Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Mchambuzi wa siasa na mwanasiasa mkongwe Said Miraj amesema kuna athari kubwa sana kwa chama cha upinzani CHADEMA kususia Uchaguzi Mkuu ujao, akitaja mifano kadhaa ya makosa kama hayo yaliyowahi kufanywa na chama chake cha zamani, CUF.
“Ni Uchaguzi wenye sura tofauti. Chaguzi nyingi zilizopita zilikuwa ni baina ya wapinzani na CCM, lakini Uchaguzi huu kwa kiasi kikubwa wimbi la ushindani lipo ndani ya CCM yenyewe kuliko kwa wapinzani. Mimi sitaki kuzungumzia CHADEMA kwenye Uchaguzi huu kwa sababu wenyewe wamesusa, wamesusa,” amesema Miraj.
Aidha, Miraj amefafanua zaidi kuhusu athari za uamuzi wa chama kikuu cha upinzani kususia Uchaguzi huo, akitoa mifano ya matukio yaliyowahi kutokea Zanzibar.
“Labda niseme tu, athari za kususia ni kubwa. Sijui kama wamejaribu kutazama faida na hasara zake. Nikupe mifano sisi Zanzibar tuliwahi kususia mambo kadhaa. Kwanza, tuligoma wanafunzi kwenda shule, serikali ikawazuia kuendelea na masomo, ikabidi tuwatafutie vituo vya kufanyia mitihani Bara. Tulipata gharama kubwa na usumbufu mkubwa.