Mahakama siku zote ipo kwa ajili ya kuhukumu kesi yenye ushahidi na kesi ambayo haina ushahidi inatupiliwa mbali sasa wanajamvi tujiulze kwa njia anayotumia makonda kupambana na wauza madawa ya kulevya ataweza kuwapata na ushahidi?
After thought 1 Utawezaje kuwapata na ushahidi wakati ujawachunguza na kujua njia zao wanazotumia na kuwajua washirika wao.Hivi hata ungekuwa wewe unaambiwa unatafutwa kwa kosa la kuiba TV alf ni kweli iyo TV uliiba na ipo ndani kwako kwa haraka haraka lazima tu iyo TV utaitafutia sehemu ya kuificha na wale ulioshirikiana nao kuiba lazima utawaambia wawe makini au hata wakajifiche ina maana hapo utakuwa umepoteza ushahidi na utakuwa upo tayari kwa kukabiliana na kesi hatimaye kushinda. Kwa mfano huu Makonda hatoweza kufanikiwa mwisho wa siku wauza madawa wataendelea kupeta na kuendelea kufanya biashara yao tena kwa umakini wa hali ya juu.
Nani asiyejua kuwa Dogo Hamidu or Petit Man ni wauzaji wa madawa ya kulevya mwisho siku kiko wap? si hao wameachiwa huru na wameachiwa huru kwa sababu kulikuwa hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa wao ni wauza madawa ya kulevya na saivi wapo mtaani wanapeta tu na kama wanaendelea kuuza wanazd kuuza tu na vijana wanaendelea kuangamia na madawa ya kulevya. Hapo nani mshindi kati ya Dogo Hamidu, Petit Man na Paul Makonda? jibu unalo.
After thought 2 Mkuu wa mkoa ndiye mwenyekiti wa usalama wa mkoa na wajumbe wake wakiwemo watu wa usalama na police najiulza hili analo lifanya Makonda kwa sakata la madawa ya kulevya amelipitisha na kujadiliana na kamati yake ya usalama?
Kwa uwelewa wangu nadhani hajalipitisha kwenye kamati yake ya usalama najua utaniulza unauhakika gani hajalipitisha kwenye kamati yake ya usalama? Kwanza kabisa kamati ya usalama inawakilishwa na watu makini kutoka idara mbali mbali ikiwemo usalama wa taifa na police na hizi idara zina utaratibu wake wa kufanya kazi na hawawezi kuvunja utaratibu wao wakufanya kazi katika hili la madawa ya Kulevya utaratibu haujafatwa hivi usalama wa taifa utamshutumu mtu bila kumfanyia upelelezi? lakini katika hili sakata la madawa ya kulevya utaratibu haujafatwa watuhumiwa hawajafanyiwa upelelezi ndo maana watuhumiwa wengine wameachiwa huru ingawa ni kweli ni wauzaji wa madawa ya kulevya.
Hata majina ya watuhumiwa yameandikwa kihuni huni tu yani unamuandika mtuhumiwa kwa AKA yake badala ya jina lake halisi na majina mengine yamekosewa kuandikwa mfano jina la Free Man mbowe walikosea kuandika hii inamaana kwamba walishindwa hata kuchunguza majina halisi ya watuhumiwa? kwa namna hii uwezi kubisha kwamba hili sakata ni la kukurupuka na ulopokaji na halijafata utaratibu bali mkuu wa mkoa kajiamuliya ye mwenyewe na police hawana namna inabidi wafate tu atakachosema mkuu huku wakijua utaratibu haufatwi na hauwezi kufanikiwa kupata ushahidi wa wauza madawa ya kulevya.
After thought 3 wananchi umakini umepotea na wala hawashangazwi na majina yanayotajwa badala yake wanachukulia kama wanatazama bongo move tu.Ila kama wangekuwa wanatajwa sambamba na ushahidi umakini wa wananchi ungekuwa mkubwa sana na wangeungana kuipigania hii vita ya madawa ya kulevya ila kwa sasa wanaona kama bongo move tu kwamba mwisho wake unajulikana.
After thought 4 utaratibu unaotumika kuwapata watuhumiwa siyo mzuri uwezi ukamtuhumu mtu moja kwa moja eti kwa sababu katajwa na jirani yake na bila kufanya uchunguzi unachukua jukumu la kumtuhumu huu ni uhuni na siyo utaratibu hii inamaana kila mwenye chuki na mwenzake anaweza akamtaja hata kama hausiki na madawa ya kulevya. Kwa njia anayotumia Makonda madawa ya kulevya yataendelea kuuzwa nchini na vijana wengi wataendelea kuangamia. Njia anayotumia hawezi kupata ushahidi wa muuzaji.
Tueendelee kupambana na wauzaji wa madawa ya kulevya kwa njia iliyo makini ili tuweze kuwatokomeza kabisa na kuirahisishia mahakama kufanya kazi yake kwa kuwa na ushahidi wa kutosha.