Safari zisizosahaulika

Safari zisizosahaulika

Billen

New Member
Joined
Oct 23, 2018
Posts
4
Reaction score
6
Habari za jioni wana forum.

leo ningependa tusimuliane machache kuhusu safari na ugumu wake.

kuna mwaka nilienda katika harakati za kutafuta rizki mkoani hapo.
Nilienda lkn mambo hayakuwa kama nilivyoyatarajia basi nikawa nipo kwenye process za kurudi mjini.siunajua ile kauli ya mgeni njoo mwenyeji apone nami nikawaa nadumisha ile kauli.nikawa nipo busy namanunuzi mwenye kuniambia niletee shuka ya kigoma huyu niletee sijuu dagaa za kigoma na mengineyo pasina kusahau wenye kuniagiza madawa ya kienyeji basi nikajikuta kile kidogo nilichokuwa nacho kimeniishia zaidi ya nauli na hela za kujikimu siku mbili huku ni kiwa niko niko tayari kwa safari.

nikiwa na cash kama elfu 40000 na pesa zingine zikiwa kwenye simu (tigopesa).Na kama ilivyo ada yangu huwa sikati tiketi kabla huwa nakata ticket stendi alfajiri ya safari kuepuka mambo ya kupitiwa na usingizi pamoja na changamoto za siti za basi kukaribiana kitu ambacho kinanikera katika mabasi yetu haya. Na hua na target kabisa alfajiri nitapata siti ya mastaff kile cha mwanzo kabisa since ina space ya kutosha, na mpk sasa naendelea na desturi hiyo.

siku moja kabla ya safari nikasema nishangae shangae kidogo mjini nakuaga maeneo yote niliyokuwa napenda kwenda kwenye kijiwe cha kahawa hapo urusi tawi la act kupata porojo na maeneo mengineyo.

kufika jioni nikawa narudi gesti nilipofikia, basi nikiwa ndani ya bajaji kurudi huku nikiwa nachezea simu yangu. mara ghafla bajaji ikipigwa mkono na vijana waliokuwa wanajifanya ni abiria maeneo ya lubengela, mishale ya saa nne na maeneo hayo huwa yanapoa sana majira ya usiku,ukichukulia abiria wa kwenda Kigoma mjini huwa ni wachache sana kama ilivyo hapa mjini usiku abiria wa kwenda posta huwa niwakuhesabika.Basi tukiwa na utulivu dereva wa bajaji akisimama kuwasikiliza hao jamaa, punde tu wale vijana waliokuwa watatu wawili wakawa kama mzaha wanabishana nani ake mbele mara gafla moja akakaa kiti cha mbele akachomoa funguo ya bajaji huku wale wawili wakitoa mapanga nakututisha tuwape chochote kitu.Wakati hayo yanatokea mimi nilikuwa na simu yangu mkononi basi mimi na dereva yule tukawa tumeibiwa pale,

Basi baada ya hayo majanga wale vijana wakatokomea bondeni huku wakiwa wanatutisha . basi safari ikaendelea huku nikimpa pole yule dogo mana alikuwa bwana mdogo. safari ikielekea mjini, tukiwa tumeikaribia gesti nilipofikia nakamueleza yule dogo anishushe lkn akakaidi ombi langu nakuendelea nasafari tena kwa mwendo mkali mpk kituo cha polisi cha kilichopo hapo karibu na stesheni ya kigoma napo ni karibu na nilipofikia kama mwendo wa dakika tano kwa mguu na nilipofikia.

Basi mojakwamoja mpk kituo cha polisi. dogo akanibadilishia ubao kuwa mimi nimeshirikiana na wale wezi kwa madai yake niliforce safari ya huko bila yeye. nikawa nimepatwa na bumbuwazi au tuseme dogo kachanganyikiwa na whole scenario, basi ikiwa ni mzozo na mabishano sikuhusika na dogo akiwa kakazana nami. kwa bahati nzuri afamde tuliyemkuta alikuwa mwelewa na likuwa janki lkn mwenye busara basi nikamuambia mimi si mwenyeji hapo ni mgeni na kesho tu nilikuwa nasafari ya kurudi dsm na nimepanga gesti chini tuu.

Sasa nami nimeibiwa kama yeye. basi tukawa tunazozana mpk saa sita kasoro. mwafaka ukawa ni mimi nikwaonyeshe gesti nilipofikia,basi tukaongozana mpk gesti na baada ya kujiridhisha ni mgeni nikaruhusiwa nikimuacha yule dogo na mapolice wakipambana na hali zao.Nimeshafika gesti simu imeshaibiwa ikiwa na hela kwenye tigopesa.

namba ya simu ya mtu yeyote niliyokariri zaidi ya namba yangu hamna.(jamanj google account nyinyi🧐)basi kujisearch mfukoni nina kama 28000 niliyobkiza nikapiga moyo konde nikasema hiii itanifikishaje dsm!? basi nikiwa niko kwenye mawazo nikapata njia ya kunisaidia kufika nayo nikwakuungaunga, nikisema nitajulia hukohuko stendi.

.Alfajiri imefika nachukua bodaboda nailipa 3000 mpk stendi ya mabasi. nabakiwa na 25000. target ikiwa nifike nyakanazi, hapo naweza kupata lifti ya malori ya wasomali yanayotoka nje. kweli nikapanda basi la takbir linaloenda mwanza kupitia nyakanazi, wakinicharge 22000. Nikabakiwa na 3000 basi kwa ubovu wa barabara na mvua kubwa tulifika nyakanazi kwenye saa tisa alasiri. huku nikiwa na furaha nikajua sasa nimeshafika sehemu salama na safari yenye nuksi imefika mwisho.

Nashuka tu njaa nayo ikiwa inaniuma vby sana nikakutana na wamama wanauza asali hapo nykanazi "baba chukua asali yngu " basi nikajifanya mnunuzi kwakujifanya mnunuzi huku nikiwa na lengo wanilindie mizigo yangu niliyoshuka nayo kwenye basi nikielekea kwenye mgahawa hapo hapo ile 3000 nikaisambua yote.

Basi baada ya kushiba nikarudi kwa wale wamama nakuchukua mizigo yangu kuwa standby kwa lift huku nikiwa barabarani. muda nao ukawa unakimbia mpka kufika saa 11 jioni kupo kimya tofauti na sikuzote .kuuliza why kumedorora hivyo nikaambiwa ni sikukuu za pasaka kwa hiyo magari hayajashusha toka alhamisi ijumaa kuu na leo ni jumamosi nasiku mbili zinazokuja ni pasaka mosi na pili kwa hiyo movement mpk j4 nikaambiwa kama ni lifti labda magari yatokayo kongo nazo nyingi zimeshapita hapo asubuhi.

Nikawa nasubiri huku muda nao ukiwa unaenda kufikia saa 12 nikiwa nimekata tamaa na kupata gari hapo nyakanazi sasa na nyakanazi si pahala salama kulala ukiwa huna kitu basi nikiwa nimeshakata tamaa kuna gari ikajakupaki hapo nikaomba lifti mpk runzewe mana runzewe ina parking kubwa ya magari.

wale wenye lile lorry walikuwa ni wacongoman na walikuwa na gari ya gesi. basi nikawaomba lift, japo mwanzoninwalisita ila baada ya kuomba wakinikubalia lift mpk runzewe,ambako si mbali na hapo masaa matatu mbele nikawa nimefika Runzewe. baada ya kushuka moja kwa moja nikawa na mizigo yangu ambao niliuona kama nimebeba mlima kilimanjaro. Nikawa napita kwenye parking kutafuta kama kuna gari nayoijua labda niombe hifadhi, lkn wapi sikupata huku nikiwa najiuliza usiku utakuwa vipi kwa usalama wa mimi na mizigo yangu!

Mungu si athumani kwa mbali nikaona tanker moja ikiwa na chata ya kampuni ya (barq) ambao ni ya wasomali ambao tunafahamiana sana ikiwa imepark , nikaifuata, baada ya kugonga akashuka tandboy wa ile gari, baada ya kumueleza shida yangu akanambia nimsubiri fmdereva wake. basi toka saa tatu mpk saa tano nikawa niko pale kama mlinzi namsubiri yule dereva.

Alipofika yule dereva akiwa na changudoa wawili huku akiwa amelewa akanipita kama mshale wala hakutaki kunisikia. saa5,30 usk nikawa naranda randa runzewe nikakaa kwenye mgahawa mmoja wa mama wa kisomali nijipumzishe mpk yule mama anafunga mgahawa mimi niko kwenye kile kiti, "baba tunafunga unasubiri nini" maneno ya yule mama, basi nikamuambia yule bi mkubwa nasubiri lift,akanambia kwa usiku ule hapana labda nilale kesho nibahatishe, basi yule mama bila kujua undani wa tatizo langu akanipeleka kwa jirani zake amabo wanagesti hapo, pia niwasomali,kuna kijana aliyekuwa anafanya kazi pale cha kwanza alichonijibu ni vyumba vime jaa.

Moyoni nikiwa na furaha na lile jibu, kuwa kama ni hivyo wanisaidie kuhifadhi mizigo yangu kwenye gesti yao na pia wanipe hifadhi nilale kwenye kiti amabavyo vilikuepo hapo uani.nikiwa, najianda kusema tu akadakia mzee mmoja amabae ni jamaa yao alikuwa nachumba chake hapo gest akinambia kijana njoo, nitakukodisha chumba changu mimi nitaenda kulala msibani. huku akinikabidhi funguo na kuniambia " elfu 10" nilichomjibu tutaonana kesho, nikapokea funguo zile nikalala.

basi asubuhi na mapema nika amka huku nikiwa sijujui nitalilipaje deni la gest. nikakurupuka huku nikiwa nashangaa shangaa barabarani. ghafla nikaona tanker moja ambayo huwa linapaki maeneo ya kwetu. nikajisemea moyoni kama nitamuambia anipe lifti mpk dar kwa hakika atakataa, nikapata wazo kumuambia kuwa anipe lifti mpk kahama mana si mbali sana na hapo hatokataa.

Kweli yule bwana nikamuomba lift mpaka kahama hakunikatalia akanikubalia ,nikamuambia na mizigo yangu naenda kuifata gesti akasema poa nisichukue muda yeye anaenda kunywa chai nifanye haraka,mtihani ukaja nitavitoaje vile vitu bila kulipa hela ya watu.nikajipa moyo konde, kuviendea vile vitu nakumbuka ilikuwa asubuhi mida ya saa mbili kasoro hivi. Mwanzo nilipotoka yule kijana wa reception alikuwa hajaamka. Baada ya kufika nikakuta bado hajaamka na kuko kimya nikatoka navyo kimyakimya ile naurudisha tu mlango, yule mzee mwenye chumba chake huyu hapa anafika.

Nashukuru mungu nilipata ujasiri wa ghafla, huku nikiwa na confidence nikamuambia mzee twende nje nikatoe hela kwenye simu, mzee hakusita ,lengo ni kutoka kwenye himaya yake. Baada ya kutoka nje kujifanya natafuta kibanda cha tigo pesa huku tukipiga hatua kuelekea kwenye gari. Nilipohakikisha gesti iko mita chache nyuma, nikamuambia yule mzee yaliyonikuta, alhamdulilah yule mzee alikuwa mwelewa akaniacha bila kunidai. tukaianza safari sasa na yule dereva mpk kahama.

tulifika kahama masaa manne mbele kabla hatujafika mjini nikambadilishia mashairi kuwa safari yangu ni mpk isaka napo si mbali sana na hapo kahama akanikubalia. ile kauli ya njia ya muongo ni fupi ikawadia baada ya kufika isaka dereva wa lori akapaki. Mzee isaka tushafika shuka uje utoe mizigo yako juu ya tanki, Nikumueleza mzee baba hii safari ni mpk dsm. kilichonifanya nijiamini ni kuwa mtoto wa mmiliki wa hayo magari ni jamaa yangu.

Baada ya kumuambia hivyo huku nikimtisha kuwa kama hatanisaidia ajiandae naye kazi atakosa nikajitapa sana namjua mpk mzee mwenyewe boss nakujinasibu na familia hiyo. Kweli dereva yule alikuwa ni mwenyeji wa singida kwa kubabaika na usomali wangu mana maboss zake walikuwa ni wasomali akakubali kunibeba kwa shingo upande. Tukiwa bado isaka akanambia gari inahitaji matengenezo madogo nishuke nimsubiri kidogo hapo nikatii amri hiyo. Nikawa nipo hapo kwa maelezo yake ataenda na mwenyeji hapo kwenye matengenezo ambako si mbali na hapo. basi nikashuka nikawa namsubiri hapo muda ukazidi kwenda almost 4 hrs jamaa hajatokeza.

Basi namimi nikaingiwa na hafu isije kuwa yule dereva kaondoka jumlajumla nikawa na randaranda kwa mguu kutafuta ile gari maeneo hayo hamadi sinikaikuta iko sehemu imehificha dereva anatoa mafuta kwenye reserve tank. Kuniona alishtukaa. nikamtoa hofu kuwa hayo ni mambo ya kawaida kwenye kazi hakuna kazi isiyokosa maarifa kwa hiyo asijali.

Kweli tuliendelea na safari muda mchache tukiwa kama bubu hakuna la kuzungumza mpk usiku mrefu tukafika manyoni.muda wote huo tulikuwa hatusemeshani hofu yake ikiwa labda nita report tukio lile kwa matajiri zake. Manyoni tuliingia usiku mrefu ikabidi tulale hapo nje ya mji . Kwa sababu gari haikuwa na kitanda ni mende so cabin haikuwa na space ya kutosha akaniacha mimi nilale ndani ya gari. Yeye akachukua chumba gesti moja iko karibu. kweli nikakaa ndani ya gari, sikulala mana utalalaje na njaa ya kutwa nzima nikawa napanda na kushuka kwenye gari mpk alfajiriilipofika yule dereva alipofika, ile anafungua tu gari mimi huyu hapa baada ya kusalimiana nikagundua yule bwana alikuwa amekunywa pombe usiku wake. akajua labda atakapokuwa anaingia kwenye gari atanikuta nimelala basi baada ya kugundua hilo yule bwana akajawa na hofu zaidi mana matajiri wengi huwa wanachukizwa na madereva walevi na ile inccedent ya kuiba mafuta yule bwana alikuwa na hofu zaidi.

Nikasema bila kutumia akili ya ziada nitakufa njaa kufika nitafika lkn nisije kufika nimekufa njaa maana shilingi moja sina? basi tukaingia kwenye gari tukiendelea na safari , huku mimi nikiwa napiga story mara za lissu mara za kibiti lkn jamaa yangu wala hayuko intrested, mwisho nikaja na story za kulaumu kwanini jana alienda kunywa pekee yake basi yule dereva kidogo akawa ananiuliza kwani nawe unakunywa nikamuambia mbona ni mlevi mzuri tuu tena kwa safari lager ni hatariii. Akawa haniamini mana kwa sisi wasomali kutukuta tunakunya pombe ni aghalabu. Basi tukatembea mpk dom tukapata lunch nzito na bila kusahau na safari za kutosha mana nae alikuwa ni mpenzi wa safari.

Basi toka hapo ikawa ni mwendo wa gear na beer tukarudisha tena story za kina Lissu mara za man u mana yule jamaa alikuwa ni mpenzi wa man u na yanga na mimi ni arsenal na simba lkn ikabidi ni pretend kuwa nami nazipenda yanga na man U , si unajua tena mambo ya kitongo nisije nikaleta upinzani nae mwisho tukawekana njaa kutwa nzima. Basi Mungu alijaalia tukafika salama mpk mjini DSM.
 
Hahahahaha msomali bhana story yako nzuri ila ndefu kwenye maandishi na pia ulipoharibu ni hapo tu kwenye Lager.

Pole sana kwa kuibiwa huko kwetu,Dah umenikumbusha maeneo mengi sana Nyakanazi,Runzewe,Kahama,Isaka,Tinde na kuendelea barabara hiyo hailali aisee.
 
Hahahahaha msomali bhana story yako nzuri ila ndefu kwenye maandishi na pia ulipoharibu ni hapo tu kwenye Lager.

Pole sana kwa kuibiwa huko kwetu,Dah umenikumbusha maeneo mengi sana Nyakanazi,Runzewe,Kahama,Isaka,Tinde na kuendelea barabara hiyo hailali aisee.
boss nimeshapoa kuhusu uandishi mimi c mzuri sana, maana hizo fani zina wenyewe.
cha muhimu hapo nikushare na wenzangu mawili matatu.
mana waha wanasema "umugabho afa agenda"
ulakoze chane
 
Hahahaha nilichomaanisha ni kuwa story yako kwenye maandishi lazima iwe ndefu haifupishiki.

Yap hata mm nshasafiri kwa mfumo huo japo mm nilikuwa na hela sema Nilipandaga Saratoga ikachelewa kuingia kahama na mm nikasema siwezi kulala kahama wkt nina bro nzega so nikacukua boda boda kahama-tinde then nikapanda scania hadi nzega,nikaweka kituo.
boss nimeshapoa kuhusu uandishi mimi c mzuri sana, maana hizo fani zina wenyewe.
cha muhimu hapo nikushare na wenzangu mawili matatu.
mana waha wanasema "umugabho afa agenda"
ulakoze chane
 
Hahahaha nilichomaanisha ni kuwa story yako kwenye maandishi lazima iwe ndefu haifupishiki.

Yap hata mm nshasafiri kwa mfumo huo japo mm nilikuwa na hela sema Nilipandaga Saratoga ikachelewa kuingia kahama na mm nikasema siwezi kulala kahama wkt nina bro nzega so nikacukua boda boda kahama-tinde then nikapanda scania hadi nzega,nikaweka kituo.

imagine tu mtu hana nauli ya kurudi tu kwake akitokea posta ama gerezani jinsibanavyo haha halafu kuna wengine wanasafiri mkoa to mkoa hana kitu unaonaje??
hapo ndo ile kauli ya mguu uliotoka umebarikiwa inapofanya kazi
 
Du, hongera kwa harakati. Mie nakumbuka 1984 nikiwa na miaka 7 hv tulitembea kwa mguu kutoka Paradiso hadi AMAN makoro Masaa zaidi ya 7, likapita gari la RC Ruvuma miaka hiyo Gama Mutazama Range Rover ya kijani, ikapigwa mkono, DER kanyoosha. Kumbe DER na baba walifahamiana lkn katii mamlaka. Aliitwa Swalaswala, Waliende MBELE zaidi ya km moja HD mngurumo hausikiki. Mie nikiwaza dah nami ningeenjoy kupanda gari kali, mtaani ningetisha sana. Ghafla nikaona ile gari inarejea tena. Baba kajuuliza kuna nini?? Mie hata sijui. Kumbe wale wakubwa walivyokwenda baba alinibeba began I mie niichoka sana, sasa RC alianza kuongea na DER wake yule jamaaa lazima ana mpango wa kujitahidi HD kitai, DER kamchomekea kuwa yule ni mtumishi wa pale pale Ofsn kwako, RC akajawa na huruma, ndipo wakarejea kutuchukua. Kiukweli badala ya kulala kitai pale Magereza tukajikuta lizaboni Songea. Nilikuwa narejea Mjini ili niweze kuandikishwa DM kule bush walimu walikomaa kwa mkono haukufika sikioni. Kitambo sana. Songea nikafanikuwa kuanza std 1 1985.
 
Nipo Kahama.Ungeshuka nikupeleke home kwangu kesho yake nikupandishe Kisbo kuliko kuhangaika na lori.
Next tym ukipata janga kama ilo drop Kahama hapa
 
boss nimeshapoa kuhusu uandishi mimi c mzuri sana, maana hizo fani zina wenyewe.
cha muhimu hapo nikushare na wenzangu mawili matatu.
mana waha wanasema "umugabho afa agenda"
ulakoze chane
Nampole chane
 
Du, hongera kwa harakati. Mie nakumbuka 1984 nikiwa na miaka 7 hv tulitembea kwa mguu kutoka Paradiso hadi AMAN makoro Masaa zaidi ya 7, likapita gari la RC Ruvuma miaka hiyo Gama Mutazama Range Rover ya kijani, ikapigwa mkono, DER kanyoosha. Kumbe DER na baba walifahamiana lkn katii mamlaka. Aliitwa Swalaswala, Waliende MBELE zaidi ya km moja HD mngurumo hausikiki. Mie nikiwaza dah nami ningeenjoy kupanda gari kali, mtaani ningetisha sana. Ghafla nikaona ile gari inarejea tena. Baba kajuuliza kuna nini?? Mie hata sijui. Kumbe wale wakubwa walivyokwenda baba alinibeba began I mie niichoka sana, sasa RC alianza kuongea na DER wake yule jamaaa lazima ana mpango wa kujitahidi HD kitai, DER kamchomekea kuwa yule ni mtumishi wa pale pale Ofsn kwako, RC akajawa na huruma, ndipo wakarejea kutuchukua. Kiukweli badala ya kulala kitai pale Magereza tukajikuta lizaboni Songea. Nilikuwa narejea Mjini ili niweze kuandikishwa DM kule bush walimu walikomaa kwa mkono haukufika sikioni. Kitambo sana. Songea nikafanikuwa kuanza std 1 1985.
Mkuu kiswahili Hujui au? Mbona hueleweki?
 
Mimi mwaka 2015 nilikua Kigoma kikazi wakati wa uchaguzi mkuu eneo la Kibondo. Uchaguzi ilipoisha nikaenda Kigoma mjini kula bata kidogo kabla ya kurudi mjini Dar.
Sasa siku nataka kuondoka hakukua na gari hata moja na sikua nataka kuendelea kukaa Kigoma tena maana nilitumia gharama kubwa sana kwa bata kule pub za ziwani. Basi nikaunga safari mpaka Nzega, kufika napo hamna usafiri kabisa maana ilishafika jioni. Nikaomba lift ya magari ya mafuta, ila dereva akataka malipo tukakubaliana safari ikaanza. Bwana gari inatembea taratibu yaan kuja kuiona Singida usiku wa manane, tukalala kwenye gari. Kesho yake safari ikaendelea, kufika Morogoro gari ikaharibika na hela nishatoa. Dereva anasema tusubiri hadi kesho yake gari ikishatengenezwa tuanue. Nikamwambia atanisamehe tu nikapanda bus pale mida ya jioni nimekuja kufika Dar saa nne usiku. Kwa uchovu wa ile safari sikunyanyuka kitandani siku mbili nafanya kuagizia chakula na kujikokota kwenda chooni tu
 
Back
Top Bottom