Sakata la mimba shuleni latua kwa Ma-DC

Sakata la mimba shuleni latua kwa Ma-DC

Majs

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
232
Reaction score
520
MIMBAA.jpg
​
Lile sakata la ujauzito sasa limeshuswa kwa wakuu wa wilaya baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwataka kusimamia utekelezaji wa sheria za nchi zenye lengo la kumlinda mtoto wa kike na mimba shuleni.

Majaliwa amewataka wabunge kushirikiana na halmashauri zao katika kuweka mikakati ya kudhibiti ujauzito kwa watoto wa shule.

“Wahamasisheni wananchi watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola ili wanaowapa ujauzito au kuwakatisha masomo waozeshwe wapate adhabu stahili,” amesema Majaliwa kabla ya kuahirishwa kwa Bunge.

Amesema dhamira ya Serikali ni kumlinda mtoto wa kike ili apate elimu kwa ajili ya manufaa yake na Taifa kwa ujumla.

“Kila Mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu. Hivyo ni lazima tuhakikishe mtoto wa kike anapata elimu stahiki na masomo yake hayakatizwi kwa kupata ujauzito,” amesema.

Alisema kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Elimu Sura ya 353 kinatoa adhabu ya miaka 30 jela kwa yeyote atakayeoa au kumpa ujauzito mwanafunzi.

“Kuwaachisha masomo wanafunzi waliopata ujauzito ni utekelezaji wa Waraka na Kanuni za Elimu za Mwaka 2002 zinazohusu kufukuzana kuondoa wanafunzi shuleni kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo uasherati, wizi kutumia dawa za kulevya,” amesema na kuongeza kuwa; “Pamoja na utoro unaotokana na baadhi ya wanafunzi kwenda kufanya shughuli za biashara ndogo ndogo kucheza kamari, kuvua samaki, kuchimba madini.”


CHANZO: Mwananchi
 
Halafu watoto kama hao wakipata ujauzito litajitokeza genge la watu wanojiita wanaharakati kuwatetea eti warudi shule sasa wakirudi shule hizo hizo si ndio mwanzo wa kuporomosha maadili kwa wenzao ambao hawakua na tabia hiyo

Nadhani hawa wanaojiita wanaharakati wanapaswa kujikita kuelimisha watoto wa kike wasipate ujauzito na sio kuwatetea warudi shule hata hivyo hajakatazwa kurudi shule ila wamezuiwa kurudi shule za serikali

Mm nashangaa wanaotokwa na povu juu ya utekelezaji wa sheria hii wakati imeanza kutekelezwa kwa miaka mingi nyuma kama kweli walikiwa wapigania haki za watoto wa kike basi wangeandamana toka miaka ile sheria imetungwa ila nachoona sasa ni mihemko ya kisiasa tu
Ifike hatua tuwe na mitazamo ya kujenga sio kila kitu watu wanapinga tu, sasa madogo kama hao unawateteaje? Mbaya zaidi hata wazazi wao hawajui kama watoto wao wana tabia kama hizo, na kupelekea kuwagharimu kuonekana kama wazazi hawako makini na watoto huku mzazi akijua mtoto wake ameenda shule
 
Halafu watoto kama hao wakipata ujauzito litajitokeza genge la watu wanojiita wanaharakati kuwatetea eti warudi shule sasa wakirudi shule hizo hizo si ndio mwanzo wa kuporomosha maadili kwa wenzao ambao hawakua na tabia hiyo

Nadhani hawa wanaojiita wanaharakati wanapaswa kujikita kuelimisha watoto wa kike wasipate ujauzito na sio kuwatetea warudi shule hata hivyo hajakatazwa kurudi shule ila wamezuiwa kurudi shule za serikali

Mm nashangaa wanaotokwa na povu juu ya utekelezaji wa sheria hii wakati imeanza kutekelezwa kwa miaka mingi nyuma kama kweli walikiwa wapigania haki za watoto wa kike basi wangeandamana toka miaka ile sheria imetungwa ila nachoona sasa ni mihemko ya kisiasa tu
Licha ya yote, ungefanya research ndogo ungegundua kuwa wanaopata mimba wengi wanaonekana wastaarabu machoni pa watu na ndio wanaukumbana ni misala kama hii

Hao wanaonekena malaya malaya wapo nusu utupu huwa ni wajanja wajanja kwenye maswala ya kungonoka huwapigi bila condom, na vile vile ni watoaji wa mimba wazuri
Mf. Mdogo wngu alikuwa vzr shulen kuanzia kwenye academics hadi tabia/maadili alikuwa hatoki kwenye nafasi 3 za juu..lakini alipewa mimba akiwa form one huwez amini tena anadai alifanya mara moja tu

Kwhyo Swala la ngono mashuleni haliepukiki hata iweje ukizingatia kipindi mtoto yupo kwenye peak ya sexual desire punde baada ya kupevuka ilihali ni mwanafunzi lazima atajikuta amerubuniwa tu tena, ni nadra sana mtoto wa kike kumaliza form six hajasex

Sheria ya kutowaruhusu kurudi shuleni inabidi iangaliwe kwa mapana zaidi, au lah kuwe na utaratibu maalumu wa kurudi shuleni na siyo kuzuia kabisa kurudi shule lasivyo watakaoathirika wengi ni watoto wanaotokea kwnye familia duni wasiomudu private schools
 
Kuna wale wanaosema wamebakwa na wahuni wasio wanafunzi....wanasaidikaje
 
Back
Top Bottom