. Mlaani yoyote yule ambaye hatasimamia hoja na kweli yako. Kwa unyenyekevu kabisa nakuomba mwenyezi Mungu usisite kuwajaza baraka tele wale wote watakaosimamia hoja na kweli yako kwa maslahi na manufaa ya watanzania.
Wajaalie watanzania wote amani na mshikamano katika kipindi hiki cha bunge la katiba. Ninaamini katika wewe Mungu, katiba mpya waitakayo watanzania inawezekana.
Mungu libariki bunge la katiba. Mungu ibariki Tanzania. Amina
Mwl Shukia
richardshukia@gmail.com