Sababu kumi za kuchagua IPv6 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu kumi za kuchagua IPv6

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kilongwe, Dec 29, 2010.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Souce: AfroIT.com

  Katika miaka ya themanini hadi mwanzo wa miaka ya tisini kitu kinachoitwa Kompyuta kilikuwa ni anasa.Hapa usiongelee Internet.Katika miaka hiyo matumizi ya Internet yalikuwa ni ya nadra na ni kwa wale wenye uwezo mkubwa tu.
  [​IMG]Katika miaka ya mlongo huu ambao tunaumalizia,mengi yametokea kuhusu teknolojia na kuwezesha kuigeuza network kuwa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.Leo hii Internet sio anasa tena bali ni kitu cha lazima.Sio tu kwenye kompyuta,bali kuanzia kwenye majokofu,televisheni na hata kwenye majiko yote sasa yanatumia Internet,ingawa kwa mazingira ya nyumbani vitu hivi vingi bado ni kwa wenye uwezo,muda unaenda na sisi tutafika huko siku si nyingi.
  Unapoongelea internet,huwezi kuepuka kuongelea kitu kinachoitwa IP,yaani kanuni za internet(Internet Protocol).IP ndio utambulishi/njia ambayo kompyuta,simu au kifaa chochote kinachotumia internet hutumia kutuma taarifa toka sehemu moja hadi nyingine kwenye ulimwengu wa internet,nimeandika makala inayoelezea IP kwa undani HAPA.

  Ukiwa kwenye anga za IP,kuna aina mbili za IP,moja ni IP toleo la nne(IPv4) na nyingine ni toleo la sita(IPv6).Ujio wa IP toleo la sita ni suluhisho la uhaba wa idadi ya IP uliokuwa unatabiriwa kuikabili dunia ya internet.Kwani [​IMG]kwenye ulimwengu wa IPv4,ilikuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa watumiaji milioni 4294.97,wakati idadi ya watu duniani inaenda bilioni sita sasa,Sasa walenga walisema tiba ni bora kuliko tiba.

  Hivyo jamaa wa IETF walitafuta njia mbadala za kukabiliana na huu utata kama NAT na CIDR,ingawa zimeleta manufaa lakini sio suluhishola moja kwa moja,hivyo kuna umuhimu wa kuja na suluhisho la milele kama sio karne kadhaa.Vilevile shinikizo toka kwa nchi zinazoendelea kama Uchina wakidai IP zaidi,kwani hapo awali Marekani walijipendelea kwa kujigawia anuani nyingi na kuzipunja nchi nyingine,jamaa wakaamua kuja na hii IP toleo la sita,

  Sasa hebu tuangalie umbo la IPv6
  1.Inatumia biti 128 za namba za hexadecimal

  Kwa wengi wetu ambao tumezoea matumizi ya IP toleo la nne,utagundua kuwa zilikuwa zinatumia namba za desimali zilizotafsiriwa toka namba za binari ambazo ziliunganishwa nne nne na kuwa 32, kwa mfano utaona ip kama 192.168.2.1, hapa kwenye kila kundi la namba za desimali kuna namba nne za sifuri au moja(binari) ambazo zimebadilishwa na kuwa za desimali,kila nambamoja ya binari ina biti mbili,hivyo kwakuwa kila kundi lina namba nne za binari basi 2*4=8,kumbuka namba ya binari inakuwa kama hivi 1=0001,lakini ukija kwenye IPv6 mambo sio,anuani haina mvuto wa anuani na iinaonekana kama minambanamba ambayo ipo kwenye mtindo wa hexadecimal.
  Kwenye anuani hizi kuna makundi nane ya namba nne nne za hexadecimal ambazo zinawakilisha biti 16 kila moja hivyo kufanya anuani ya IPv6 kuwa na biti 128 na sio 32 kama ilivyokuwa kwenye IPv4.Hapa ninamaanisha mfano wa anuani ya IPv6 ni kama huu 2001:0db8:85a3:0000:0000:8a2e:0370:7334, hapa utaona kuna makundi nane ya namba ambazo zipo kwenye mtindo wa hexadecimal,kila kundi linabeba biti nane hivyo 8*16=128. Utakuwa umejionea jinsi gani minamba ilivyoongezeka na kuharibu muonekano,ila usihofu kuna njia ya kurahisisha mambo.Pia IPv6 hutumia alama ya ":" kutenganisha namba na sio "." kama ilivyokuwa ikitumika kwenye IPv4.

  2.Anuani inaweza kufupishwa au kukatwa

  Wengi wetu walishaanza kulalama wakisema sasa hii si itakuwa kazi kukariri anuani ndefu yote hii? Mambo yamerahisishwa,kwenye IPv6 una uwezo wa kufupisha anuani kwa kuondoa misifuri isiyohitajika,kwanini? si unajua [​IMG]kwenye mtindo wa namba za hexadecimal kuna sifuri nyingi,hivyo tunaweza kuziondoa hizi sifuri na kuifanya anuani kuwa safi na murua kabisa.
  Mfano anuani kama FE80:CD00:0000:0CDE:1257:0000:211E:729CIf ambayo ndio halisia, tunaweza kuondoa misifuri na kuifanya ionekane kama hivi FE80:CD00:0:CDE:1257:0:211E:729C.Ila kumbuka sifuri za mwanzo ndio zimeondolewa na sio za mwisho,kwa mfano kwenye namba CD00 huwezi fanya lolote kwani ukiondoa misifuri italeta utata na ukashindwa jua ilikuwa wapi ila kwenye namba 0CDE tunaiondoa sifuri na kuacha CDE.
  Vilevile kwenye anuani ambazo katikati kuna misifuri miiingi,nayo tunaweza kuila panga,hii ni kwa sababu mara nyingi kwenye anuani za ndani(link local) huleta mambo kama haya ya misifuri,hivyo anuani kama FE80:CD00:0000:0000:0000:0000:211E:729C, badala ya kuondoa sifuri nne na kuacha moja kama tulivyofanya hapo juu,tunaweza kuondoa sifuri zooote zinazofuatana na
  kuwakilisha na alama ::,hivyo anuani ya juu itaonekana kama FE80:CD00::211E:729C.Kumbuka sifuri za mbele hatuzigusi.
  Kwa mtindo huu utagundua kuwa ile anuani ya Loopback ambayo kwenye IPv4 ilikuwa 127.0.0.1 na kwenye IPv6 ni 0000:0000:0000:0000:0000:0000:0000:0001,baada ya kuivunja itabakia ::1,hehe.Umeona mambo yalivyokuwa rahisi,kama unataka kuhakikisha nenda C:\Windows\System32\drivers\etc fungua faili la Host kwa kutumia notepad,kama kompyuta yako inatumia IPv6 basi utaona kuna anuani ya ::1(Kwa watu wa Vista na Windows 7 inakuja ikiwa tayari ipo).

  [​IMG]

  3.Hauitaji subnet mask za kizamani

  Kama munakumbuka,katika sehemu ambayo wengi wetu huteseka ni pale wanapotakiwa kutengeneza au kukokotoa subnet mask kwenye IPv4,binafsi nimekuwa nikipokea maswali mengi mno toka kwa watu wanaojifunza [​IMG]subneting,mambo yamekuwa rahisi zaidi.Subnet mask ni kitendo au anuani zinazopatikanika baada ya kuivunja anuani yako uliyopewa kwenye vijinetwork vidogo(subnetwork).Kwenye IPv4 subnet mask imebebwa ndani ya IP yenyewe,Si unajua IPv6 ina bit 128,basi biti 48 za kwanza zinatambulisha network na zile 16 zinazofuatia zinatambulisha network ID ambayo hutumika kutambulisha Subnet mask.Biti 64 zilizobakia zinaitwa Interface ID kwa ajili ya watumiaji(hosts).
  Ingawa siku hizi watu wameenda mbali zaidi na kuanza kutumia anuani zilizowekwa kwa ajili ya watumiaji(Interface ID) kuongezea kwenye kundi la mask kwama tulivyokuw tunachota za kwenye IPv4.Ila kwa matumizi ya kawaida haswaa kwa nyumbani,sindhani kama kuna mtu kwa siku za hivi karibuni atahitaji kwenda mbali zaidi na kutumia hizi interface id kama mask kwani mask yenye biti 16 na biti 64 kwenye device ID huweza toa subnet 65,535 na matilioni ya watumiaji.

  4.Usalama

  [​IMG]Kwakuwa ujio wa IPv6 umekuja katika kipindi ambacho matumizi ya vifaa vya mikononi ni makubwa,hivyo suala la usalama ni la muhimu kabisa,Ipv6 inatumia IPsec kama njia mojawapo ambayo huyafunga,kutoa ruhusa kwa mtumiaji na vilevile kuyakandamiza mawasiliano yote yaliyo kwenye mfumo wa IP.

  Hii inasaidia sana kuhakikisha mawasiliana yanamfikia mlengwa yakiwa kama yalivyo.Pia IPv6 imerahisisha sana matumizi ya internet kwa kuwa yao inawezesha vifaa kuhama sehemu moja hadi nyingine bila kupoteza taarifa muhimu kwakuwa kila kifaa kina anuani yake binafsi ambayo haibadiliki hata uende wapi.

  5.Hakuna broadcast kwenye IPv6

  [​IMG]Wengi wetu watakuwa wanafahamu nini maana ya broadcast,kama hufahamu,broadcast ni kitendo cha kutuma ujumbe mmoja kwa watu wengi kwa pamoja,kwa mfano magari ya matangazo ambayo yanapita barabarani ni mojawapo ya broadcast,kwenye broadcast wewe unatuma ujumbe kwa wote wanaokuzunguka,hujali nani anahitaji au la,katika internet napo hutumia broadcat kutuma taarifa kwa vyombo vingi kwa pamoja,kwakuwa broadcast ni matumizi mabaya ya hazina,kwani kuna kipindi unaweza tuma taarifa wakati hakuna hata mtu mmoja anayehitaji.

  IPv6 hutumia Multicat badala ya broadcast hata pale kifaa kinapotaka kutuma kwa wote,kwani multicat ni kitendo cha kutuma taarifa kwa wale waliojiunga tuu.Mfano mzuri ni redio au TV,wewe unatuma mawimbi ya sauti hewani,yule anayetaka atajiunga na baada ya hapo ataweza sikia.Hivyo kwenye Ipv6 multicast ndiye baba lao.


  IPv6 ni tamu na ukianza kuelezea mambo matamu yaliyo ndani yake huwezi kumaliza,hivyo tuachie hapona kama una mori wa kuifahamu zaidi IPv6 basi unaweza soma kitabu hiki.

  Faida za IPv4 kulinganisha na IPv4


  1.Anuani nyingi,hivyo hatutoishiwa anuani.

  2.Imetilia mkazo sana matumizi ya vifaa vya mikononi(Mobility).

  3.Kila kifaa kina uwezo wa kujipatia anuani yake chenyewe kwa kutumia Autoconfiguration.

  4.Mambo ya usalama ni makubwa zaidi,haswa kwa kutumia IPsec kwa mtumaji na mpokeaji.

  5.Imezingatia mgawanyo wa kijiografia (Tunapozungumzia mgawanyo huu kwenye IPv6 ninamaanisha,inafanya kazi kama vile posta na P.o Box(Postcode),kwa mfano barua iliyotumwa DSM inakuwa na anuani ya P.O ox 10XXX,ndani ya posta ya DSM nayo kuna mgawanyo ambapo Temeke kuna 103XX wakati Kinondoni kuna 102XX,hii inamaanisha anuani inajitambulisha na kuondoa utata huku ikimaanisha matumizi halisi ya mwanadamu.


  [​IMG]

  6.Vifaa vingi sasa kama PDA,kajokofu,magari nk vyote sasa vinaweza tumia IPv6.

  7.Internet inaweza kusambaa kadri iwezavyo na kufikia dunia nzima,hata sisi waafrika hatuna haja ya kuhofia uhaba wa IP tena.

  8.Wana IT wanaweza itumia IPv6 bila matatizo,hakuna mzigo mkubwa kwa watu wanaofanya kazi za IT,si umeona kuwa kwenye IPv6 subnet mask inakuja yenyewe,(ila mambo sio rahisi kama unavyoweza fikiria),hehe.

  9.Kwa wana IT watakuwa wanafahamu hili,Routing ndani ya IPv6 ni rahisi na haraka mno kwani header ya IPv6 imeondoa vitu vingi visivyo na umuhimu ambavyo huwa vinajirudiarudia,kwa mfano kwenye IPv6 sehemu ya Option huwekwa kwenye header pale tu ambapo leya za juu zinahitaji matumizi yake.Hivyo kitendo cha routing huwa ni haraka zaidi.Hii inasaidia sana kwenye QoS hususan kwenye mkandamizo wa header(Header Compression).  [​IMG]

  10.IPv6 ni rafiki wa tekinolojia mpya,aina hii ya IP imetengenezwa kuiruhusu kushirikiana na kuwezesha kufanya kazi na teknolojia mpya ambazo bado hazijavumbuliwa.

  Sasa kama IPv6 ina mifaida yote hiyo,je kwanini dunia nzima isiamue kuhamia kwenye teknolojia hiyo nzuri? Zifuatazo ni baadhi ya changamoto zinazoikabili IPv6

  1.Gharama na hofu

  Ili kuhakikisha IPv6 inafanya kazi ni lazima kuwe na wataalam wenye ujuzi wakutosha pia kuna mabadiliko ambayo yanatakiwa kufanyika,zote zinahitaji fedha,pia makampuni mengi bado yanahofu kuwa wanaweza kuingia mkenge kwa kutumia IPv6 wakati IPv4 kwa inafanya kazi kama kawaida.

  2.NAT bado inaleta usiku

  Kwa wale ambao wamewahi kucheza na mambo ya Networks,utakubaliana nami nami kuwa kwa kutumia NAT,inaweza okoa IP nyingi mno,kwa mfano kwa wale wanaotumia ile nati ya kubebesha(PAT).

  3.Wataalam

  Wataalam wengi bado hawana uzoefu au kuizoea IPv6,nimewahi kukutana na jamaa wengi ambao wameiva kwenye masuala ya networks ila kwa IPv6 ni mama mkwe,binafsi pia sijisikii amani saana pindi ninapofanya kazi kwenye IPv6,hivyo IPv6 inahitaji muda kuizoea na kuipenda.

  4.Wanyonge hawana sauti

  Kwa kuwa nchi nyingi ambazo tulinyimwa au kupunjwa IP bado hatuna mahitaji makubwa ya IP,kwa wao wazee wa juu bado wana nafasi kubwa ya IPv4 hivyo kwao IPv6 bado haina maslahi makubwa sana,ingawa wameanza kutumia.Angalia picha chini uone jinsi gani jamaa walivyojimilikisha IP,hivyo kwao hakuna hofu kwa sana kwa sasa.


  [​IMG]  Baada ya kuangalia yote kwa undani,Basi tumia muda wako kusoma zaidi kuhusu IPv6 na baada ya hapo endeleza makala hii kuchangia nini unajua,matatizo au ushauri kuhusu IPv6.
   
Loading...