SADC yataka DR Congo kuunda Serikali ya Muungano

SADC yataka DR Congo kuunda Serikali ya Muungano

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,607
Muungano wa maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC, umetoa wito wa kuundwa kwa serikali ya muungano nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia mzozo uliokumba matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi uliyopita. Tangazo hilo limetolewa kupitia taarifa ya rais wa Zambia Edgar Lungu.

eba4a1d2c3ba62ce7671d22870757de9

Kwa mujibu wa BBC, Afrika Kusini pia inaunga mkono wazo la kubuniwa kwa serikali ya muungano.

Hatua hii ya SADC inakuja siku moja baada ya mgombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu uliyofanyika nchini Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo amewasilisha kesi katika mahakama ya katiba kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

Martin Fayulu amesisitiza kuwa alishinda uchaguzi huo lakini tume ya uchaguzi ikamtangaza mshindani wake Felix Tshisekedi kuwa mshindi.

Rais wa Zambia, Edgar Lungu, amesema kuwa wamezingatia “mvutano mkali uliyoibuka” kupinga matokeo ya awali.

eba4a1d2c3ba62ce7671d22870757de9-1

Amesema viongozi wa kikanda wanaonelea njia mwafaka ya kusuluhisha mzozo huo ni kupitia muafaka wa kisiasa ambao utatoa nafasi ya kuundwa kwa serikali ya muungano wa kitaifa.

Bwana Lungu alitoa mfano wa mwafaka wa kisiasa uliopatikana nchini Zimbabwe na Kenya.

Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini,Lindiwe Sisulu, anapendekeza mchakato wa kisheria ufuatwe DRC kuhusiana na suala hilo huku akitoa wito kuwa watu wa nje wasiwalazimishe Wacongo jambo ambalo hawajaridhia.

eba4a1d2c3ba62ce7671d22870757de9-2

Hata hivyo amesema bwana Sisulu, amesema kuwa serikali ya muungano wa kitaifa huenda ikawa ndio suluhisho kwa mzozo wa kisiasa unaokumba taifa hilo la kanda ya maziwa makuu ambayo inahitaji kupata amani ya kudumu

Pendekezo la SADC tayari limeanza kuvutia hisia mseto.

Baadhi ya watu wanahoji kuwa mtindo huu wa kumaliza mzozo unahujumu demokrasia katika mataifa ya Afrika.

Bongo 5
 
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imeitaka tume ya uchaguzi nchini DRC kuhesabu upya kura ili mshindi halali aweze kutambulika, baada ya mshindi wa pili Martin Fayulu kudai kuna wizi wa kura. Fayulu amefungua kesi Mahakama ya Katiba kupinga matokeo hayo.
 
Back
Top Bottom