Sababu ya Biashara nyingi ndogo kushindwa kuendelea

Big Phil

Member
Nov 20, 2019
50
338
Biashara ndogo ndogo zimekuwa ni mkombozi kwa vijana wengi sana haswa kipindi hiki ambacho ajira ni ngumu kupatikana, biashara ndogo ndogo zinahitaji mtaji mdogo kuanzisha ambapo inakopesheka au unaweza kuomba hata rafiki au mzazi na akakuazima pesa mfano wa biashara hizo ni kuuza matunda, kuuza duka la bidhaa za nyumbani, migahawa, umachinga nk.

Chanzo kinachopelekea biashara kushindwa kuendelea.

1. Kutofanya utafiti wa soko la bidhaa yako (Not investigating the Market) - tunafanya biashara ili tuuze na kupata faida. Ili biashara iwe na faida lazima uwe na wateja wa uhakika, sehemu nzuri ya kuuza, bei nzuri na bidhaa bora. Wengi wetu tumekuwa tunaanzisha biashara kutokana na upepo kwamba flani kanzisha biashara fulani na mimi napita nayo hiyo hiyo. Lazima ufanye utafiti wa soko la bidhaa yako vinginevyo utakuwa umeanzisha biashara ya kitimoto Zanzibar.

2. Kutokuwa na muongozo bora wa biashara (Business Plan) kutokuwa na muongozo bora wa kufahamu faida na hasara za hiyo biashara na namna gani unaweza kukabiliana na changamoto za biashara hiyo, kodi, cost benefit analysis inaweza kudondosha biashara yako.

3. Kuweka mtaji kidogo kwenye biashara (Too little Financing) - wote tunafahamu kwamba mwanzo ni mgumu kwenye kila jambo, kuweka mtaji mdogo sana kwenye kuanzisha biashara inaweza kufanya biashara yako ife mapema kwani utashindwa kusuruhisha migogogoro ama changamoto zitakazoweza kujitokeza bila kutarajiwa (uncertainty).

4. Kuweka biashara yako sehemu isiyo sahihi (bad location) - kuna zile market strategy tulizojifunza ama tunahita 4Ps ( Product, Price,Place and Promotion) hivi ni vitu muhimu sana kuzifahamu na hazina ulazima wa kuzisomea chuo kikuu, unaweza kujifunza kutokana na mazingira yaliyotuzunguka. Angalia uhitaji wa bidhaa yako na wateja unaokusudia kuwahudumi mfano kama upo kwenye jamii ya wakulima uza mbolea, vifaa vya Kilimo nk kama upo kwenye mji unaoendelea fungua duka la vifaa vya ujenzi. Upo kwenye sehemu ya joto uza nguo laini zinazoendana na hali ya hewa ya upande huo na ndo maana vaa ya wadada wa Dar ni tofauti na wa mikoani sababu ya mazingira.

5. Kutotaka kubadilika (Remaining Rigid) - Biashara inahitaji kubadilisha upepo, wafanyabiashara wengi hatupendi kubadilika kuwa flexible, kama umeona biashara fulani haina tija na wateja wanataka bidhaa fulani badilisha na fanya biashara yenye uhitaji.

6. Kutaka kujitanua ambapo bado hujajitosheleza (Expanding too Fast) Mara nyingi biashara zinavyoanza kufanya vizuri sokoni na kuwa na ubora mzuri na wateja wengi, soko la uhakika tunaanza kutanua biashara hii ni nzuri ila angalia uwezekano wa kufanya market survey kufahamu changamoto kwani unaweza kutanua biashara ili uwafikie watt wengi na ubora ukapungua, uzalishaji ukapungua na ukawa na wateja wengi husioweza kuwamudu mwishowe ukakosa vyote. Kwani kuna msemo wa kiswahili unasema mtaka yote kukosa yote.

Ni vyema kujifunza kwa wafanyabiashara wazoefu namna wanavyotatua matatizo na jinsi gani wanaweza kuhimili mikikimikiki ya biashara. Tafuta role model ambaye utakuwa unamwangalia kwenye shughuli zako za kila siku hii itakusaidia kukua vizuri kibiashara.
 
Ukifanya market research ndo utajua namna gani unaweza kulipa kodi za TRA na mamlaka zingine husika, proper financial documentation. Bwana Shimba ya Buyenze.
Nimekuelewa mkuu.

Uzi mzuri sana ila sasa ndo hivyo. Hautapata wachangiaji wengi. Ingekuwa unazungumzia makalio au Dayamondi Platinamuzi ungeona ambavyo uzi ungewaka moto....
 
Watu wanapenda zaidi udaku kuliko vitu vyenye tija.

Ukichukulia vitu vyenye tija serious ukafanikiwa, utaitwa Mjenzi huru (Freemason).

Binafsi nimeshawahi kuwa mfanyabiashara, licha ya mtaji kuwa mdogo ila pia nilishindwa kubadilika kutokana na changamoto za biashara yenyewe.
Wakati naanza mambo yalikuwa mazuri, baadae competition ikanitoa kwenye reli.

If you live in the past, the future will never find you.
 
Biashara ndogo ndogo zimekuwa ni mkombozi kwa vijana wengi sana haswa kipindi hiki ambacho ajira ni ngumu kupatikana, biashara ndogo ndogo zinahitaji mtaji mdogo kuanzisha ambapo inakopesheka au unaweza kuomba hata rafiki au mzazi na akakuazima pesa mfano wa biashara hizo ni kuuza matunda, kuuza duka la bidhaa za nyumbani, migahawa, umachinga nk.

Chanzo kinachopelekea biashara kushindwa kuendelea.

1. Kutofanya utafiti wa soko la bidhaa yako (Not investigating the Market) - tunafanya biashara ili tuuze na kupata faida. Ili biashara iwe na faida lazima uwe na wateja wa uhakika, sehemu nzuri ya kuuza, bei nzuri na bidhaa bora. Wengi wetu tumekuwa tunaanzisha biashara kutokana na upepo kwamba flani kanzisha biashara fulani na mimi napita nayo hiyo hiyo. Lazima ufanye utafiti wa soko la bidhaa yako vinginevyo utakuwa umeanzisha biashara ya kitimoto Zanzibar.

2. Kutokuwa na muongozo bora wa biashara (Business Plan) kutokuwa na muongozo bora wa kufahamu faida na hasara za hiyo biashara na namna gani unaweza kukabiliana na changamoto za biashara hiyo, kodi, cost benefit analysis inaweza kudondosha biashara yako.

3. Kuweka mtaji kidogo kwenye biashara (Too little Financing) - wote tunafahamu kwamba mwanzo ni mgumu kwenye kila jambo, kuweka mtaji mdogo sana kwenye kuanzisha biashara inaweza kufanya biashara yako ife mapema kwani utashindwa kusuruhisha migogogoro ama changamoto zitakazoweza kujitokeza bila kutarajiwa (uncertainty).

4. Kuweka biashara yako sehemu isiyo sahihi (bad location) - kuna zile market strategy tulizojifunza ama tunahita 4Ps ( Product, Price,Place and Promotion) hivi ni vitu muhimu sana kuzifahamu na hazina ulazima wa kuzisomea chuo kikuu, unaweza kujifunza kutokana na mazingira yaliyotuzunguka. Angalia uhitaji wa bidhaa yako na wateja unaokusudia kuwahudumi mfano kama upo kwenye jamii ya wakulima uza mbolea, vifaa vya Kilimo nk kama upo kwenye mji unaoendelea fungua duka la vifaa vya ujenzi. Upo kwenye sehemu ya joto uza nguo laini zinazoendana na hali ya hewa ya upande huo na ndo maana vaa ya wadada wa Dar ni tofauti na wa mikoani sababu ya mazingira.

5. Kutotaka kubadilika (Remaining Rigid) - Biashara inahitaji kubadilisha upepo, wafanyabiashara wengi hatupendi kubadilika kuwa flexible, kama umeona biashara fulani haina tija na wateja wanataka bidhaa fulani badilisha na fanya biashara yenye uhitaji.

6. Kutaka kujitanua ambapo bado hujajitosheleza (Expanding too Fast) Mara nyingi biashara zinavyoanza kufanya vizuri sokoni na kuwa na ubora mzuri na wateja wengi, soko la uhakika tunaanza kutanua biashara hii ni nzuri ila angalia uwezekano wa kufanya market survey kufahamu changamoto kwani unaweza kutanua biashara ili uwafikie watt wengi na ubora ukapungua, uzalishaji ukapungua na ukawa na wateja wengi husioweza kuwamudu mwishowe ukakosa vyote. Kwani kuna msemo wa kiswahili unasema mtaka yote kukosa yote.

Ni vyema kujifunza kwa wafanyabiashara wazoefu namna wanavyotatua matatizo na jinsi gani wanaweza kuhimili mikikimikiki ya biashara. Tafuta role model ambaye utakuwa unamwangalia kwenye shughuli zako za kila siku hii itakusaidia kukua vizuri kibiashara.
Really Helpful..thx
 
Sio kwa sisi wa kujilipua mkuu.

Kuna time ukicalculate risks unaona kabisa hapa sifungui biashara yoyote.

Ni kweli ni vizuri kuzingatia hizo mambo ila kuna time inabidi tu mtu ajitungie shwria na mipango yake nje ya mingi inayofahamika na kufatwa na wengi (kama uliyoandika).

Ila biashara ikisimama basi ndo unaanza kufuata misingi kama hiyo, sometimes huwaga ni kucheza bahati nasibu tu.
 
Back
Top Bottom