SABABU ZINAZOWAFANYA WANAFUNZI KUFELI MITIHANI.

SABABU ZINAZOWAFANYA WANAFUNZI KUFELI MITIHANI.

MMASSY

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
293
Reaction score
199
Tatizo la kufeli mitihani limekuwa ni kubwa sana na kuwaathiri wazazi ,walezi ,walimu ,serikali na hata wanafunzi wenyewe.Ukubwa wa tatizo umesababishwa na wadau wenyewe wa elimu ikiwamo wanafunzi.Mbaya zaidi ni kwamba katika kushughulikia hili tumejikita zaidi katika mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu na sio yaliyo ndani ya uwezo wetu.Katika kijitabu hiki tutakupatia mbinu zaidi za namna mwanafunzi anaweza
Kwa nini wanafunzi wanafeli mtihani?
Tatizo kuu la wanafunzi kufeli mtihani ni kutoelewa walichojifunza au kuelewa kwa kiasi kidogo sana ikiwa ni pamoja kutokuwa na mikakati kabambe ya namna ya kujibu maswali kwenye mtihani.Kutoelewa kunatokana na sababu kadhaa ambazo zimeorodheshwa hapo chini tafadhali pitia kwa umakini.
Uwezo mdogo wa kuelewa haraka
Kila mtu hapa duniani ana akili, tena akili za kutosha, isipokuwa kwa wale wenye magonjwa yanayohusiana na akili.Kusema hivyo ni kwamba kila mtu anauwezo wa kufaulu mtihani, ilimradi tu kama alipata nafasi ya kujifunza.
Watu wenye uwezo mdogo wa kuelewa haraka huwa wanafeli kutokana na kutopata muda wa kutosha kueleweshwa.Kundi hili lina idadi kubwa sana ya watu mashuleni kuliko wale wanaoelewa haraka.Kwa kawaida mwalimu hutumia dakika zisizozidi 40 darasani akifundisha.Ni dhahili kuwa muda huu hautoshi kufanya kila kitu kinachomwezesha mwanafunzi kubaki ameelewa 100%.Hivyo kundi la hawa wanafunzi wasioelewa haraka hubaki na pengo la kuelewa kila siku wanapotoka darasani.
Wakati bado wanashughulikia pengo lao ili wafanane na wale wenzao walioelewa, hujikuta wakikabiliwa na mitihani.Matokeo yake hujikuta wakijibu mtihani ama kwa jinsi wanavyoelewa wao au kwa kubahatisha, hivyo kufeli mtihani.
Ulemavu
Kama mwanafunzi hajakaguliwa sawasawa kuhusiana na ulemavu na kuhudumiwa kipekee ,kunauwezekano mkubwa wa kufeli mtihani.ulemavu ambao una madhara makubwa sana katika ufaulu ni pamoja na ulemavu wa akili,uoni hafifu na kutosikia vizuri.Kuna baadhi ya wanafunzi wenye uoni hafifu au kutosikia vizuri wasiojulikana na walimu wao.Kwasababu ya kutojulikana kwao hujikuta wakijifunza kwa mashaka tu mpaka mwalimu anamaliza kufundisha darasani.Matokeo yake hujikuta wakiwa hawajaelewa mpaka mitihani inapowakuta.
Uwezo mdogo wa kuchukuliana na mazingira
Mwanafunzi mwenye uwezo mdogo wa kuchukuliana na mazingira, anaweza kuelewa taratibu au kutoelewa kabisa na kujikuta akifanya vibaya katika mitihani yake.Hapa ndipo unapokuja ule usemi ninaoupenda sana usemao kile usichoweza kukizuia kiepuke.
Mazingira yanaweza kumuathiri mwanafunzi endapo kama hatoelewa nini cha kufanya wakati yanapofikia hatua ya kuathili uelewa wake darasani.
Hapa ndipo unapoweza kuona tofauti .Kwamba mwanafunzi anayeishi katika mazingira magumu au...............
jipatie kitabu chenye muongozo wa mbinu za kusoma na kuelewa unachokisoma,mbinu za kukumbuka kile unachokisoma,namna ya kukumbuka kile unachokisoma,maandalizi ya mitihani, mbinu za kujibu maswali ya essay,ya kuchagua, na namba n.k.
Ni kijitabu kilichowasaidia wengi kufikia malengo yao ya ufaulu.Kinaitwa ........

KWANINI NIFELI MITIHANI? “NAJIFUNZA HATUA KWA HATUA MBINU NA MIKAKATI YA KUFAULU MITIHANI
YANGU.SINA TENA SABABU YA KUFELI”
Kimsingi utanufaika sana kwa kukisoma kitabu hiki, ewe baba,mama,mwanafunzi na mtu yeyote yule,jipatie kitabu hiki.Tupigie au tuandikie sms au whattsapkwa kupitia 0758673441.Karibuni sana katika Holy Hands Book Project

Lets Achieve Excellence Together

JEROME MMASSY
Mkurugenzi mtendaji
Holy Hands Book Project
 
Last edited:
Back
Top Bottom