Sababu zinazo sababisha ndoa nyingi kuvunjika

Richard chilongani

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
324
112
Ndoa nyingi zipo mashakani kwa sababu manung'uniko, hasira, kutovumiliana,kufoka,kutukanana,kutoaminiana, kuwaziana mabaya badala ya mazuri, kujikweza kwa majivuno yasiyo na maana, kunyimana unyumba bila sababu ya msingi, kuachiana kazi za nyumbani, kutotoka out pamoja, kupiga au kupigiwa simu na watu baki na kuongea mbali na mwenzi wako, kuchati muda mrefu wakati upo na mwenzi wako, kuweka visingizio lukuki hayo na mengine mengi ndivyo vya ndoa kuvunjika, wapendwa kuyashinda Hays in kufunga na kuomba kwa Jina la Yesu.
 
Yesu anasingiziwa sana kwahyo ata kuchati napenyewe yesu aombwe duu!!
 
Tunapozungumzia taasisi ya ndoa ina changamoto nyingi zinazopelekea kuvunjika kwake na muhimili Mkubwa katika ndoa ni upendo, kwani palipo na upendo tutavumiliana, tutasameheana, tutabebeana, mizigo , tutahurumiana

cha msingi hapo ni kuhakikisha tunatumia mbinu zozote zile kuhakikisha upendo haukauki , ndani ya ndoa na vile vile tumshirikishe MUNGU katika ndoa zetu.
 
Hata ukigongewa utavumilia.

Uvumilivu downloading.....
 
kinachodondosha ndoa nyingi ni kuzoeana kupita kiasi,kummiliki mtu kama mali binafsi,dharau,malalamiko

Kuna wengine ,akishavalishwa pete tu basi anajiona yeye ndio mmiliki halali wa mwenza wake hivyo atataka mali, simu na account zote za mitandaoni za mwenza wake azijue na awe na uhuru navyo

Ataanza mchagulia mwenza marafiki na hata watu wa kuongea nao.inakata stimu ya ndoa.

Malalamiko hayaishi tena kwa kauli za kabla hatujaoana nilikua huru au ulikua unanijali na kuwahi kurudi. Kosa kidogo lawama na malalamiko tele.

Tamaa ya vitu vikubwa,wapo wanaodhan wakiingia ndoan watapata vitu ambavyo walikua wanavitaman bila kujali uchumi wao wote wawili
 
Back
Top Bottom