Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Serikali ya awamu ya tano imeanza kupoteza mvuto kila inapopita siku kwa sababu zifuatazo;
Bunge kutokuwa live, Serikali hakuna kitu ambacho imekosea kama kuliweka bunge Gizani, Maana kwa kupitia bunge wananchi ndio walikuwa wanajua wamefanya nini na watafanya nini.
Katika riport ya Twaweza imebaini wananchi wengi wanapenda Bunge kuwa live sasa hivi serikali imeweka pamba maskioni wewe subiri wananchi wengi sasa wamepoteza Imani na serikali kuliko Mwanzoni.
Tulia Ackison, huyu mwanadada ambaye ni naibu spika amefanya watu wengi kuichukia serikali kwa jinsi anavyoendesha bunge kupendelea upanda mmoja kwa sababu ya wingi wa wajumbe ( Majority member) wa chama chao.
Watu wanasema ni mtu alioletwa kwa kazi ya kuudhoofisha upinzani bungeni, kwa kupitia mama huyu bunge limekuwa Kibogoyo watoa hoja wakuu ni wakina Bashungwa na Goodluck Mlinga ndio wamekuwa wanarusiwa kuongea kwa maana hii serikali inashutumiwa moja kwa moja kulidhoofisha bunge kwa kupitia huyu mama.
Kauli za Dr Magufuri, nayo ni sababu ya serikali hii kuchuuja mapema sana zimekuwa ni kauli tata ambazo hazina Afya katika ustawi wa jamii yetu mfano " Meya anapenda ujambazi"
Na ile kauli ya hakuna siasa mpaka 2020 na ile nyinyi wakuu wa mikoa mnauwezo wa kuweka mtu ndani masaa 24, ukweli hizi kauli zimesababisha serikali hii kukosa mvuto mapema.
Jeshi la polisi, jeshi la polisi kuzuia mikutano ya hadhara, maafali na midaalo za upinzani imesababisha watu kuchukia serikali hii ya mbele kwa mbele polisi wamekuwa nao wanasiasa.
Wameenda kinyume na Nadharia ya Tradional military professionalism ya Samweli hurtdom kwa polisi wanatakiwa wasiwe na upande bali watumie taaruma zao kuisaidia jamii.
Matokeo yake polisi ameacha kutumia ujuzi wao kusaidia jamii wanatumia Bunduki na magari ya washa (coercive apparatus) kunyamanzisha upinzani ukweli watu wameichukia serikali kwa kutumia polisi kuwaonea wapinzani.
Ninachua utawala wa pharao ulishupaza shingo kwa kupuuza ujumbe wa Musa lakini Mungu hakushindwa kuwaondoa utumwani watu wake tulieni ni suala la kuvuta subira watanzania lazima wakombolewe.
Mhere Mwita.