Sakata la vyeti feki: Wanasiasa wanaweza kuwaharibia Wahanga kwa Rais Magufuli

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,741
6,432
Nimeona Matamko ya Mh Lowassa na wansiasa wengine wa Upinzani wakisema wanashangaa Mh Rais kuwafukuza watu wote waliofoji Vyeti kuwa hali hiyo nikukosa ubinadamu.

Kwa taarifa zilizopo ni Kwamba serikali ilikuwa inaangalia njia bora ya kuwasaidia lakini kama wanasasa wataanza kulitumia kutafuta sifa basi mh Rais anaweza akasitisha mipango mzuri na kuwaambia waende mahakamani kudai haki na hapo ndo watapoteza na kufungwa.

Hivyo wanasiasa waliache hili suala kulizungumzia kwa sasa kwani wanaweza kuharibia maisha ya watu.
 
Nimeona Matamko ya Mh Lowassa na wansiasa wengine wa Upinzani wakisema wanashangaa Mh Rais kuwafukuza watu wote waliofoji Vyeti kuwa hali hiyo nikukosa ubinadamu.Kwa taarifa zilizopo ni Kwamba serikali ilikuwa inaangalia njia bora ya kuwasaidia lakini kama wanasasa wataanza kulitumia kutafuta sifa basi mh Rais anaweza akasitisha mipango mzuri nakuwaambia waende mahakamani kudai haki na hapo ndo watapoteza na kufungwa. Hivyo wanasiasa waliache hili suala kulizungumzia kwa sasa kwani wanaweza kuharibia maisha ya watu

Vyeti feki. OK. Vipi kuhusu kodi waliyolipa serikalini? Nayo ni feki?
 
Hii kitu nmeifikiria mda mrefu sana...ila sikupata mda wa kuanzisha thread. Kuna wanasiasa hapa nchini watatuharibia mipango aisee.....wabunge wanatumia matukio yanayotokea kujinufaisha kisiasa bila kuangalia madhara ya wengine hapo baadae...yaani wao wanawaza ya leoleo baasi!!!!.... Hawana maono kabisa....na wakifuatwa kwa kile wanachokisema basi tupo hatarini kuharibu mambo mengi sana
 
Serikali ndo yenye makosa kwanini iliajiri watu wenye vyeti feki
Pili wahusika wanamakosa kwanini walidanganya vyeti
Tatu kutokana na makosa hayo kuna labour force yao ilifanyika kwa weredi bila wasiwasi na uzoefu kazini wakudumu kwanin msiwalipe mafao yao
 
Nimeona Matamko ya Mh Lowassa na wansiasa wengine wa Upinzani wakisema wanashangaa Mh Rais kuwafukuza watu wote waliofoji Vyeti kuwa hali hiyo nikukosa ubinadamu.Kwa taarifa zilizopo ni Kwamba serikali ilikuwa inaangalia njia bora ya kuwasaidia lakini kama wanasasa wataanza kulitumia kutafuta sifa basi mh Rais anaweza akasitisha mipango mzuri nakuwaambia waende mahakamani kudai haki na hapo ndo watapoteza na kufungwa. Hivyo wanasiasa waliache hili suala kulizungumzia kwa sasa kwani wanaweza kuharibia maisha ya watu
Ishu sio kuomba hiyo ni haki yao na serikal iwape haki yao wakileta kiburi chuki na visas vya hawa mamia ya watanzania wenye familia zao na ndugu zao itakuja kuleta sana shida . wapewe haki yao mbona wamenufaisha taifa kwa utumishi wao kwanini wadhulumiwe haki zao.

Wanasiasa wana haki ya kutoa maoni yao maana ndiyo wawakilishi na wasemaji wa wananchi

Na kwa lowasa lazima aone hiyo ni sehemu ya kumjengea point huko baadaye itakuja kumsadia kuwakumbukusha hao walio fukuzwa na wengine kufa kwa pressure kisa vyeti feki na familia zao juu ya unyama na ukatili wa viongoz wetu hawa
 
Mwambieni huyoo nabii wenu aweke basi na yeye PhD yake mezani.. Sio mnapiga kelele tuu hapa eboooooo
 
Nimeona Matamko ya Mh Lowassa na wansiasa wengine wa Upinzani wakisema wanashangaa Mh Rais kuwafukuza watu wote waliofoji Vyeti kuwa hali hiyo nikukosa ubinadamu.Kwa taarifa zilizopo ni Kwamba serikali ilikuwa inaangalia njia bora ya kuwasaidia lakini kama wanasasa wataanza kulitumia kutafuta sifa basi mh Rais anaweza akasitisha mipango mzuri nakuwaambia waende mahakamani kudai haki na hapo ndo watapoteza na kufungwa. Hivyo wanasiasa waliache hili suala kulizungumzia kwa sasa kwani wanaweza kuharibia maisha ya watu
Maisha yao yameshaharibiwa na 'double standard' , chuki na visasi vilivyoandamana na zoezi hili. Wengine kwa sasa ni Marehemu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Vyeti feki. OK. Vipi kuhusu kodi waliyolipa serikalini? Nayo ni feki?
Kwani wale majambaz wanao pola mali za watu Fedha na n.k je, zile Fedha zao zinapotumika kulipa kodi zinakua sio halali.. Ndio mana ata Fedha za madawa bado watu wanatoa sadaka kanisani
 
Nimeona Matamko ya Mh Lowassa na wansiasa wengine wa Upinzani wakisema wanashangaa Mh Rais kuwafukuza watu wote waliofoji Vyeti kuwa hali hiyo nikukosa ubinadamu.Kwa taarifa zilizopo ni Kwamba serikali ilikuwa inaangalia njia bora ya kuwasaidia lakini kama wanasasa wataanza kulitumia kutafuta sifa basi mh Rais anaweza akasitisha mipango mzuri nakuwaambia waende mahakamani kudai haki na hapo ndo watapoteza na kufungwa. Hivyo wanasiasa waliache hili suala kulizungumzia kwa sasa kwani wanaweza kuharibia maisha ya watu

Tatizo la wapinzani ni kuongea bila kufikiri. Mwizi kakamatwa na kuku na kapata kichapo hadharani...utasema kaonewa? Hawa waliofoji vyeti ni maraharamia haramu, walifirisi nchi na kutia taifa hasara kwa kuajiriwa bila kuwa na taaluma sahihi. Sheria yake ilibidi wakamatwe na kufungwa na kuidanganya serikali, in short hawana haki yeyote.
 
Back
Top Bottom