Saikolojia: Matatizo ya utu(Personality disorders)

Kuna kipengele hapo maelezo yake yanamuhusu huyu rais wetu namba moja,huyu wanayesema Ni muhutu. Huyu kichwa upanga. Sasa tutawezaje kumpa dawa Na nani atamueleza tatizo lake.

nani atamfunga paka kengele???
 
Paranoid Personality Disorder anayo Mange.
maana kila linalofanyika anahisi kuna mtu ana plot against her
 
Sijajua kwa uhakika ila kwa maelezo yako ni dalili za depression. Njia nzuri ya kukabiliana na haya matatizo ni kuyaelewa vizuri, jaribu kusoma na kuelewa kuhusu depression. Pia kuna kitu tunaita rumination, mtu anakuwa anakazia mabaya tu akifikiria historia yake, hilo linamfanya aone hata yanayokuja yatakuwa mabaya tu, hii inaweza pelekea kujiua. Jitahidi kuwa positive, kumbuka mazuri uliyotendewa hata na hao ndugu waliokuumiza, kumbuka good moments kwenye maisha yako, tembelea watu hata kama hupendi maana ni dawa hiyo, Dawa huwa hatupendi ila hunywa. Ikiwezekana muone hata counselor shuleni kwenu, matatizo ya kisaikolojia yakianza kuathiri kazi, masomo au maisha huwa yanakuwa yamefika level ya kuhitaji matibabu.
 
Tatizo kubwa la watu wenye Personality disorders ni kuwa huwa hawakubali kuwa wana tatizo
Hii hufanya iwe kazi sana kuwatafutia matibabu.
Mkuu nin rafiki yangu ana tatizo la kuamini uchawi kupita kiasi yani yeye amepanga nyumba zaidi ya tano ndani ya mwaka mmoja. Kote anakohama anakubali kuacha kodi kwenda kuhamia sehemu nyingine anasema hizo nyumba anarogwa.

Mara ya kwanza tulimchukulia kawaida lakini hali imezidi kuwa mbaya mpaka ofisini amefikia hatua haelewani na wafanyakazi wengine anasema ni wachawi.

Yani nikikaa naye ni stori za yeye kurogwa, akiumwa, akiumia, akipoteza fedha yeye ni kurogwa.

Amepoteza fedha nyingi, ameshindwa kudumu hadi kwenye mahusiano kwa tatizo hili.

Je hili nalo ni tatizo la kisaikoloji? Kama ndio je ninaweza kumsaidiaje?
 
Kun kitu tunaita delusion. Hii ni kuamini vitu ambavyo ushahidi unaonyesha dhahiri kuwa havipo. Hii ni moja ya dalili ya ugonjwa wa akili(Schizophrenia). Mara nyingi imani za kidini na kiuchawi huwa haziwekwi kama zinatokana na kichaa ila zikizidi kama za huyo jamaa yako au mtu akianza kusema anaongea na Mungu huchukuliwa kama ni dalili za ugonjwa wa akili.
 
Tiba?
 
Poleeee weeeh
 
Mleta mada hongera Sana kwa kutuletea mada nzuri kwa wakati muafaka kabisaa
 
Nashangaa uzi wenye mambo...muhimu kama haya, unakuwaje na wachangiaji wachache hv? Hapa ndio utagundua kundi kubwa lililopo Jamii Forum ni watu wa aina gani, any ways...mtoa mada umenifunza mengi sana...natamani kujua zaidi. Mfano kipengele cha ant-social personality diosioder, mama mwenye nyumba wangu ana hizo tabia 100%. Mungu akubariki sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] unanikumbusha kaka yangu alikuwa mlokole kupitiliza unaweza kutembea nae akawa anakamata fly's kama nzi, mbu, vipepeo n.k anadai eti ni mapepo yametumwa kwake kuharibu huduma[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nikaona huyu ni kichaa mtarajiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…