Kwetu-Mbagala
JF-Expert Member
- Jun 26, 2013
- 203
- 39
Habarini wakuu, Awali ya yote ninapenda kujitambulisha kwenu kuwa, japo mimi ni mkazi wa Mbagala na kwetu ni Kusini (mikoa yenye gesi), ila nina maslahi na wilaya ya B'Moyo hasa katika jimbo la Uchaguzi Chalinze.
Mimi nimeoa huko (katika kijiji cha Madesa, jirani na Msata) na nina maslahi huko-shamba na nyumba. Hivyo siasa za B'Moyo kwa namna fulani zinaniathiri. LEO ninapenda kuleta kwenu hoja kuhusu Mbunge wetu wa jimbo la Chalinze, Mh. Said Bwanamdogo.
Kwa hakika, mimi sijaweza kuona kwa ukaribu ni kitu gani mpaka sasa kinachoonekana ambacho amefanya katika kuleta maendeleo ya jimbo letu. Sione ubunifu wowote ule.
Shule za kwetu bado ni za chini ya miti, mbavu za mbwa na zaidi nyingine ni zimejengwa kwa udongo! Kwa ufupi hakuna elimu ya uhakika. Shule zetu za kata (kama Kikalo nk) zipo hoi! Wanafunzi wanazurula ovyo mitaani, hakuna mabweni za zaidi hakuna mkakati wowote ule wa upatikanaji mabweni.
Ndugu zangu bado wanaendelea kulima kwa jembe la mkono (katika zama hizi za sayansi na teknolojia)!!! Kilimo kwanza...? Hakuna ubunifu wowote ule (hata kwa awamu) wa kuleta hata teknolojia rahisi ya jembe la kukokotwa na ng'ombe, 'Kubota' nk. Hivi hali hii mpaka lini? Hakuna jitihada zozote za kuanzisha hata kilimo cha umwagiliaji! Tuna mto wami, je umetumikaje katika kuchochea maendeleo yetu? Kilimo cha umwagiliaji ...? Michezo nako hoi, hatuna lolote la kujivunia. Uhamasishaji wa SACCOS (ili wananchi wajiendeleze kiuchumi) hakuna!
Wananchi sasa wameamua kuwa walevi kupindukia, nadhani ili kuondoa stress za maisha...
Kwa ujumla hali ni ngumu. Kumbuka mbunge huyu tulimchagua kwa kishindo kikubwa. Kitu kingine ni kuwa, hakuna ushirikishwaji wowote wa wananchi (wapiga kura?) walio ndani ya jimbo na sio tulio huku mjini ili kujadiliana namna gani ya kuliendeleza jimbo letu! Au uwezo wake ni mdogo (kama jina lake?)? Jimbo letu linatakiwa kuwa ni kioo cha majimbo mengine kujifunza, kwani jimbo letu ndio limetoa rais wa JMT kwa sasa. Pia kama kuna mtu ana rekodi za huyu mbunge wetu huko mjengoni tunaomba atujuze--amechangia kitu gani (maswali ya msingi, maswali ya nyongeza, muswada binafsi nk) toka awe mbunge.
Binafsi sijawahi kumsikia kabisa!!! Wadau, ninaomba mmpe mbunge taarifa mbunge wetu popote alipo ajitokeze tumsikie na atujibu mashaka/maswali yetu haya!
Tupo SERIOUS jamani tunamhoji mbunge wetu Mh.Bwanamdogo.Ninaomba wadau wa wilaya ya B'Moyo hasa jimbo la chalinze tujitokeze kuhoji.TUNAMUOMBA Mh.Bwanamdogo (au wapambe/wasaidizi wake) nae ajitokeze ajibu hoja.NINAOMBA habari za Minaki/Kisarawe tuziache kwa muda! Tuna kiu ya majibu ya hoja zetu.Hatuhitaji siasa ktk hili!
Said Bwanamdogo si aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya fulani Kigoma huko!ataweza kuwa karibu na wananchi wakati ana kazi ingine serikalini?wananchi wa jimbo la Chalinze mjipange tu kutafuta mbadala!nilifuatilia sana wakati wa kampeni ili nijue mustakabali wa Iman Madega maana aliutaka sana Ubunge!nilipofuatilia nikakuta kuna ukabila wa kutisha jimboni Chalinze!wakwere wako wachache sana,wadoe na waziguo ndio wengi zaidi!sasa kampeni zote zinapigwa uziguani ambapo ndipo kuna watu wengi na ndio wanaamua mbunge awe nani!....2015 nadhani ile vita itaanza upya!ule usemi wao wa katumwa na mjomba,hautakuwa na nguvu tena maana ndio silahaya yao ya ziada kila mtu anaegombea cheo chochote ndani ya bagamoyo anatumia silaha ya msaada ya ujomba!!anzia Kawambwa,Bwanamdogo,CCM Wilaya pale na madiwani wengi tu hadi ujumbe wa NEC!napita tu!
kingine nasikia huyu jamaa toka achaguliwe afya yake ni mgogoro.

Mbona mnachangia bila kuwa na info za kutosha, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ni yule kilaza mwingine aliyerithi jimbo kutoka kwa dhaifu, anaitwa RAMADHANI MANENO. Bahati mbaya hilo jimbo halijawahi kupata mbunge makini. Wote waliopita hapo ni VILAZA watupu. Nawasikitikia sana wakwere