Saidoo ndie mchezaji anayeikosesha Simba SC magoli

kalisheshe

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
1,870
3,492
Sielewi kwanini makocha, mashabiki na wachambuzi hawalioni hili,

Tangu apewe kiatu uchwara alichomtapeli Fistoni Mayele amekua ni mchezaji wa hovyo sana Msimbazi. Kila anapokua na mpira analazimisha kushoot au kudribble mpaka mipira inachukuliwa na wapinzani mwisho wa siku movement nyingi zinaishia kwake Simba inapocheza.

Kwakweli nashindwa kuelewa huyu ni no10 gani!.

Haiwezekani no 10 alazimishe kufunga yeye na sio kutoa assist Kwa mshambuliaji wa mwisho, hebu jiulize huyu no10 ka assist mara ngapi?.

Na kinachoumiza kingine huyu jamaa anapataje namba mbele ya Chama?!!, Mbona Chama ni mzuri akicheza no10 kuliko huyu mfungaji Bora uchwara?! Tukubali tukatae Chama Bado ana nafuu Kwa wachezaji tulionao Simba Kwa sasa.

Kingine ni kwanini acheze dk zote 90 while hakuna kitu Cha maana anachokifanya uwanjani zaidi ya kupoteza mipira na kuwapa Kazi wachezaji wenzake?!..

Kama saidoo ataendelea kucheza no10 hakuna mechi tutakayoshinda zaidi ya kutoa droo ama kupoteza.

Najua watetezi wa huyu no10 wa hovyo kuwahi kumuona watakuja hapa.
 
Tatizo ni kwamba yeye kidogo anajituma ila chama ni mzuri ila anatembeaga tu team ikiwa haina mpira.

Makocha wa kisasa hawataki mchezaji abiria uwanjan, hata yule aziz ki mechi ngumu ile ya Al ahly hafai kuanza kwasabab yupo slow na anachelewa kufanya maamuzi.
 
Kweli kabisa Key anajivuta ni mzito kufanya maamuzi ya haraka same kwa Saidoo anajituma lakini mwisho wa siku anapoteza mipira kizembe.

Nadhani umri ushamtupa ile fitness haipo yupo yupo tu.
 
Ndio anajituma
Lakini kujituma kwake hakuifaidishi timu

Ana magoli au assist ngapi mpaka sasahivi?
 
Kweli kabisa Key anajivuta ni mzito kufanya maamuzi ya haraka same kwa Saidoo anajituma lakini mwisho wa siku anapoteza mipira kizembe.

Nadhani umri ushamtupa ile fitness haipo yupo yupo tu.
Ingekua busara kama angekua anapangwa dk 15 au 25 za mwisho
Sielewi kwanini hawa makocha wanashindwa kumuonea huruma mzee mwenzao
 
Back
Top Bottom