Sababu ya kocha Simba SC kutomuingiza Kagere

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
18,511
68,141
Nimetafakari kwa muda sababu ya msingi kwanini kocha hakumuingiza Kagere nikapata sababu mbili.

1. Nimehisi sub zinazotakiwa mwisho ni tatu, japo wapo wanaosema sababu ya Corona zinatakiwa sub mpaka wachezaji watano, kwasababu kama bado kocha alikuwa na nafasi ya kumuingiza Kagere baada ya Mugalu kuonekana amepwaya kule mbele, sioni kwanini hakufanya hivyo.

2. Sababu yangu ya pili inayoendana na ile ya kwanza ni kuumia kwa Lwanga, hii ilisababisha nafasi ya kumuingiza Kagere iwe imeshajazwa kwa aliechukua nafasi ya Lwanga (ambae ni Nyoni) hivyo kuondoa nafasi ya Kagere kuingia.

Kama hizi sababu zote mbili sio za kweli, maana yake kocha alikuwa na nafasi ya kumuingiza Kagere lakini hakufanya hivyo, kitendo chake cha kuonesha mahaba kwa mchezaji aliekosa ubunifu kule mbele kimechangia Simba SC kuondoshwa, hasa nikizingatia uwezo wa Kagere kwenye kuzifumania nyavu, kama ambavyo alikuwa mfungaji bora wa ligi yetu misimu miwili mfululizo.
 
Kifupi coach hampemdi kagere tuseme..

Subs zilikiwa hazijaisha.. Ana matatizo mahali, ama tuseme alikiwa kavurugwa bemchi la ufundi lilipaswa limkumbushe, pamoja ma yoote kagere ndio mfungaji wetu tegemeo kwa misimu kadhaa, na msimu huu ni nafasi tu kanyimwa lakini mie naamini katika uwezo wake.
 
Simba bahati haikua yetu leo, hata angeanza MK14 mtu wa kazi. Ukiangalia magoli mengi wachezaji waliyokosa ni mengi sio Mugalu tu hata, Boko, Chama na Morison. Pia kuna mchezaji wa Kaizer alishika ndani ya box lakini refa kapotezea.

Simba ni timu bora sana ingawa imetolewa lakini kazi imefanyika ya kiwango cha kimataifa.

Simba nguvu moja.
 
Viongoz wa simba nao wamezd zalau ata kama kagere na boko hawafai sio wa kuwafananisha na mugalu huu msimu wataukumbuka sana ulikuwa mwepes kwao kufka nusu ila uzembe na zalau wangezitumua zile nafas kusajili baada ya kufka robo leo wangetoboa kuna baadhi ya wachezaj walifanya kila ktu ila wachache kutokana na viwango vyao ndio kumewafelisha kupata magol zaid

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Simba wamejitoa wenyewe hawajatolewa na Kaizer.
 
Kifupi coach hampemdi kagere tuseme..

Subs zilikiwa hazijaisha.. Ana matatizo mahali, ama tuseme alikiwa kavurugwa bemchi la ufundi lilipaswa limkumbushe, pamoja ma yoote kagere ndio mfungaji wetu tegemeo kwa misimu kadhaa, na msimu huu ni nafasi tu kanyimwa lakini mie naamini katika uwezo wake.
Kama kila kocha anamchukia Kagera basi kunashida mahali
 
Simba kwa kuwa wameijuliaa uwanja wao wa nyumbani bas katk mech zingine cjazo wahakikishe kuwa magoli ya away yaziwe Zaid ya mawili tu Zaid Sana moja tu ili ikija dsm uwanja wake ifanye mambo lait Kama Simba kaliwa mbili kule bondeni bas leo angepita kirahisi Sana Leo ingekuta Ni sherehe had yule aliyefiwa na bb ake angesherekea tu
 
Vyema ampe nafasi na Kagere kuliko kukomaa na Mugalu muda wote no matter what.
Ila kitu nachokuhakikishia mimi simkubali Mugalu nampendekeza zaidi MK14,ila kuna kitu cha kiufundi pengine anacho ambacho kwa sisi mashabiki hatuwezi kukiona.

Kocha Gomes anakaa na wachezaji kwa muda na anawaona wakiwa mazoezini.

Simba nguvu moja.
 
Simba bahati haikua yetu leo,hata angeanza MK14 mtu wa kazi.
Ukiangalia magoli mengi wachezaji waliyokosa ni mengi sio Mugalu tu hata,Boko,Chama na Morison.pia kuna mchezaji wa Kaizer alishika ndani ya box lakini refa kapotezea.
Simba ni timu bora sana ingawa imetolewa lakini kazi imefanyika ya kiwango cha kimataifa.
Simba nguvu moja.
umemaliza baba. Simba ni mfalme wa nyika
 
Na huyu kocha utadhani karogwa na Mugalu. Jitu halina tija yoyote pale mbele na amemuacha acheze dakika zote 90. Asipoangalia ataondoka yeye na Mugalu wake kwa sababu huyu Mugalu anatutia machungu sana sisi wana Simba na hasa pale anapopoteza nafasi za wazi kila mechi.
 
Labda asepe Mugalu ila kwa huyu kocha ni mzuri sana tu,na tegemea kwenye mapendekezo ya kucho kurekebisha timu huwenda akabaki ndo utajua togauti makocha na mitazamo ya sisi mashabiki,ila Mugalu anatia aibu sana.
 
Back
Top Bottom