chakochetu
Senior Member
- Oct 13, 2012
- 108
- 35
Nimekuwa nafuatilia tatizo hili la uzembe,rushwa,ufisadi(rushwa kubwa) ndani ya sehemu mbalimbali za vyombo na taasisi za Serikali.
Kwa mtazamo wangu sasa hata maadili ya kazi vilevile yamepungua sana.
SABABU YA YOTE NILIYOYATAJA HAPO JUU:
[1].Watumishi kutokuwa na kipato kinacholingana na hali ya maisha yaliyopo;maisha yanabadilika sana mtaani wakati kipato hakiongezeki kulingana na hali ya uchumi.
[2].Utandawazi;ujio wa makampuni ya kigeni ambayo yanalipa mishahara na masilahi ya kutosha kwa wafanyakazi wake,hii imefanya wafanyakazi walio katika utumishi kutafuta namna ya kupunguza that GAP.
[3].Kuanguka kwa mifumo ya Elimu na maisha;sasa hivi kila mtu anataka kumpeleka mwanae shule binafsi ili kupata elimu nzuri.Pesa ya kugharimia maisha na Elimu nzuri kwa watoto(hapo kipato hakitoshi!!!,hali katika inayokaribisha rushwa,uzembe wa kazi kwani mtu nahangaikia mambo yake binafsi)
[4].Wafanyakazi wengi wamekaa sehemu moja zaidi ya miaka 5 mpaka miaka 20 kituo kimoja katika kazi;hii inazuia mabadiliko na uwajibikaji kazi HATA UKIBADILI VIONGOZI mabadiliko hayatatokea!!!!
NINI KIFANYIKE ILI KUPUNGUZA RUSHWA,UZEMBE NA UFISADI:

- Kuwahamisha watumishi waliokaa muda mrefu katika WIZARA na taasisi [miaka 5 na kuendelea!!!].Mfano hapa DAR watumishi wengi hawajui mazingira ya mikoani,ndio maana kila kitu kinafanywa na kuwekwa DAR hata huduma ambazo zingepeelkwa mikoani zinabaki DAR,hii imesababisha vijana wengi kukimbilia DAR kutafuta maisha.!!!!
- Muundo wa utumishi upitiwe upya[Namna ya kuajiri,sifa za elimu katika nafasi ya kazi,mishahara ipitiwe upya]
- Wanasiasa wasiwatishie watumishi[kuwakomoa kwa kutumia nafasi zao za kisiasa]
- Mfumo wa Elimu ya Msingi iimarishwe{vitabu vichapwe na Serikali na vifanane nchi nzima .!!!}
- Wanafunzi wanaosoma kasikazini,wakifaulu wapelekwe kusini na wa mashariki wapelekwe magharibi;hii itajenga utaifa na kufanya mwanafunzi kujua nchi yake,kuleta uvumilivu wa mila za watu na makabila mengine.!!!!!