Sababu za watu kusaliti katika mapenzi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
UNAHISI mwenzi wako anakusaliti kwa maana kwamba anafanya ngono na wanawake au wanaume wengine? Fahamu kuwa wapo wengi wenye kulalamikia hilo.

Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza kwanini hasa anatoka na wengine ikiwa aliahidi kwamba atakuwa ananipenda milele? Wengine wanakwenda mbali zaidi na kufikiri kila kitu ambacho anakifanya kwa mwenzi wake kitakuwa ni chenye kumpendeza mwingine.


“Mimi najitahidi kumfanyia mambo mengi mazuri, bado anaonekana haridhiki,” ndivyo baadhi ya watu wanavyojisemea.

UKWELI UKOJE?: Ni vizuri katika mapenzi kupata muda wa kuzungumza mwenzangu unapendelea nini na usingependa ufanyiwe nini.

KUAMINI KUWA UNAYOFANYA NI MAZURI, BILA KUAMBIWA NA UNAYEMFANYIA, SIO SAHIHI.
Maisha ya raha katika uhusiano ni kuhakikisha kunakuwa na fursa ya wapendanao kukaa na kujadili namna gani wamekuwa wakiishi na nini cha kufanya ili waweze kuwa na maisha bora zaidi.


KUKWAZANA NI MAMBO YA KAWAIDA KATIKA MAPENZI. IKIWA UMEKAA KWENYE TUMBO LA MAMA YAKO NA BADO KUNA WAKATI MNAKWAZANA, IWE MTU AMBAYE MMEKUTANA TU MITAANI?
Jambo muhimu katika ndoa ni kuhakikisha kunakuwa na nafasi ya wanandoa kujadili hali ya ndoa yao.


Kama ilivyo katika biashara kwamba wafanyabiashara wakati fulani wanajadili hali ya maendeleo ya biashara ili kujua kama kuna matatizo gani nk, ni muhimu sana wanandoa kutenga muda wa kujadili hali ya uhusiano wao.

SABABU ZA WATU KUSALITI
Wakati fulani nimekuwa nikiongea na watu wanaosaliti ndoa...baadhi yao ukiwauliza unaonaje sasa ukaondoa

kwenye ndoa na kuoana na huyo wa nje, jibu ni kwamba hawezi kwa sababu anasaliti si kwa sababu hampendi aliyenaye, bali wakati mwingine ni kutofautiana.


Kwa mfano katika utafiti wangu nimegundua kwamba idadi kubwa ya wanandoa waume, hawana uhakika wa kupata tendo la ndoa kwa wakati wanaotaka, kama ilivyo kwa baadhi ya wanawake.


Tafiti ambazo nimekuwa nikifanya pia nimegundua kuna tofauti ya mahitaji katika ndoa, kwa mfano wakati wanaume ni wenye kuhitaji mno tendo la ndoa, furaha ya wanawake walio wengi sio hilo wakati fulani ni uhakika wa kupatikana kwa mahitaji ya ndani na amani.


*Kutopata mapenzi ya kweli katika ndoa hasa ikiwa Kijana/Binti alilazimishwa kuoa/kuolewa na mtu ambaye hakumpenda.
-Wengine

hawapata mapenzi ya kweli kwa sababu tu mwanaume au mwanamke hamjali, kitendo ambacho kinasababisha baadhi yao kuona kwamba suluhu pekee ni kwenda nje ya ndoa.


*Uchafu, kutojijali au kujipenda kwa mwanaume na mwanamke
-Wapo wanaume na wanawake ambao wamekuwa wachafu wa mwili na kutojipenda, kiasi kwamba ukiwa nae unahisi kichefuchefu. Kuna wanaume na wanawake kwa mfano wanalala bila kuoga, wengine unakuta

mwingine mlevi, mwingine hanywi, kisha anarudi nyumbani anaomba abusiwe...mhh! raha iko wapi hapa?

*Kutotosheka/kuridhika katika tendo la ndoa

-Ingawa wakati mwingine huwa ni uroho wa mtu, mara nyingi hata majumbani watoto kama hawajashiba, baadhi yao hukimbilia kudowea chakula kwa jirani.


*Ubize wa kazi kupita kiasi/Kusafiri 
-Kuna watu wako bize kila kukicha, wakati mwingine si kweli kwamba wako bize bali ni unafiki au labda kutojua namna ya kupangilia mambo. Wengine ni watu wa safari kila mara, hiyo ni mbaya kwa wanandoa.


*Tamaa ya mali: Kuna wengine wako tayari kufanya ngono hovyo ili wapate mali. Huu ni ujinga, badala ya mtu kufanya kazi, anafikiri kwamba njia rahisi ni kubabaikia wanaume wenye magari, wenye fedha nk.


*Kujifunza mambo au mitindo mipya 
-Wakati mwingine kuna wengine wanatoka nje ili kusaka miondoka mipya...kuna wengine wamekuwa waoga wa kusema ukweli kwa wenzi wao juu ya yale ambayo wanayataka, matokeo yake wanaona wafanye hiyo ‘dawa mbadala’.


*Kutopata tendo la ndoa muda mrefu, labda kwa sababu mume ana matatizo au mke ana uja uzito mkubwa ama amejifungua n.k
-Hata hivyo kitaalam kuna njia za kuridhishana si lazima tendo la ndoa la aina moja, bali wapenzi wanaweza kuchezeana na kila kitu kikawa chenye kuwafurahisha wote au kumfanya mwenzi wake afurahie.
 
Wivu katika mapenzi ni ugonjwa mpana sana na hauna dawa halisia,na hisia ni mbaya unaweza ukapata ugonjwa wa moyo kama hutajiangalia na ku control hisia zinazoendana na wivu!!!
 
Well said MziziMkavu...Lakini nionavyo mie TAMAA is the source of all evils, waweza kuta mke/mume anampenda mwenza wake,anamjali,walioana kwa mapenzi yao bila kulazimishwa na mtu lakini baada ya miezi kadhaa au mwaka mmoja wanaanza kucheat. Nilishawahi kushuhudia familia flani mke anamjali mume kiasi kwamba hata usiku anaamka kumchemshia maziwa kama mtoto lakini mume alikua hashikiki mtaani. Kuna wengine ni tabia yao tu, hawezi kutulia na partner mmoja na watu wa namna hii hata ufanyeje hua hawabadiliki. Kumridhisha binadamu ni kazi ngumu sana.
 
Last edited by a moderator:
okay! nionavyo mie kuna haya mazoea katika wapenzi au mume/mke, yale ulokuwa unamfanyia wakati mkiwa gf & bf mkishaona kama alikuwa anakubusu kabla hajaenda kazini basi anapuuza na kuacha, mke pia kama alikuwa na kawaida ya kupiga goti wakati wa kukaribisha chakula mezani sasa ataanza hivi: chakula kipo mezani tayari, n.k so kuna vitu mke/mume wanaona ni vidogo au wanavipuuza ila vinadumisha mapenzi.
 
Ntairejea baada ya Iftar.....hii ukisoma lazima uwe unatafuna kaimati...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom