Safari za Rais John Magufuli nje ya nchi tangu aingie madarakani 2015

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,635
29,509
Wadau,

Kama mjuavyo Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kusafiri nje ya nchi kwa mara ya kwanza kwenda Nchini Rwanda hapo kesho kukutana na na Rais Paul Kagame wa nchi hiyo. Hii ni safari ya kwanza toka atangazwe na NEC kuwa mshindi kutokana na uchaguzi uliofanyika October 25, 2015.

Uzi huu utakua maalum kwa ajili ya kurecord safari za nje ya nchi za Mh. Rais, pamoja na siku atakazokua amekaa ili kuweka tu kumbukumbu sawa.

Pia itapendeza kama wahusika watakua wanatoa gharama ya safari na faida tutakayopata ili tujue tunasogea kwa kwenda mbele au kurudi nyuma.

Safari ya Kwanza, Tar 06-Apr '16- Rwanda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kwa kutembelea nchi jirani ya Rwanda, yeye na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mh Paul Kagame wamefungua Kituo cha Pamoja cha Utoaji wa Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) na Daraja la Kimataifa la Mto Rusumo katika Mpaka wa Tanzania na Rwanda.

Safari ya Pili, Tar 11 May '16 - Uganda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Jijini Kampala nchini Uganda ambapo na kesho anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni.

Safari ya Tatu, Tar 31-Oct '16 - Kenya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, anaanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Pamoja na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta Ikulu Jijini Nairobi
Pia anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.

Rais Magufuli anatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 01 Novemba, 2016 na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Safari ya Nne, Tarehe 28-Jan '17 - Ethiopia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28/01/17 ameondoka nchini kuelekea Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi za Africa (AU). Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Rais nje ya Africa Mashariki toka aingie madarakani.

Safari ya Tano, Tarehe 09-Nov '17 - Uganda,
Rais John Magufuli wa Tanzania yuko nchini Uganda kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais Museveni mpaka wa Mutukula.Hii ni mara yake ya pili Rais Magufuli kufanya ziara nchini Uganda.

Rais hao wawili wameweka jiwe la msingi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. Bomba hilo litakuwa na urefu wa kilomita 1444, kilomita 296 zitakuwa Uganda na linatajirwa kusafirisha mapipa ya mafuta 216,000 ya mafuta ghafi kila siku.

Safari ya Sita, Tarehe 21-Feb '18 - Uganda,
Rais John Magufuli ameondoka leo, Jumatano kwenda nchini Uganda kushiriki Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Kampala.
 
Hope amejaza fomu ya kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi na kuainisha gharama za safari hiyo, faida ambazo taifa litapata kwa kusafiri na hasara kwa taifa kama hatasafiri
 
Hivi hapa watu wanapenda nini? Nafikiri ukiweka kichwa cha habari lowasa au mbatia kuna watu wataongea mpaka wasivyo vijua na watakuja na ushahidi wa uongo kweli ! Na wengine watasema weka picha. Watanzania tumelogwa na aliye turoga yupo meru anatengeneza viroba
 
Wadau,

Kama mjuavyo Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kusafiri nje ya nchi kwa mara ya kwanza kwenda Nchini Rwanda hapo kesho kukutana na na Rais Paul Kagame wa nchi hiyo. Hii ni safari ya kwanza toka atangazwe na NEC kua mshindi kutokana na uchaguzi uliofanyika mwaka jana October 25.

Uzi huu utakua maalum kwa ajili ya kurecord safari za nje ya nchi za Mh. Rais, pamoja na siku atakazokua amekaa ili kuweka tu kumbukumbu sawa.
Karibuni!!

Amesha tuambia safari hii tanzania itafaidikaje? Kama Rais mwingine alisha wahi kwenda kwa nini kunamuhimu kwenda tena? Maana hivi ni baadhi ya vigezo alivyoweka kwa mtumishi wa umma kueleza kabla hajapata kibali kusafiri nje ya nchi.
 
Wacha aende, ninamuunga mkono maana ninaamini ana mengi sana ya kujifunza kutoka kwa Kagame.
 
Wadau,

Kama mjuavyo Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kusafiri nje ya nchi kwa mara ya kwanza kwenda Nchini Rwanda hapo kesho kukutana na na Rais Paul Kagame wa nchi hiyo. Hii ni safari ya kwanza toka atangazwe na NEC kua mshindi kutokana na uchaguzi uliofanyika mwaka jana October 25.

Uzi huu utakua maalum kwa ajili ya kurecord safari za nje ya nchi za Mh. Rais, pamoja na siku atakazokua amekaa ili kuweka tu kumbukumbu sawa.
Karibuni!!
Atatumia usafiri gani?

kwa nini safari ya kwanza ya mh. raisi wetu imekuwa Rwanda kulikoni?
ngoja tusubiri tuone nini kitajiri.
 
Back
Top Bottom