Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
KAULI ya mkuu wa jeshi la polisi nchini, Simon Sirro, kuwa mwa ndishi wa habari, Silas Mbise, aliyepigwa na askari polisi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, alishambuliwa kwa kuwa aliingia kwenye eneo ambalo halifuhusiwi, haikubariki na imelenga kutetea uhalifu nchini.
Hii ni kwa sababu, ndani ya uwanja wa taifa hakuna mahali kokote ambako kumepigwa marufuku waandishi wa habari kufika.
Aidha, mwandishi aliyepigwa alikuwa yuko kazini- kama ambavyo polisi walikuwa wakifanya kazi zao- kitendo cha kumshambulia; na au kumzuia kufanya kazi zake, ni uvunjifu wa katiba.
Hivyo basi, hatua ya Sirro kutetea kitendo cha askari wake kupiga mwandishi, kinapaswa kujibiwa mara moja na waandishi na wahariri kwa kuchukua hatua ya kutangaza, kuchapisha, kusambaza na kupiga picha, habari zote zinazomhusu Sirro na jeshi lake kwa ujumla.
Kwani hiyo ndio silaha pekee ya waandishi ambayo tumekuwa tukiitumia kwa miaka nenda rudi.