Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 395
Baada ya kusoma kitabu chote cha Morgan Housel hakika nasema kuwa kuna madini mengi sana kwenye vitabu ila ikiwa tu tutazingatia kuyasoma. Haya yafuatayo ni baadhi ya mambo 10 kwa ufupi sana ambayo Morgan Housel ameyasema ndani ya kitabu chake chenye chapter 20 na page zaidi ya 200.
•Kutafuta fedha na kuzimudu fedha ni vitu viwili tofauti. Lakini hiko cha kwanza hakiwezi kutokea bila hicho cha pili. Jifunze kumudu fedha zako ili uweze kuzitafuta kwa uhuru. Usipoweza kumudu fedha zako basi utateseka maisha yako yote ukiwa unazitafuta.
•Kutumia sana fedha sio kipimo cha kuwa wewe ni tajiri bali kuzitunza na kumudu ndio kila kitu. Morgan anasema kuna utofauti mkubwa sana kati ya Rich man na Wealthy man, na kutokujua utofauti wake basi ni chanzo kikubwa cha kuwa na matumizi mabaya ya fedha.
• Usitumie fedha kwa ajili ya kuwaonesha watu ni jinsi gani una fedha. Hiyo ni njia ya haraka sana itakayokuua.
• Jifunze kutunza sana fedha, kuwa na akiba. Akiba itakupa uhuru wa kupambana na baadhi ya mambo au shida ambazo huwa hazipigi hodi kwenye dunia hii ya mshangao.
Morgan anasema kwamba, tunza tu hela hata kama huna sababu maalumu ya kutunza we tunza tu !
• Usitumie fedha zako zote kununua kitu. Yaani usipende kuchukua hela zako zote (hadi akiba yako) kununua kitu huku ukitegemea kesho ni siku utapata tena fedha zingine.
•Epuka tamaa na ujifunze kuishi bila kushawishika au kukwazika na mitazamo au maisha ya wengine. Housel anaelezea nadharia ya watu wengi kuwa huwa wanatumia fedha zao ili waonekane na wengine kuwa na hela au kuishi maisha ya kushindana.
•Hakikisha unatumia fedha kidogo zaidi ya zile unazoingiza, kamwe usijaribu kutumia kiasi kikubwa kuliko kile unachoingiza. Utakufa ..
•Usifanye biashara kwa kuambiwa na watu. Muandishi anasema kwamba kila kazi ni rahisi sana ukiwa unahadithiwa lakini sio kwa kuifanya. Hivyo ogopa sana kuingia kwenye biashara kwa maneno tu.
•Hakuna kitu cha bure. Morgan anasema kwamba kila kitu duniani kina gharama hata kama gharama zake hazionekani wazi wazi. Hivyo kabla hujafanya jambo lolote linalohusiana na fedha ni lazima ujue gharama za jambo hilo ili lisikusumbue.
•Hasara ni sehemu ya maisha ya fedha, makosa pia ni mapungufu ya mwanadamu. Kamwe usikate tamaa mambo hayo yakitokea kwenye maamuzi yako ya hela..
Tamati, Morgan Housel anatoa mifano mingi ya maisha ya kweli kila anapoelezea jambo Moja. Hakika, kitabu chake kimesheheni mambo mengi sana kuhusu saikolojia ya fedha na kufanya kitabu hiko kuwa kwenye mauzo makubwa sana katika soko la vitabu la dunia.
Ahsante kwa kunisikiliza, naitwa Amani Dimile