Sababu 5 za kumfanya Lowassa kuhama CCM

Sababu 5 za kumfanya Lowassa kuhama CCM

Umenena vyema Lowasa angejiunga na Chadema achukue form ya kugombea Urais, Slaa agombee ubunge waunganishe nguvu ya ukawa hapo CCM lazima iangukie pua
 
ha ha ha...naona sasa vijana wamelipwa kuja mitandaoni kutuletea porojo.
ACHENI POROJO NA KUTUMIKA...
Lowasa mwenyewe ni hatari kwa afya yake binafsi...sembuse familia yake na watanzania.
hawezi toka ccm!!
 
Mkuu Dawa GENTAMYCINE,Kwanza Lowassa sio mpendwa wangu tafadhali.Mimi najaribu kueleza possibilities.Mpendwa wangu kisiasa hapa Tz ni CHADEMA.Unafiri Lowassa hana mafundi? Kaulize kwanini fundi wa butiama alipekwa kutibiwa kwa mabepari na sio kwa wajamaa na pia uliza nini kilitokea.Kiufupi,huko kwenye mafundi ni wengi sana.

Kama Lowasa ni fundi, mbona kakatwa? Anyway sidhani kama Lowasa anapendwa na watu Kama unavyotaka tuamini, namhurumia sana maana atakuwa looser kwa mara nyingine. Pole Lowasa na team yako
 
kwanza lowasa hana cha kumfanya Kikwete. pili napingana na wewe kuwa lowasa ndo aliyemuingiza Kikwete madarakani, kwani yeye lowasa alikuwa hautaki urais? sasa anahangaikia nini? ukweli ni kwamba lowasa amesafiria nyota ya kikwete kwa muda mrefu.
tatu lowasa hata akiondoka ccm bado hawezi shinda huo urais. hao watu elfu 80 aliowahonga na media hawawezi kusaidia chochote. bado atashindwa tu. huku kijijini wanasubiria Magufuli aliyesimamia mabarabara kila kona ya nchi kuapishwa kuwa rais.

Lowassa atahama CCM na kwenda chama cha upinzani kwa sababu zifuatazo,

1. Afya yake: Lowassa anajua kuwa afya yake haipo imara sana kumfanya asogeze matumaini mbele ya kuwa rais.

2. Fedha: Lowassa ametumia pesa nyingi sana kwa ajili ya marafiki.Hatakubali kusalimu amri na kuwasaliti marafiki na wafadhili.Atagombea urais ili hata asipoupata,atapata wabunge kadhaa (marafiki) na hivyo kurejesha sehemu ya fadhila.

3. Kukubalika sana: Kwa ushawishi,Lowassa ndio amejitengenezea ushawishi mkubwa kuliko Mtanzania yeyote (Labda Dr.Slaa).

Ushawishi unatokana na rekodi ya utendaji kazi alipokuwa PM na kugawa pesa kwa makundi karibia yote.

4. Kulipa kisasi kwa Kikwete na CCM: Inasemekana kuwa Lowassa ndiye aliyemwingiza Kikwete ikulu kwa makubaliano maalum.Kikwete hajaonekana kumjali na kulipa fadhila,hivyo Lowassa anaona bora Kikwete na CCM yake wapate maumivu ya usaliti.

5. Uhakika wa kuiondoa CCM madarakani: Lowassa anakubalika na ana pesa.Anajua kabisa akiondoka ,CCM itabaki skeleton na hata kama yeye hatashinda urais,UKAWA watashinda tena kirahisi na hivyo kinga dhidi ya Kikwete na watu wake haitakuwepo na yeye atashiwishi(akiwa kama kiongozi mkuu wa upinzani) kushughulikiwa kwa Kikwete.

Kwa sababu hizi na zingine, simuoni Lowassa akiendelea kuimba iyena iyena.
 
Makashfa yake yote wanayo ccm. Hata kesi watamfungilia. Na hizi hazitakuwa kesi feki

Atakuwa anahangaika na kesi na huku anatakiwa apige kampeni.
Kila akipita watu watakuwa wanaita mwizi mwizi na nk

Ni vizuri abaki ccm
 
Nitawashangaa sana vyama vya upinzani wote kwa ujumla wao. Viongozi na wafuasi wakimpokea kwa shangwe ndugu Edward Lowassa kwenye vyama vyao baada ya kushindwa kutwaa nafasi ya kuwania urais kupitia ticket ya CCM.

Kwani wapinzani Hao Hao ndio walioibua hoja ya wizi wa Richmond na EPA iliyopelekea kujiuzulu kwa huyu ndugu ambaye ni moja kwa moja amehusika.

Kwa kitendo cha kumpokea tu. Itadhihirishia umma kwamba hawana Nia thabiti ya kuongoza Hili taifa Bali wamejaa uchu wa madaraka.

Ni hayo tu.
kama msimamo ni Lowasa kuhusika katika sakata la Richmond basi ufahamu wazi indirect unamhusisha Mkuu wa Kaya na familia yake!!! Jaribu kuangalia vizuri kisha tupe tathmini yako! Au ulitaka Mkuu wa kaya ndiye ajiuzulu???
 
asihame chama.atulie tu.asiwe wa kusema sana.ni ushauri tu
 
Hv ukawa hakuna wagombea urais mpaka tumsubiri low asa aje achukue nafas hiyo?
 
Nataka kuona tamko anahama lin hizi ngonjerA zingine acheni
 
lowasa akihamia cdm nitaipigia kura ccm milele lowasa ni messi wq ufisadi hasafishiki hata kwa dodoki
 
Back
Top Bottom