Sababu 9 zinazochangia kuvunjika kwa mahusiano mengi au ndoa

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,601
5,943
.
Matarajio yaliyopitiliza.....

Kwa kawaida kila mmoja wetu hutazamia mambo makubwa kutoka kwa mwenzi wake, ikitokea matarijio yako yakawa kinyume na vile ulivyomdhania mwenzi wako, ni lazima mgogoro utaibuka katika mahusiano au ndoa yenu utakaopelekea kuvunjika kwa mahusiano au ndoa yako.

Fikra HASI juu ya mwenzi wako...

Unapokuwa na fikra hasi au wasi wasi juu ya mienendo ya mwenzi wako, na ukaamua kukaa kimya juu ya hilo, ni wazi kuwa badala ya kujenga unabomoa mwenyewe. Yawezekana vile unavyowaza wewe kumuhusu mwenzi wako, sivyo alivyo. Kuendelea kuishi na fikra hasi zinazomuhusu mwenzi wako ambazo huwa huziongea ni lazima mahusiano yako yatakuwa na mgogoro utakaopelekea kuvunjika kwa mahusiano yako..

Usiri uliopitiliza......

Wapenzi wa siku hizi wanaweza wakaishi hata miaka mitano bila kufahamiana kwa undani zaidi.Hii inatokana na ukweli kwamba wapenzi wengi hawapo huru katika kueleza ukweli wao kwa wenzi wao, Utakuta mtu upo katika ndoa yako lakini kuna baadhi ya mambo yanayohusu familia unayafanya mwenye bila kumshirikisha mwenzi wako, siku akijua kuhusu hilo nae ataanza kuishi kwa usiri kama unavyoishi wewe, hali hii itapelekea kutoaminiana katika maisha yenu ya mahusiano au ndoa....

Uongo.......

Bila ya shaka uongo ni kitu chenye kukera sana, mwanzo unapoutumia uongo hukufanikishia mipango yako na unaufanya kuwa ndoo silaha yako kuu.
Lakini bila ya kujua kuwa silaha hiyo hiyo ndio itakayokuja kukuhukumu hapo baadae.

Mahusiano au ndoa iliyojengwa katika misingi ya UONGO na ulaghai huwa haiwi imara na haishiwi na migogoro. Kuishi ndani ya dimbwi la uongo ni kazi kubwa sana kwa kuwa tangu siku utakayoongopa ndipo utakapoanza vita ya kuulinda uongo wako na siku ukweli utakapofahamika mahusiano yako au ndoa yako haitakuwa na uhai wa kuishi tena.
DAIMA UKWELI UTAKUWEKA HURU........
Jenga tabia ya kuwa mkweli....

Kutokutimiza wajibu...

Mahusiano au ndoa imara hujengwa na watu wenyewe waliopo kwenye mahusiano au ndoa na wanaobomoa mahusiano au ndoa ni wanandoa wenyewe.. Lakini pia mahusiano au ndoa imara inajengwa na kila mtu au mwanandoa kutimiza wajibu wake kwenye mahusiano au ndoa.......

Ikiwa hutotimiza wajibu wako ipasavyo ni lazima mahusiano yako au ndoa yako haitokuwa na uhai zaidi ya migogoro kila kukicha...
kama wewe una haki ya kupata furaha kwenye mahusiano au ndoa yako, basi vile vile una wajibu wa kuhangaikia kuitoa furaha hiyohiyo kwa mwenzi wako.

Uelewa finyu juu ya mahusiano au NDOA......

Mahusiano mengi au ndoa nyingi za vijana zinavunjika kwa tatizo la kukosa Maarifa kuhusu mahusiano, kuishi na mtu mwenye tabia tofauti na yako sio Jambo rahisi unahitaji kuwa na maarifa ya kujielewa mwenyewe na kumwelewa mwenzi wako .kuwa na uelewa mdogo wa mahusiano ni jambo linalosababisha mahusiano mengi kuvunjika.

Mahusiano ya nje....

Endapo mwenzako atagundua kwamba unakula tunda jingine na sio lake tu basi ole wako! Safari ya talaka imeanza . Unapoanza kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa mwenzako huhisi kutengwa , na pia kupatwa na hofu ya uwezekano wa kuachwa .Wakati huo watu wengi huwa na chaguo la kujiondoa mapema kutoka ndoa hiyo kuliko kungoja hadi watakapoachwa.

Matatizo ya kifedha.

Utafiti unaonyesha kwamba ukosefu wa fedha za kuendesha mipango yenu kama wanandoa ni hatua inayoweza kusababisha talaka .wakati pesa zinapokosekana kuna uwezekano wa kuwepo hali ya taharuki na migogoro mingi ambayo pia huvuruga uhusiano wenu.

Muingiliano wa familia, ndugu jamaa na marafiki..

Mahusiano au ndoa nyingi zinavunjika kwasababu ya kukosa watu sahihi wa kuwashirikisha Mambo yenu ya ndani Kama Wanandoa,, Sio kila mtu anafaa kushirikishwa Maendeleo ya mahusiano yako au ndoa yako. Ikiwa una tabia ya kumshirikisha kila mtu Maendeleo ya mahusiano yako weka mipaka kwa ajili ya usalama wa mahusiano yako....
 

mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
26,646
39,128
Bila sababu kuu ya kuwa tunaingia kwenye mahusiano na breki pumbuz basi hujakamilisha mada yako.
 

welding1682

JF-Expert Member
Aug 20, 2019
394
643
Wafundishaji wa ndoa wenyewe hawana ndoa na wenye ndoa ni majanga matupu,
Mwanamke olewa mwanaume oa kila mmoja atatokea kwa mlango alio ingilia!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom