Sahara Media wamelipa deni lao kwa TCRA: Je, walitakiwa kulipa au kutumikia adhabu?

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,306
Hii habari kwa sisi tusiojua sheria tunabaki njia panda! Deadline ya kulipa ilikuwa Dec 31, 2015, wakashindwa kulipa, wamepewa adhabu mnatuambia wamelipa, huu ni uhuni mnaufanya.

Saa sita TCRA kutoa taarifa ya ambao hawajalipa..

Screenshot_2016-01-20-12-36-10.png
 
Mmiliki Ni Mpiga Debe Wa MAGUFULI, Aliahidiwa Kutosahaliwa Mbele Halaiki Ya WATANZANIA Pale CCM Kirumba 24 Dec 15!! Ahadi Ikitolewa Na M/ Kiti Wa CCM TAIFA Na MGOMBEA Urais Wao (MAGUFULI) Kama Fadhira Ya CHAMA Kwa Mmiliki Wa SAHARA Media, Kwa "KAZI NZURI "
 
Kuna watu hawataona kile anachokisema Gambas kwa sababu zao binafsi, kwa ufupi ni kwamba tunataka nchi iendeshwe kwa taratibu, kanuni na sharia. Hapakua na haja ya kuwafungia miezi mitatu kama walivyotangaza, wangeweka wazi kwamba wanawafungia hadi pale watakapolipa.
 
KUFUNGIWA SIONI TIJA.WAKISHALIPA WAENDELEE ILA WAPEWE ONYO. UKIIFUNGIA MADHARA NI MAKUBWA

Inabidi viongozi wajifunze kutafakari na kupima uzito na hizo athari za matamko yao kabla ya kuwahi kutoa matamko kwanza ndio wanaanza kufikiria matokeo ya hayo matamko.
 
Kuna watu hawataona kile anachokisema Gambas kwa sababu zao binafsi, kwa ufupi ni kwamba tunataka nchi iendeshwe kwa taratibu, kanuni na sharia. Hapakua na haja ya kuwafungia miezi mitatu kama walivyotangaza, wangeweka wazi kwamba wanawafungia hadi pale watakapolipa.
Samaritan watu hawawezi kuona kwa sababu wamezoea kuvunja sheria, kwasababu kama wanaweza kulipa muda wowote basi TCRA hawakuwa na justification ya kutoa adhabu ya miezi mitatu kwa hawa jamaa kushindwa kulipa dec 31 ambayo ndo ilikuwa deadline
 
Inabidi viongozi wajifunze kutafakari na kupima uzito na hizo athari za matamko yao kabla ya kuwahi kutoa matamko kwanza ndio wanaanza kufikiria matokeo ya hayo matamko.

Hata wewe ndiyo unapaswa utafakari kabla haujaandika! Unajuaje kama hilo TAMKO la kufungiwa ndilo lililowafanya walipe hilo deni kwa haraka?
 
Mimi nimetafakari, kumbuka madhara ya kauli yangu na kauli ya serikali yanatofautiana. Kulikua na haja gani ya kusema wanawafungia miezi mitatu? ingetosha kututangazia kwamba wanafungiwa hadi watakapolipa, hiyo ingeleta tatizo gani?
 
Sioni tatizo lako liko wapi! Nafikiri unaumwa ule Ugonjwa wa Kitanzania wa pinga pinga ili tu na wewe uonekane umechangia kitu!
Lengo lilikuwa ni kwamba wadaiwa walipe Deni, ni mbinu gani anayedai anatumia kupata fedha yake siyo ishu hapa, kila mtu ana mbinu yake na hii ni Dunia nzima, hata kama Benki inakuda huwa inakutisha kwamba usipolipa mpaka siku fulani tutauza nyumba yako ingawaje kiuhalisia hata kama hiyo siku ikipita hawatauza nyumba yako bali wanataka kukushinikiza ili ulipe na ndivyo TCRA walivyofanya, sasa ungekuwa na hoja kama deni lisingelipwa halafu dead ikapita lkn Deni limelipwa hivyo hapo hamna cha kulalamika tena, na hii ni Dunia nzima!
 
Unalinganisha madeni ya saccos na maswala ya kisheria na kikanuni!
 
Kumbuka sio suala la ugonjwa hapa, ni ukiukwaji wa taratibu na sheria.
 
Unalinganisha madeni ya saccos na maswala ya kisheria na kikanuni!

Ni sheria gani iliyovunjwa na TCRA hapo? Hata Benki kubwa kama IMF au Benki ya Dunia hufanya hivi kama wanakudai watakwambia mpaka siku fulani uwe umelipa deni la sivyo tutafanya abc aidha tutakuondolea sifa ya kukopesheka au adhabu nyingine yoyote na lengo kufanya hivi ni lile lile kama TCRA kukushinikiza Ulipe, sasa sijui tatizo lako liko wapi?!
 
Nafikiri watu hawajui taratibu za kodi. Hata kama umechelewa kwa mda uliopangwa haiwi sababu ya kukufungia kama uko tayari kulipa. Na likitoka tangazo la kukufungua halafu ukajisarimisha kwa kulipa au kwa makubariano fulani hilo tangazo hufa hapohapo. Hakuna sheria ya kodi kandamizi kama watu walivyokuwa wanafikiria. Tulizungumza humu kuwa hawawezi kufungiwa watu wakaendelea kuwa mihemuko ya kisiasa kwenye issue zisizo za kisiasa.
 
Sina huwo Muda!
Ukiunganisha na kauli ya JPM katika viwanja vya furahisha ni dhahiri kua hawawezi kumfungia Anton Dialo. Mamlaka ilitingisha kiberiti kuona kama kimejaa au la kesho yake mzee mwenyewe Anton Dialo akaruka hewani na kusema wametudhalilisha. Mpaka sasa RFA iko hewani na watangazaji wake wanasema tunaendelea... RFA RFA bado tuko hewani.

Uzuri ni kwamba walitoa ufafanuzi kwa nini wamechukua maamuzi ya kuwafungia na sikwamba wakilipa hawatafungiwa. Dealine ilikua Tareh 31 Dec. wenyewe walijitetea kua adhabu ni halili yaho.
Sasa kwa kua watanzania kwa kuongea ni mabingwa subiri utasikia utetezi... oh sisi tulimaanisha hivi ohh ohh hatuogopi mtu.. utetezi kibao.

Hapo ni goli la wazi kwa serekai ya JPM.
 
Back
Top Bottom