singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,538
Zipo sababu nyingi zinazosababisha vyama vya upinzani kushindwa na chama tawala. Vyama vya upinzani ni vile ambavyo havijaingia katika mfumo rasmi wa uongozi wa kisiasa katika nchi. Chama au vyama vilivyoingia katika mfumo wa uongozi wa kisiasa ndiyo uitwa tawala.Makala hii itajadili sababu za kushindwa kwa vyama vya siasa nchini Tanzania, kwa kuhusisha sababu za ndani na za nje.
Sababu za ndani ni zile zinazoangalia matatizo yanayotokana na vyama vyenyewe vya upinzani nje ya chama tawala na zile za nje zinazotokana na mwendo wa chama tawala.
Chama tawala kwa sasa nchini Tanzania ni Chama Cha Mapinduzi (CCM). Chama hicho kimetokana na muunganiko wa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) cha Tanganyika na Afro Shiraz Party (ASP) cha Zanzibar.
Vyama vya siasa vya upinzani kwa Tanzania ni Civic United Front (CUF), Tanzania Labour Party (TLP), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), National Convention for Constitution and Reconstruction-Mageuzi (NCCR-Mageuzi), National League of Democracy (NLD), Democratic Party (DP), Demokrasia Makini, Alliance For Change And Transparency (ACT) kwa kuvitaja vichache.
Wingi huo wa vyama unatokana na kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi. Mfumo wa vyama vingi ni hali ya kuwa na chama zaidi ya kimoja, katika nchi moja. Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa na kuleta maendeleo ya nchi.
Upinzani wa kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani, bali vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii husika. Mfumo wa vyama vingi vya siasa ulirejeshwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, mwaka 1992. Ni mfumo uliorejeshwa, kwa sababu wakati wa harakati za uhuru na baada ya uhuru kulikuwa na chama zaidi ya kimoja.
Siasa inatafsiri nyingi. Siasa inaweza kuwa ni mkusanyiko wa watu wenye itikadi, madhumuni na shabaha inayofanana. Au ni njia ya kufanya maamuzi katika taifa, mji au hata dunia nzima (siasa ya kimatatifa) kwa kuhusisha chama au vyama vya siasa. Mambo muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka.
Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi. Mfumo huu wa demokrasia uhusisha siasa za zaidi ya chama kimoja au vyama vingi.
Kwa sasa Tanzania ipo katika kipindi cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu. Bila shaka kila chama cha siasa kitakuwa na malengo mbalimbali kuhusiana na uchaguzi huo.
Lakini shabaha ya wazi kwa vyama hivyo ni kushiriki uchaguzi na kukamata mamlaka kwa lengo la kuleta maendeleo.Kwa namna siasa zinavyokwenda sasa ni wazi kuwa vyama vya siasa hususani vile vya mageuzi vinapaswa kujitafakari na kufanya mapitio kwenye mikakati yao ya uchaguzi.
Kujitafakari kwa kuangalia huwa vinashindwa wapi kila mara vinapopambana na CCM kwenye chaguzi mbalimbali. Ni wazi kuwa vyama hivyo vimeanzishwa vikiwa na shabaha ya kushinda uchaguzi na kutwaa madaraka ya nchi.
Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha kushindwa kwa vyama vya upinzani. Sababu hizo ni kukosekana kwa kura za akiba, kutokuwa na ushirikiano na vyama vingine kutoka kwenye nchi zilizoendelea, kushindwa kuvifanya kuwa vyama vya kitaasisi, vitisho kuwaelekea maofisa wa vikosi vya ulinzi na usalama, kutobainisha sera zao na badala yake kutumia muda mwingi kutafuta udhaifu wa chama tawala, suala la kuundwa kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kupokonyana madaraka kwa kuyataja mambo machache.
Sababu ya kwanza, ni vyama vya mageuzi kutafuta visingizio vya kushindwa hata kabla havijashiriki uchaguzi wenyewe. Kwa mfano, hivi karibuni mmoja wa viongozi wa juu wa CUF, hakusita kuwashutumu maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kuwa wamekuwa wakitumia hila kuandikisha wapingakura.
Jambo linalotengenezwa hapo ni kuwa ZEC inashirikiana na CCM kutengeneza mazingira ya ushindi. Huu ni udhaifu wa wazi kwani viongozi hao waandamizi wa CUF wameshindwa kupanga mikakati kukabiliana na hali iliopo na badala yake wamegeuka kuwa sehemu ya walalamikaji.
Hii pia inaweza kuwa moja ya sababu ya kushindwa, kwani vyama na viongozi wake wameshajitayarisha kushindwa hata kabla ya uchaguzi haujafanyika.
Je, ni kweli mara zote CCM imekuwa ikivishinda vyama vingine kwa kuviibia kura? Je, vyama hivyo huwa havina mawakala kwenye vituo vya kupigia kura? Kama wapo, wakati vinaibiwa kura, mawakala wao huwa wapi? Je, huu hauwezi kuwa ujanja wa vyama vya upinzani kutafuta visingizio vya kutaka kuwaaminisha wananchi kwamba kushindwa kwao kumetokana na mizengwe ya CCM na siyo udhaifu wao? Je, endapo wagombea na vyama vyao watakiri kwamba wameshindwa kihalali na CCM, je huo hauwezi kuwa mwanzo wa mwisho wa vyama hivyo kisiasa? Je wagombea wa upinzani waliokiri kushindwa katika kinyang'anyiro wataendelea kuaminiwa na wapigakura?
Sababu ya pili ni kukosekana kwa mtaji wa wapigakura. Mtaji wa wapigakura ni wale wapigakura walioweza kubadilika kirahisi. Ni aina ya wapigakura wanaoweza kushiriki uchaguzi kwa hali yoyote inayohusisha matatizo katika uchaguzi.
Kwamba mtaji wa wapigakura unahusisha wafuasi wavumilivu wa hali ya hewa kama vile mvua au jua kali, matatizo ya kucheleweshwa kwa vifaa vya kufanikisha uchaguzi nakadhalika. Wapiga kura wa aina hii wanapatikana ndani ya CCM. Ndiyo wanaofanikisha ushindi wa chama hicho.
Kwa upande wa vyama vya upinzani vyenye nguvu kisiasa kama vile CHADEMA, CUF, ACT, NCCR-Mageuzi, TLP na UDP, bila shaka vinaungwa mkono na vijana wengi.
Lakini vijana hawa siyo wavumilivu wa matatizo yanayojitokeza wakati wa zoezi la upigaji kura. Mathalani ni vijana wangapi wanaoweza kuacha biashara zao na kutumia saa sita au nane kusubiria vifaa vya kupigia kura vilivyochelewa kufika katika kituo husika kwa wakati? Bila shaka ni wachache.
Sababu ya tatu, vitisho vinavyotolewa na viongozi waandamizi wa vyama vya upinzani dhidi ya maofisa wa juu, wa kati na wa chini wa Idara ya Usalama wa Taifa, jeshi la polisi nakadhalika. Vitisho vinavyotolewa na wanasiasa wa upinzani ni namna watakavyowawajibisha maofisa hao pindi wakiingia madarakani. Unaweza kuwasikia wakisema, "sisi tukiingia madarakani hawa polisi na maofisa usalama, lazima tutawaonesha kazi. Tutafukuza wote hawa.
"Ni ofisa gani atakayekubali kusubiri kupoteza kibarua chake kwa kufanikisha vyama vya upinzani kutwaa madaraka? Bila shaka taswira inayojengeka kichwani mwa ofisa yeyote mwenye familia ni kuhakikisha CCM inashinda ili watoto wake au familia yake iweze kupata mkate wa kila siku. Ni askari gani atakayekubali kuwaona wazazi wake au yeye mwenyewe akipata shida kwa kuruhusu chama chenye vitisho dhidi yake kupata ushindi?
Inawezekana kuwa wanasiasa wanaotoa vitisho dhidi ya maofisa wa ulinzi na usalama wanafanya hivyo kwa lengo la kujikweza kisiasa na kutaka kuonesha kuwa wao ni watu wasiohofu chochote mbele ya wafuasi wao. Lakini kwa upande mwingine, wanajiathiri wao wenyewe kwa sababu wanawajengea maofisi hao mazingira ya kuhami ajira zao kwa kufanikisha ushindi wa CCM.
Sababu ya nne, ni kushindwa kuvifanya kuwa vyama vya kitaasisi. Vyama vya kitaasisi ni vyama vya siasa vyenye nguvu kiuchumi na uwezo wa kujiendesha bila kutegemea ruzuku (subsidy). Hivyo, tatizo la msingi linalovikabili vyama vya siasa vya upinzani nchini ni kutokuwa vyama vya kitaasisi vyenye vyanzo tofauti vya mapato. Kukosekana kwa vyanzo mbalimbali vya mapato, kumeibua matatizo mbalimbali. Kumekuwa na migongano ya mara kwa mara kuhusiana na ruzuku.
Maofisa wa vyama hivyo kwenye ngazi ya kitaifa, kimkoa, kiwilaya, kijimbo, kitarafa, kikata, kimtaa au kijiji na kitongoji wote wanategemea ruzuku kutoka makao makuu. Ruzuku inayotolewa hujikuta ikiishia ngazi fulani tu na kuyaacha maeneo mengine watendaji wake wakiwa katika hali ngumu kutekeleza majukumu yao.
CCM huwa haina migongano ya mara kwa mara kuhusiana na ruzuku. CCM kupitia Jumuiya zake ina miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imekuwa chanzo cha mapato. Mfano ina miliki viwanja vya mpira, kumbi za starehe, mradi wa ukodishaji wa majengo ya biashara kwa kutaja michache. Hivyo basi, vyama vinapokosa nguvu ya kitaasisi ni wazi inategeneza mazingira ya kushindwa kirahisi kwani tayari kinatengeneza migogoro.
Sababu ya tano ni vyama vya upinzani kutumia muda mwingi kutafuta udhaifu wa CCM badala ya kutangaza sera. Imekuwa vigumu kwa wananchi wa kawaida kuelewa vyama vya upinzani vina sera gani kuhusiana na huduma ya kijamii, uchumi na siasa.
Matatizo yaliopo katika elimu yatatulizwaje na chama husika endapo kikiingia madarakani. Matatizo ya maji yanayovikumba vijiji vya Chiungutwa, Rivango, Nakarara, Mnavira, kwa kutaja maeneo machache yanatatuliwaje? Wapinzani watatumia sayansi gani kuhakikisha miundombinu ya umeme, maji, barabara inaboreshwa.
Watatumia sayansi gani kuzuia matatizo yanayojitokeza kuhusiana na uwindaji haramu na ufisadi unakomeshwa. Wananchi hawataki kusikia habari za kusimuliwa kuhusiana na kushindwa au kufanikiwa kwa CCM, kwani wanauona na wanaushiriki.
Wananchi wanamuona namna Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana anavyozunguka huku na kule kuhakikisha anaibua kero zao mbalimbali, ili serikali izitatue kwa haraka.
Ingawa kuna mapungufu katika namna ya kuzikabili, lakini kuna unafuu kwa kiasi fulani kwani mkakati huo wa CCM unalenga kukirejesha chama hicho mikono mwa wananchi badala ya kuendelea kuwa cha viongozi. Ninachosisitiza hapa ni kuwa vyama vya upinzani ni lazima vijikague na kuacha kuwa vyama vya walalamikaji na wakosoaji.
Vinatakiwa kuwa vyama vinavyowajibika kwa wananchi kwa kutumia sera zake. Ni vyama mbadala vinavyojitolea kutatua matatizo ya wananchi bila kujali kama vimekasimishwa madaraka au la. Vishiriki katika kutatua matatizo ya wananchi wakati wote badala ya kuwa vyama vya kuvizia kuteleza kisiasa kwa CCM.
Sababu ya sita ni kukosekana kwa ushirikano wa kisiasa kutoka kwenye vyama vingine vya nje ya nchi. Ushirikiano wa kisiasa ni ule unaojumuisha vyama vingine vilivyopo kwenye nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Ushirikiano wa namna hii unaweza kusaidia kubadilishana uzoefu na mbinu anuai katika kufanikisha ushindi kwa njia ya kistaarabu.
Ni ukweli uliko wazi kwamba ni vigumu kwa nchi (taifa) kushirikiana na chama cha siasa. Endapo nchi itajiingiza katika masuala ya ndani kwa kushirikiana na chama cha siasa ni kuingilia masuala ya utawala ya ndani ya nchi inayoingiliwa. Hivyo, ili kuepuka hilo lazima vyama vya hapa viwe na ushirikiano kutoka kwenye vyama vingine kutoka katika nchi mbalimbali.
Chanzo: Taifa imara