Sakata la Sukari

mayaJr45

JF-Expert Member
May 12, 2016
560
205
Nakuu alichosema mh rais february 17:

"Nakuagiza waziri mkuu kuanzia leo marufuku mtendaji yeyote wa serekali kutoa kibali cha kuagiza na kuingiza sukari toka nje vibali vyote natoa mimi".Mwisho wa kunukuu.

Napata shida sana kuelewa hizi kauli za rais amepiga marufuku uingizwaji wa sukari kutoka nje zilianzia wapi ? nchi inajulikana mahitaji ya sukari ni tani 420,000 na uwezo wa viwanda vya ndani ni tani 300,000 so hakuna namna ambayo rais makini kama mh magufuli atapiga marufuku wakati akijua kuna shortage hiyo.

Utoaji wa vibali hivyo kila mwaka unafanyika mwezi wa tisa na wa kumi kwa maana ya kipindi ambacho viwanda vya ndani vinamaliza uzalishaji shukari iwe tayari imeshaingia nchini maana kutoka brazil hutumia miezi miwili na kidogo .Wakati anasema vibali atatoa yeye tayari alikua anajua ni kina nani wamepewa vibali hivyo na tayari vilikua vimeshatoka toka hata hajaapishwa kuwa rais.

Turudi nyuma bunge lililopita kulikua na malalamiko mengi sana kutoka kambi ya upinzani kupitia hotuba ya waziri kivuli wa viwanda na biashara kwa miaka 2 iliyopita kuhusu sakata la sukari wakati huo hoja kubwa zilikua 2 kuhusu sukari

a) Serekali inatoa vibali hovyo sukari inaingia nyingi kiasi cha sukari ya ndani haiuziki na inaharibikia kwenye maghala ya sukari

b) sukari ya viwandani toka nje inauzwa mitaani na kwenye supermarkets.

Swala la sukari ni biashara kubwa na agizo hilo la rais kutoa vibali mwenyewe ni pigo kubwa kwa wafanyabiashara wajanja wajanja kwahiyo tunategemea jambo hili kupata muonekano wa kisiasa na hujuma kwa wafanya biashara wakubwa waliokua wanatumia viongozi wa serekali kufanikisha matakwa yao jambo ambalo linawapa wakati mgumu sana kwa serekali hii.Hivyo kutumia njia mbadala kufanikisha adhma hiyo

Uganda walifanya maamuzi hayo miaka ya nyuma na ulitokea mtikisiko mkubwa zaidi ya huu ila wakavuka salama leo hii wanaexport sukari.Serekali ipo imara haiwezi kuyumbishwa na wafanya biashara wachache wasio waaminifu kwa maslahi yao binafsi ila ni rafiki wa wafanya biashara waaminifu wanaojali maslahi ya watu.
 
Kama tutaendelea kuwa walalamikaji hatutaishia kulalamikia Sukari tu tuatendelea kulalamikia kila kitu.

Tutafute hela full stop
 
Tanzania ni kelere tu!! Mashamba yenyewe ya miwa hamna, Viwanda bado vipo Human labour based, Gunia kutembea kwenye mkanda utadhani mtoto wa miezi 5 anaetambaa.

Uchumi wa nchi unamilikiwa na Wahindi (ni rahisi kuhujumu nchi).

Budget ya kilimo na ya Viwanda na Biashara hazina ushirikiano utadhani demu anaejikirimu na Karoraiti.
 
investment ya viwanda vya sukari vinachangamoto kubwa sana kwanza inahitaji maeneo makubwa sana ya mashamba ya miwa yanalomilikiwa na kiwanda chenyewe kama 40% ya miwa inayohitajika kwa kiwanda lazima itokane na mashamba ya kiwanda then hii 60% urudi kwenye jamii kuhamasisha walime miwa kuwawezesha walime ikiwezekana ili kupata quality ya miwa inayotakiwa kwahiyo ni changamoto kubwa .japo inabidi tuikabili haswa private sector
 
Sasa kama mahitaji yetu ni tani 420000 /year japo hiyo figure huwa siiamini sana maana watu huwa wanatengeneza hayo mahitaji feki ili wapete ,hiyo fursa , na sisi tunazalisha 300000 / year je kuanzia mwezi FEB MPAKA LEO HILO GAPE LA 100000+limeshaaonekana ? Kwa maana nyingie matumizi yetu kwa mwezi ni tani 35,000
Kutoka feb , mpaka leo ,ni wastani wastani wa miezi 3 ambayo ni sawa na tani 100000+ kwa kwa hiyo miezi 3 je hili gape lilipaswa kujitokeza kwa hii miezi mitatu ya mwanzo maana na kumbuka bodi ya sukari ilisema kuliko na sukari ya kutosha na ndio maana wakaaweka hadi bei elekezi 1800
 
vibali vilivyotolewa ni kwa idadi hiyoyo ambayo hutolewa miaka yote na hakuna mwaka ambao umetokea upungufu kama huu na wakati rais anapiga marufuku vibali vilishatolewa toka oct last yr na hutolewa once per yr
 
Sasa oct mpaka feb ,sukari ilikuwa bado haijafika ? Au ni ile iliyokuwa depot kweli wakasema ilikuwa mara haijapata vibali vya TFDA /TRA
 
Sasa oct mpaka feb ,sukari ilikuwa bado haijafika ? Au ni ile iliyokuwa depot kweli wakasema ilikuwa mara haijapata vibali vya TFDA /TRA
hujuma imeanza baada ya tangazo la raisi vibali atatoa mwenyewe
 
Back
Top Bottom