Nikukumbushe
JF-Expert Member
- Jun 4, 2013
- 2,602
- 409
Salamu!
Kwa wale wana ccm waliolewa madaraka kama Nape Nnauye,Mwigulu Nchemba,Januari Makamba na wengine wenye hulka kama hawa.Kwanza nawapa pole kwa kauli zenu za kiuudhi,kejeli na dharau,hii dhahiri kuwa mmelewa madaraka ya kupewa kwa migongo ya baba zenu au rafiki zenu.
Napenda kutoa ushauri tu kwenu kuwa,kauli zenu za kejeli,dharau na kuudhi zitawagharimu kwani ninyi kama vijana SAFARI YA KISIASA KWENU BADO NI NDEFU.
Mmekuwa mkitoa kila aina ya kauli za matusi,dharau na kejeli kwa wapinzani na watu wengine kwa kuwa mpo katika chama tawala mkilindwa na dola,lakini angalieni sana.Ninyi bado ni vijana na mna nafasi kubwa sana ya kulitumikia taifa hili la Tz,sasa mnapojikita kutukana,kukujeli na kudharau upinzani wakati hatujui mimi na wewe kesho tutakuwa wapi kisiasa huku ni kujichimbia kaburi.
Punguzeni ulevi wa madaraka,umri wenu bado mdogo sana hivyo hamjui kesho mtakuwa wapi kisiasa.Epukeni kauli za kuudhi na dharau,tafakarini kesho chama gani kitakuwa tawala huku mkiangalia nafasi zenu kisiasa hapo baadae.
Siasa sio uadui bali ni ushindani wa hoja.Ni ushauri wangu tu.