Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,266
- 2,870
Mashaka na mkewe wameishi katika ndoa kwa miaka 7 sasa. Wana watoto wawili na kila anayewaona nje anaamini ni familia yenye furaha. Kipindi wameoana walikuwa na maisha ya kati mpaka baadaye mashaka alipokuja kuyumba kiuchumi baada ya kuachishwa kazi kwa miaka 5 wamesota sana.
Maisha kwa Mashaka yalikuwa magumu ndani na nje. Ila hakuna aliyejua. Mke wa Mashaka alikuwa amkikashifu mumewe kwa maneno kadhaa wa kadhaa..."mwanaume unashindwa kunihudumia, kuhudumia watoto, angalia wenzako x na x wana maisha mazuri, wamejenga na wana magari" ilifikia hata akawa anamnyima tendo la ndoa.
Mashaka akiomba ataambiwa kuwa yeye mwanamke hajisikii, anaumwa, amechoka n.k n.k . Kakuna alitejua kuwa ndani Mashaka ananyanyaswa na mkewe. Wakitoka nje wanacheka na kuonekana wenye furaha, Mashaka hakuwahi kusema hayo kwa watu.
Hatimaye Mashaka alifanikiwa kupata kazi ambayo ilimlipa sana. Akaanza kunawiri, akanunua kiwanja na kuanza kujenga. Mkewe kipindi hiki alibadilika sana. Akawa anaonesha mapenzi kwa Mashaka, hata kumuita mume, kumweka picha yake kwenye profile na hata kupost kwenye mitandao akimsifia.
Kipindi hiki Mashaka alikuwa ameshajifunza kitu. Mkewe alikuwa akimheshimu na kumpenda akiwa na pesa. Mapenzi ya mashaka kwa mkewe yalishapungua sana, kila akikumbuka manyanyaso na dharau za mkewe aliumia sana. Na hapa ndipo alipokuja kukutana na Tumaini. Tumaini alikuwa msichana mzuri ambaye alishatendwa vibaya na aliyekuwa mchumba wake.
Akaamua kuishi tu maisha yake mwenyewe mpaka alipokuja kuonana na mashaka. Hakutaka kumpenda Mashaka lakini siku zilivyozidi kwenda akajikuta anampenda Mashaka pamoja na kuwa alikuwa ni mume wa mtu. Tumaini alimjali mashaka sana kwa mapenz na maneno mazuri mashaka akatekwa kimapenzi.
Mke alikuja gundua mumewe ana nyumba ndogo na katka kuchunguza hata akapa iona picha ya Tumaini. Tumaini hakuwa mzuri sana ukimlinganisha na mke wa Mashaka. Na mke wa Mashaka alipogombana na mumewe alimwambia "kwanza mwanamke mwenyewe wala si mzuri wa kunizidi" hakujua Mashaka alitekwa na moyo wa upendo wa yule dada.
Watu wengine walimlaumu sana Mashaka kuwa aliishi na mkewe aliyemvumilia kipindi cha shida sasa amepata pesa amebadilika. Mashaka alipokea lawama zote. Hawakujua alivyokuwa akiteswa na kunyanyaswa, hawakujua kuwa alikuwa anadhalilishwa kwa kupigiwa nyimbo za mwanaume suruali n.k
Haya yote Mashaka aliyaweka moyoni. Sasa amempata Tumaini. Na hajarogwa hata chembe. Ni mapenzi tu yaliyomtia kiwi cha macho.
Wanawake wengi huwanyanyasa waume zao wanapokuwa hawana pesa. Na wengi huwadhalilisha sana na kuwadharau, kuna wanaume ambao huachiwa chumba au kitanda kisa mkewe haoni haja ya kulala naye wakati hamnunulii vitu vya thamani n.k
Kuna wanaume wanaishi na wake zao lakini huambulia kupiga punyeto kila siku sababu mke hataki kutoa tendo la ndoa au haoneshi ushirikiano kwa kuwa mumewe hana pesa.
"Mwanamke mpumbavu huiharibu nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe"