Said Bwanamdogo: Mbunge wetu wa jimbo la Chalinze... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Said Bwanamdogo: Mbunge wetu wa jimbo la Chalinze...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kwetu-Mbagala, Jul 5, 2013.

 1. K

  Kwetu-Mbagala JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2013
  Joined: Jun 26, 2013
  Messages: 203
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habarini wakuu, Awali ya yote ninapenda kujitambulisha kwenu kuwa, japo mimi ni mkazi wa Mbagala na kwetu ni Kusini (mikoa yenye gesi), ila nina maslahi na wilaya ya B'Moyo hasa katika jimbo la Uchaguzi Chalinze.

  Mimi nimeoa huko (katika kijiji cha Madesa, jirani na Msata) na nina maslahi huko-shamba na nyumba. Hivyo siasa za B'Moyo kwa namna fulani zinaniathiri. LEO ninapenda kuleta kwenu hoja kuhusu Mbunge wetu wa jimbo la Chalinze, Mh. Said Bwanamdogo.

  Kwa hakika, mimi sijaweza kuona kwa ukaribu ni kitu gani mpaka sasa kinachoonekana ambacho amefanya katika kuleta maendeleo ya jimbo letu. Sione ubunifu wowote ule.

  Shule za kwetu bado ni za chini ya miti, mbavu za mbwa na zaidi nyingine ni zimejengwa kwa udongo! Kwa ufupi hakuna elimu ya uhakika. Shule zetu za kata (kama Kikalo nk) zipo hoi! Wanafunzi wanazurula ovyo mitaani, hakuna mabweni za zaidi hakuna mkakati wowote ule wa upatikanaji mabweni.

  Ndugu zangu bado wanaendelea kulima kwa jembe la mkono (katika zama hizi za sayansi na teknolojia)!!! Kilimo kwanza...? Hakuna ubunifu wowote ule (hata kwa awamu) wa kuleta hata teknolojia rahisi ya jembe la kukokotwa na ng'ombe, 'Kubota' nk. Hivi hali hii mpaka lini? Hakuna jitihada zozote za kuanzisha hata kilimo cha umwagiliaji! Tuna mto wami, je umetumikaje katika kuchochea maendeleo yetu? Kilimo cha umwagiliaji ...? Michezo nako hoi, hatuna lolote la kujivunia. Uhamasishaji wa SACCOS (ili wananchi wajiendeleze kiuchumi) hakuna!

  Wananchi sasa wameamua kuwa walevi kupindukia, nadhani ili kuondoa stress za maisha...

  Kwa ujumla hali ni ngumu. Kumbuka mbunge huyu tulimchagua kwa kishindo kikubwa. Kitu kingine ni kuwa, hakuna ushirikishwaji wowote wa wananchi (wapiga kura?) walio ndani ya jimbo na sio tulio huku mjini ili kujadiliana namna gani ya kuliendeleza jimbo letu! Au uwezo wake ni mdogo (kama jina lake?)? Jimbo letu linatakiwa kuwa ni kioo cha majimbo mengine kujifunza, kwani jimbo letu ndio limetoa rais wa JMT kwa sasa. Pia kama kuna mtu ana rekodi za huyu mbunge wetu huko mjengoni tunaomba atujuze--amechangia kitu gani (maswali ya msingi, maswali ya nyongeza, muswada binafsi nk) toka awe mbunge.

  Binafsi sijawahi kumsikia kabisa!!! Wadau, ninaomba mmpe mbunge taarifa mbunge wetu popote alipo ajitokeze tumsikie na atujibu mashaka/maswali yetu haya!
   
 2. C

  CHOYA Member

  #2
  Jul 5, 2013
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo jamaa nae kilaza kama alivyo dhaifu, jimboni haonekani wala bungeni hasemi chochote, ndio tatizo la wakwere kuchagua chagua ovyo ovyo, wakati ni maskin wa kutupwa
   
 3. mdeki

  mdeki JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2013
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 3,301
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Uchaguzi ukifika pigeni chini huyo

  "To know the enemy is half the victory"
   
 4. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2013
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,077
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi kuna jina kama hili pale mjengoni?Bi kirobot hebu kam kipande hii utupe udhibitisho una hii jina kwa daftari yako?
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2013
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145

  Huyu BWAMDOGO alizungumziwa na Prince Ridhwani Kikwete; Wana UNDUGU - ukimsikiliza Inaonyesha Wakware wote ni NDUGU na ni Wavivu? hawashurtishi Kazi, Angalia Rais wetu sio MKALI wengi wanatumia status yake KUIBA; KUTUTENGA; KUTUBAGUA; KUJITAJIRISHA...

  Mfano Mzuri ni Mbunge wa Sasa hivi wa KISARAWE aligombea ili awe Waziri sio kuwa MBUNGE MCHANGIAJI
   
 6. ruhi

  ruhi JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2013
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 683
  Trophy Points: 280
  sisi tuliosoma Minaki tunaona na tunajua mengi sana ya kisarawe kuhusu umaskini
   
 7. K

  Kwetu-Mbagala JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2013
  Joined: Jun 26, 2013
  Messages: 203
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tupo SERIOUS jamani tunamhoji mbunge wetu Mh.Bwanamdogo.Ninaomba wadau wa wilaya ya B'Moyo hasa jimbo la chalinze tujitokeze kuhoji.TUNAMUOMBA Mh.Bwanamdogo (au wapambe/wasaidizi wake) nae ajitokeze ajibu hoja.NINAOMBA habari za Minaki/Kisarawe tuziache kwa muda! Tuna kiu ya majibu ya hoja zetu.Hatuhitaji siasa ktk hili!
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2013
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 9,756
  Likes Received: 4,620
  Trophy Points: 280
  Said Bwanamdogo si aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya fulani Kigoma huko!ataweza kuwa karibu na wananchi wakati ana kazi ingine serikalini?wananchi wa jimbo la Chalinze mjipange tu kutafuta mbadala!nilifuatilia sana wakati wa kampeni ili nijue mustakabali wa Iman Madega maana aliutaka sana Ubunge!nilipofuatilia nikakuta kuna ukabila wa kutisha jimboni Chalinze!wakwere wako wachache sana,wadoe na waziguo ndio wengi zaidi!sasa kampeni zote zinapigwa uziguani ambapo ndipo kuna watu wengi na ndio wanaamua mbunge awe nani!....2015 nadhani ile vita itaanza upya!ule usemi wao wa katumwa na mjomba,hautakuwa na nguvu tena maana ndio silahaya yao ya ziada kila mtu anaegombea cheo chochote ndani ya bagamoyo anatumia silaha ya msaada ya ujomba!!anzia Kawambwa,Bwanamdogo,CCM Wilaya pale na madiwani wengi tu hadi ujumbe wa NEC!napita tu!
   
 9. L

  Lua JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2013
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kingine nasikia huyu jamaa toka achaguliwe afya yake ni mgogoro.
   
 10. M

  Malila JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2013
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,333
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  Huyu bado bwana mdogo hawezi mambo ya kikubwa.

  Halafu Madesa sio kijiji, ni kitongoji cha kijiji cha Kihangaiko.
   
 11. Ntale Wi Isumbi

  Ntale Wi Isumbi JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2013
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pamoja na kuwa mimi sio mkazi wa jimbo la Chalinze, ila namfahamu kwa kiasi fulani Bw. Said Bwanamdogo. Aliteuliwa kuwa DC wa Kasulu mara tu JK alivyoingia madarakani nafikiri mwaka 2006 na baadaye kuhamishiwa Wilaya ya Kondoa mwaka 2009, kabla ya kugombea ubunge mwaka 2010. Kabla ya hapo alikuwa mhadhiri (wa hesabu kama sikosei) CBE kampasi ya Dodoma. Kwa hiyo kutokuonekana kwa jimboni au mjengoni hakuna uhusiano kabisa na majukumu mengine ya kitaifa maana kwa sasa sio DC. Inasemekana jamaa ni swahiba wa karibu sana wa mkulu na hata huo uDC na baadaye ubunge ni takrima kutoka kwa mkulu. Watu wa Kasulu au Kondoa wanaweza kusema kuhusu utendaji wake au ndio mtindo ule ule wa kupeana vyeo bila weledi wa kuitendaji......
   
 12. Ntale Wi Isumbi

  Ntale Wi Isumbi JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2013
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna kipindi nafikiri alikuwa nje ya nchi kwa matibabu (sina uhakika ni nchi gani) kwa muda mrefu tu
   
 13. saronga

  saronga JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2013
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 910
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mbona mnachangia bila kuwa na info za kutosha, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ni yule kilaza mwingine aliyerithi jimbo kutoka kwa dhaifu, anaitwa RAMADHANI MANENO. Bahati mbaya hilo jimbo halijawahi kupata mbunge makini. Wote waliopita hapo ni VILAZA watupu. Nawasikitikia sana wakwere
   
 14. t

  tenende JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2013
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hata yeyealipewa ukuu wa wilaya. Ila 2010 alimgomea JK akitegemea kupewa uwaziri. 2015, CCM watamsimamisha Imani Madega wa Yanga na CDM atasimama Ucheche.
   
 15. K

  Kwetu-Mbagala JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2013
  Joined: Jun 26, 2013
  Messages: 203
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kama mmeshamhukumu mbunge wetu kuwa 2015 hatorejea ktk nafasi yake! Sisi bado tunamhitaji! ILA BADO tunasubiri majibu ya hoja toka kwa mbunge wetu, au wasaidizi/wapambe wake.Natumaini huwa wanapita hapa. Tungependa kujua nini kinaendelea kwa sasa ktk hoja tulizoleta(bila ya kuingiza siasa) na pia kuhusu uboreshaji wa huduma za afya ktk jimbo letu, nazo zipo duni na hazipatikani kwa urahisi.Ninaomba na wadau wengine wa jimbo la chalinze tuorodheshe kero zetu na tusubiri majibu toka kwa mh.mbunge au wasaidizi/wapambe wake.
   
 16. C

  Changamoto2015 JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2014
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 744
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Nadhani majibu sasa unayo kwamba alikuwa ni mgonjwa!
   
Loading...