Safari yangu na Mnyika, Buriani Mzee Dalali

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
377

Na. Mtemi Wa Wanatta
·
John Mnyika, na safari yetu, Mungu akupe faraja.
Dunia inazunguka sana, leo nimetulia saa kadhaa nimejaribu kukumbuka safari yangu ya kisiasa, tangu 2005 May. nikakumbuka zile safari za miguu toka mtaa hadi mtaa tukiwa na kaka yangu, raifki yangu, na mwalimu wangu wa kisiasa John Mnyika
Lakini nikakumbuka sana mapito magumu ya safari hiyo yaliyokuwa yamejaa uvumilivu na kujitoa kwa moyo
Nikakumbuka siku moja tulitembea tokea mabibo mpaka kimara kampeni za mtaa kwa mtaa, tulienda mpaka mbezi mwisho,
Sikuishia hapo nikakumbuka siku matokeo ya uchaguzi ule yalipotangazwa Mzee Keenja akiwa ameshinda
Nilichojifunza ni namna ambavyo Mnyika hakukata tamaa kabisa na aliongeza ari ndani ya utumishi wa chama mpaka 2010 alipoibuka mshindi.

Bado tafakari yangu ikanikumbusha uchaguzi wa vijana wa taifa chadema ulivyogubikwa na sarakasi
Nikakumbuka Jinsi Marehemu Chacha Wangwe alivyokuwa akitaka kuondoa taswira ya chadema kuwa chama cha mtu na kukifanya taasisi, kipindi hicho Chacha Okong'o na akina Mzee Lichonyo na Marehemu Shelembi wakiwa wasimamia misingi ya chama aliyoipigania Marehemu Zakayo Chacha Wangwe
Nikakumbuka kipindi hicho Zitto Kabwe akiwa mwanamikakati wa Mwenyekiti mbowe kuhakikisha Chacha wangwe hakatizi
Lakini pia nikakumbuka zaidi baada ya kifo cha Wangwe fikra zake hazikupotea bali zilimnasa zitto na wengine wakageuka na kuona umaana wa aliyokuwa akiyapigania Zakayo Chacha WangweWakaanza kupambana na hali hiyo
Lakini nikakumbuka zaidi hili lilivyowagharimu mpaka kufukuzwa kwao uanachama huku Dr Slaa akiwa mtendaji mkuu wa chama na pengine msimamizi wa utekelezaji huu wa kuwafukuza uliokuwa umeandaliwa kiufundi na Mbowe,
Lakini jicho langu la tabasamu likatazama namna tulivyopambana kuhakikisha tunabaki ndani ya chama hicho na hawa akina zitto lakini ikashindikana, na sasa wanafanya siasa katika vyama vingine

Pumzi nzito nilipokumbuka siku nimeambiwa kwamba Dr SLAA sio mwanachama tena ameandika barua ya kuondoka kabisa uanachama
Nilipokuja kumuona Mzee Lowassa anatangazwa kupokelewa na kugombea urais kupitia chadema, nilijikuta hatokwa jasho la hamaki
Nikamtazama rafiki yangu na rafiki yangu sana tu licha ya utofauti wa kisiasa JJ Mnyika na nikajikuta naiambia nafsi yangu, pole brother, kumbuka uliniashauri niwe mvumilivu sana, hasa ninapogundua kuwa kuna kundi nyuma yangu linanitazama ili liamue
Salaam za pole ya kuondokewa na Mzazi wako mpendwa Mzee John Dalali, pole sana kaka, Mungu akupe uvumilivu na utulivu katika vipindi hivi vigumu

Ushauri kwa vijana wenzangu

Usimchukie mtu kwa sababu za utofauti wenu kwa kisiasa, siasa ni maji yenye mwendo mbele na nyuma, leo utamuona kiongozi fulani anafaa sana, lakini kesho mambo yanaweza kugeuka na ukajikuta unayumba sana

Miongoni mwa mambo ambayo sijawahi kufanya ni pamoja na kumchukia mtu kisa vyama vyetu, ila huwa ninafanya kazi kubwa ya kuzikataa itikadi na falsafa za vyama visivyo vyangu, ila utu na ubinadamu wa mtu unabaki pale pale

Rafiki zangu toka vyama vyote wataendelea kuwa vilevile na thamani yao kwangu itabaki vile vile, ila linapokuja suala la itikadi za vyama na imani zetu hatuko pamoja kabisa
Nitasema ccm oyee...na wao watasema vibwagizo vya vyama vyao...
Nitadumu kuwa Mjamaa na wao watabeba itikadi zao

Mnyika Mungu akuongoze upate wakati wa kutulia na kutafakari hatima yako kama kijana na familia yako, taifa letu na mengine
Asante sana, Mungu ailaze Mahala pema peponi Roho ya Marehemu Mzee Dalali.
 
Mbowe ndio ameivuruga kabisa CHADEMA.. kitendo cha kumuuzia Lowasa Chama na kumfukuza dr.slaa ni usaliti wa mageuzi na upinzani... sasa hivi Chadema imepoteza dira.na muelekeo..muda si mrefu kitabaki historia..kiufupi Chadema imeshapotea kwenye ramani ya vyama vya siasa.
 
Pole sana Mnyika! Uko vizuri sana ingawaje umepotea njia kuingia chama cha Mafisadi ni imani yangu utajurudi sasa ! Hata hivyo pole sana na Mungu akuonyeshe njia hasa kipindi hiki cha mfungo na mwishowe utoke chadema!
 
ukweli mtupu. Chadema ilibugi sana kwenye zile fukuza fukuza zao wa wasaliti wa kubuni.
 
Haya tuletee na hadithi za Ccm au huko huna unachokijua? Tuelezee watu Kama kina Kambona,Kombe,karume,Jumbe,Sokoine.... etc. Wao mamboyqo yalikaeje kaeje ama mtoamada alikuwa mtoto asojua lolote!
l
 
Mbowe ndio ameivuruga kabisa CHADEMA.. kitendo cha kumuuzia Lowasa Chama na kumfukuza dr.slaa ni usaliti wa mageuzi na upinzani... sasa hivi Chadema imepoteza dira.na muelekeo..muda si mrefu kitabaki historia..kiufupi Chadema imeshapotea kwenye ramani ya vyama vya siasa.
kamuulize wassira kama cdm hipo ama aipo?
 
Back
Top Bottom