Safari ya Rais JK, USA

Safari ya Rais JK, USA

malipesa2014

Member
Joined
Jun 2, 2014
Posts
22
Reaction score
8
Mkuu wa nchi anaposafiri kwenda popote pamoja na delegation yake kikazi, pia huwa anabeba waandishi wa habari ili kuujulisha umma yale yanayotokea huko. Lakini iko tofauti kwa waandishi wetu wanaoambatana na JK, maana kwao imekuwa kama ni vacation au picnic.

Coverage ya President imekuwa so shallow and poor, ilhali wao wakiwa busy kutupia kwenye facebook na instagram picha za matukio yao binafsi - just to show off their experience on the trip!

Nawasihi wenzetu hawa wajitahidi kutuma picha na habari za kutosha kwa watanzania wenzao ambao wana shauku kubwa ya kujua kile kinachoendelea huko aliko Mh. Rais. Watambue kwamba kutuma clip moja ya video na picha mbili, haitoshi!

Hiyo safari imesheheni mambo mengi ya msingi kwa mustakabali wa nchi yetu. Sina imani kwamba dhumuni kuu la safari ya rais ilikuwa ni kukutana na watanzania walioko huko tu, thats a very minor fraction for the whole purpose of the trip. Lakini maripota hawa wamekazania kuripoti mambo ambayo ni mepesi mepesi tu ukilinganisha na uzito wa safari yenyewe iliyojumuisha wakuu wa nchi za Africa 50, pamoja na Marekani yenyewe.

Hebu changamkeni ndugu zetu kuuhabarisha umma wa watanzania yale yanayojiri kwenye hiyo safari kwa manufaa ya nchi yetu. Uandishi mahiri sio kuji show off, bali ni kuwa kiungo muhimu cha yanayojiri kwa walaji wa habari.
 
Hakuna la maana analoenda kufanya huko sasa unataka waripoti uharo wa hizo trip.
 
Kiongozi kalikoroga la Rasimu ya Katiba ameona akapotezee huko dhambi ya kudharau maoni ya watanzania na kuteketeza fedha za walala hoi zilizotumika kuandaa rasimu na kuendelea kuwalipa wajumbe Wa bunge LA katiba anayo
 
Back
Top Bottom