Sakata la Bandari: Kiongozi wa dini apinga viongozi wa Serikali kuburuzwa Mahakamani

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Arusha

Kiongozi wa dini ya kiislamu ya TWARIKA jijini Arusha, Sheikh Haruna Hussein ametoa tamko la kupinga vikali Sakata la uwekezaji bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World kufikishwa mahakamani akidai bado kuna muda kuweza kujadiwa likiwa nje ya mahakama.

Akiongea na vyombo vya habari kiongozi huyo, alisema hafurahishwi kuona serikali ikiburuzwa mahakamani wakati jambo hilo bado linaweza kuzungumzika juu ya vipengere vinavyolalamikiwa katika mkataba huo wa bandari.

"Kwa sasa kuna suala nyeti linaongelewa sana suala la bandari mimi kama kiongozi wa dini niwaombe wananchi wenzangu na wanasiasa watulie nchi kama nchi haiwezi ikauzwa ambayo inawatu wasomi tena wenye taaluma zao,rais ni mtu makini na anajua anachokifanya na anafanya kwa niaba ya watanzania".

Kiongozi huyo aliwaomba wale walokimbilia mahakamani warltulie kwani kwenda mahakamani ni sawa na kumdhalikisha kiongozi wa nchi...

"Inakuwaje leo unampeleka amrijeshi mkuu mahakamani kwa sababu wale walioshtakiwa wameshtakiwa kwa niaba ya rais bado tunawasihi sisi viongoI wasini warudi wake ili kuondoa sintofahamu iliyojitokeza".

Kesi hiyo ilifunguliwa Juni 27, mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kupinga baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

Katika kesi hiyo namba 05/2023, inawahusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Katibu wa Bunge.

20230704_122028.jpg
 
Jambo linazungumzika vipi ikiwa mhusika mkuu alishatamka wazi ameziba masikio?

Kwanini hataki wapelekwe mahakamani? alitaka wapelekwe wapi pengine?

Aache kuongozwa na hisia kwenye mambo ya msingi yanayogusa mustakabali wa taifa letu, kuanzia kizazi chetu na vizazi vijavyo vyote vya Tanganyika yetu, huyo Sheikh atumie akili kutafakari.
 
Mama sanyoko suluhu si kaziba masikio sasa mtajadiliana vipi?

BURUZA MAHAKAMANI MABOYA HAOO.
 
Back
Top Bottom