utiyansanga
JF-Expert Member
- May 19, 2010
- 213
- 7
naona wewe umetumwa padri aoneshe huruma kwa wanaodai haki.!nyie wanufaika na uozo na mafisadi siku yenu inakuja
Mwanasheria wa CHADEMA, Mabere Marando amewasilisha rasmi NEC barua ya kupinga matokeo.
Hatua zilizochukuliwa/tutakazochukua ni:
1. Kwenda NEC - (barua imewasilishwa jana)
2. Tunakwenda kueleza Nchi wahisani ambazo zimefadhili shughuli za Uchaguzi
3. Tunakwenda kuwaeleza wananchi kilichotokea kwa kuwaonyesha ushahidi kamili.
4. Dk. Slaa amepanga kuwakilisha ushahidi MZITO unaoonyesha uchakachuaji mkubwa wa kura za Urais ulivyofanyika. Ushahidi huo ni pamoja na matokeo halisi ya vituoni yenye saini za mawakala ambayo yanapishana na yale ya NEC.
Marando alisema hadi juzi Jumatatu matokeo ambayo tayari walikuwa wamekusanya kutoka katika maeneo mbalimbali ya Nchi, yanaonyesha Mgombea Urais wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa anaongoza kwa wastani wa asilimia 61.6%.
My take; Mahakamani je?
OH NOW I SEE, kaka umenifungua macho
Chama chochote kina uhuru wa kukataa ama kukubali matokeo kulingana na maslahi inayopata. Hivi sasa ccm inaitumia cuf kukandamiz haki za watu wa tanzania bara. Hebu fikiria tokea kinana alipokurupuka kutangaza idadi ya viti vya ubunge hakuna mkurugenzi aliyethubutu kuruhusu matokeo yanaoonyesha chadema kushinda viti zaidi vya ubunge. Hizo ni njama za kuhakikisha kuwa cuf inakuwa kambi ya upinzani katika bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania kwa kupata viti 24 vya ubunge ambapo 22 kati ya hivyo nji vya pemba; na kuizidi chadema yenye viti 21 vya watanzania bara.
.
Lengo la kupinga si kwa uchaguzi huu tu bali mpango mzima wa chaguzi zijazo pia, bila kurekebishwa sasa mambo yatajirudia uchaguzi ujao.