Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Ngoma inogile. TAKUKURU acheni siasa ili wananchi wawe na imani nanyi. Msaidieni Rais kutumbua majipu hata kama yamekaa sehemu mbaya
============
Siku tatu baada ya kuibuka kwa kashfa ya rushwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemuita Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kumhoji.
Muda mfupi baada ya taarifa za kashfa hiyo kuwa wazi, Zitto na mwenzake wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ambao ni wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii, walimuandikia barua Spika wa Bunge, Job Ndugai kujiondoa kwenye nafasi zao ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
Zitto alithibitisha kupata wito kutoka makao makuu ya Takukuru ili kuhojiwa juu ya sakata hilo na akapongeza kuwa endapo vyombo vya Serikali vitakuwa makini kushughulikia tuhuma zote zinazoelekezwa kwa wanasiasa na watumishi wengine wa umma, itasaidia kuongeza uwajibikaji na kupunguza uzushi kwa wananchi.
“Nimepata wito huo kupitia Ofisi ya Bunge. Nasikia Bashe ameitwa pia. Nafurahi wito wetu wa uchunguzi umechukuliwa kwa uzito unaostahili na tutatoa ushirikiano wote kwa vyombo vya uchunguzi ili kumaliza zoezi hili kwa haraka na kwa ufanisi,” alisema Zitto.
Alipotafutwa Bashe ili kupata ukweli wa kuitwa kwake, ingawa hakutimiza ahadi yake, alisema:“Sipo kwenye nafasi nzuri ya kuzungumza hivi sasa.”
Mpaka jana, wakati Takukuru ikiendelea kuwahoji wanasiasa na watendaji wa mashirika yaliyotajwa kuhusika kutoa rushwa ili kubadili maoni ya wajumbe juu ya utendaji wao, wabunge wawili walithibitika kuitwa na Takukuru.
Tuhuma hizo zimekwenda sambamba na Ndugai kuwaondoa wenyeviti wa kamati za Ardhi, Maliasili na Utalii; Nishati Madini; Uwekezaji na Mitaji ya Umma huku ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Huduma na Maendeleo ya Jamii lakini akisema ni uhamisho wa kawaida
Mkurugenzi Mkuu wa Taakukuru, Valentino Mlowola, bila kuingilia uchunguzi unaoendelea alithibitisha kuwaita wabunge hao na watendaji wa mashirika waliohojiwa.
“Hili ni suala la uchunguzi Bado linaendelea hivyo si wakati muafaka kutaja watu waliohojiwa mpaka sasa ingawa mahojiano yanaendelea. Kazi ikikamilika utapata taarifa kamili,” alissema Mlowola.
Chanzo: Mpekuzi