City Hunter 1922
Member
- May 5, 2017
- 94
- 32
Mara baada ya sakata la Uongozi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kutaka kumshughulikia kijana mzalendo ambaye ni Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho kwa kile ilichosema ni kosa la Kiongozi huyo kutuma malalamiko yake Wizarani. Baada ya wanyetishaji kudaka barua alizotuma Rais huyo ikabainika kuwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dr. Bhaskara Raju alitaka kutumia tukio hilo kumtengenezea mashtaka Rais huyo kwa lengo la kumfukuza Chuo kupitia sheria ndogondogo za Chuo hicho.Rais alikuwa anaikumbusha Wizara na Ofisi ya PM kuwa ni mwaka mzima tangu Serikali ya wanafunzi iliyomtangulia iliporatibu mgomo na MwanaFalsafa waraka ulioambatanisha kero zote za msingi wanafunzi wa Chuo hicho lakini mpaka sasa yapo baadhi ya matatizo hayajatatuliwa na hakuna dalili za kuyatatua! Waraka huo ulitupiwa humu mwaka jana! Baada ya nyeti hizo kunifikia nikachimba niliyochimba nikayaleta hapa kuhusu huyu Dr.Bhaskara Raju.Kwa kifupi walipoona waliogopa kuendelea na mipango yao ya kumfukuza Rais huyu jasiri.Leo mnyetishaji wangu amefanikiwa kuwadaka akina Dr. Bhaskara Raju wakifungua barua aliyotumiwa Rais huyu na Ofisi ya Waziri Mkuu wa JMT huku wakijua ni UHAINI kuingilia mawasiliano kati ya PM na Kiongozi huyu wa wanafunzi wa St. Joseph. Mnyetishaji alifanikiwa kuipiga picha barua hiyo na nitaileta hapa maana haina maudhui mabaya yatakayoiumiza serikali yetu njema.TCU ni muda wa kushughulikia kikamilifu tatizo namba la waraka ambalo ni UONGOZI MBOVU unaoharibu sifa za Chuo hicho.Mkishatumbua kaeni na wanafunzi mjue uongozi wa Chuo hicho utabadilishwaje ili kumaliza tatizo hilo once and for all! Tumbua Dr. Bhaskara Raju... Tumbua na yule Dean wao muhindi wanayemtegemea kukandamiza serikali ya wanafunzi jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya vyuo vikuu! TUMBUENI HAYA MAJIPU KABLA HAYAJAWAGHARIMU KAMA YALIVYOWAGHARIMU WATANGULIZI WENU. Muda ni sasa.
Yours loving,
CITY HUNTER
(KIJANA MTIIFU WA JPM KTK KUTUMBUA MAJIPU)
Yours loving,
CITY HUNTER
(KIJANA MTIIFU WA JPM KTK KUTUMBUA MAJIPU)