Sababu Yako 🥲

Joined
May 6, 2019
Posts
9
Reaction score
4
SABABU YAKO:

Sikulaumu wala siwezi kuja kulaumu,
Ila ni sababu yako mimi kuwa hivi,
Ni aghalabu kuona tabasam langu yani nimekuwa chakaramu,
Unapokuwa kibogoyo ni nadra kutafunia fizi,
Ila kwakweli nimezidi maana huu si ubinadamu.

Nimekuwa sisikii na nikisikia siambiliki hata uwashe spika,
Umekuwa wangu mchezo kila gari nadandia,
Situlii kituo kimoja nikipanda Makango juu Kilimani tu nashuka,
Nashuka sitembei napanda gari nyingine inayokimbia,
Haijalishi kwenye bonde ama kasi likizingua naruka.

Sababu yako nimekuwa sijali,
Hisia za wengine nawaona kama wewe,
Sijawahi kukuota ila nakuwaza silali,
Sikulaumu maana uliamua kuwa mwewe.

Ndio mwewe ! Sijui nikuite bundi ama kunguru?,
Ulijivika maumbile ya binadamu anayevutia kumbe jini,
Ulininyonya maana kwa penzi lako nililipia ushuru,
Hata nikisimamishwa mbele ya mungu wangu sijui nitamwambia nini,
Maana nilofanya ni zaidi ya kumkufuru.

Nilikupea ulichotaka na ziada nikakupa,
Hukutaka nilichotaka na sikuwahi kujuta,
Uliniloga mwanahizaya ukanipeleka pupa,
Sikujua kuwa jitihada zote ziliishia kugonga ukuta , mwenzenu najuta.

Sababu yako moyo sijamfungulia mtu,
Sio kama naogopa la hasha, kwa moyo gani haswa,
Moyo ulojaa uasi na visasi hauna hata chembe ya utu,
Kwangu hili ni kasha tu , sina nachosubiria zaidi ya kifo kunasa.

Sababu yako bora nife angalau mimi,
Niende kwa mungu maana kuna haki,
Yako wapi ya kujifanya Vee wa Rotimi,
Hadi leo siamini kwamba yale yote uliniziaki.

Nimekuacha salama shukuru Jibwa wewe,
Tena mbwa koko ama Paka la baa,
Kwa jinsi ulivyonitumia kwa manufaa yako mwenyewe,
Sina budi nifungue kesi unilipe hata mirabaa.

Sijakusamehe mimi, siwezi kudanganya,
Kwanza ya nini? na ukweli nipingane,
Natamani kukushika na kukukatakata kama nyanya,
Upotee ulimwenguni ili tusionane.

Ila jua mimi shujaa mpigania moyo,
Nitahakikisha unapata maumivu pia,
Najua umeniona bwege ama poyoyo,
Naondoka ila ulionifanyia ni KARMA na yatajirudia.

0674855951

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…