Sababu 5 za kumfanya Lowassa kuhama CCM

Sababu 5 za kumfanya Lowassa kuhama CCM

pepsin

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
3,486
Reaction score
6,172
Lowassa atahama CCM na kwenda chama cha upinzani kwa sababu zifuatazo,

1. Afya yake: Lowassa anajua kuwa afya yake haipo imara sana kumfanya asogeze matumaini mbele ya kuwa rais.

2. Fedha: Lowassa ametumia pesa nyingi sana kwa ajili ya marafiki.Hatakubali kusalimu amri na kuwasaliti marafiki na wafadhili.Atagombea urais ili hata asipoupata,atapata wabunge kadhaa (marafiki) na hivyo kurejesha sehemu ya fadhila.

3. Kukubalika sana: Kwa ushawishi,Lowassa ndio amejitengenezea ushawishi mkubwa kuliko Mtanzania yeyote (Labda Dr.Slaa).

Ushawishi unatokana na rekodi ya utendaji kazi alipokuwa PM na kugawa pesa kwa makundi karibia yote.

4. Kulipa kisasi kwa Kikwete na CCM: Inasemekana kuwa Lowassa ndiye aliyemwingiza Kikwete ikulu kwa makubaliano maalum.Kikwete hajaonekana kumjali na kulipa fadhila,hivyo Lowassa anaona bora Kikwete na CCM yake wapate maumivu ya usaliti.

5. Uhakika wa kuiondoa CCM madarakani: Lowassa anakubalika na ana pesa.Anajua kabisa akiondoka ,CCM itabaki skeleton na hata kama yeye hatashinda urais,UKAWA watashinda tena kirahisi na hivyo kinga dhidi ya Kikwete na watu wake haitakuwepo na yeye atashiwishi(akiwa kama kiongozi mkuu wa upinzani) kushughulikiwa kwa Kikwete.

Kwa sababu hizi na zingine, simuoni Lowassa akiendelea kuimba iyena iyena.
 
Karibu Ukawa Lowassa umuunge mkono Dr Slaa nasi tutakuwa Pamoja nawe
 
na pia kuna sababu 5 zitazomfanya asitoke
1. Afya yake: pamoja na Afya dhoofu hakuna anayependa kufa bwana sasa athubutu kutoka aone kilichompata Mwakyembe na wengine wengi
2: pesa: Hizo pesa alizotumia ni ndogo kuliko alizonazo sasa kama anataka afilisike basi athubutu tu.
3: Ushawishi: hana ushawishi wowote zaidi ya kujitekenya yani kashindwa kuwashawishi kina mkapa,karume,msekwa apite hata 5 bora tu. Na hii si kwa kupenya tu hata mgombea ambaye watu wake waliamua kumpa kura yule Amina
hakupata hata nusu ya kura zote.Watu waliokuwa wakimsapoti jana hiyo hiyo wengine washamgeuka hiyo ni dhahiri kuwa aikuwa akijitekenya na kucheka mwenyewe
4: Mapenzi kwa Familia yake: Atakuwa mpumbavu kuharibu future ya watoto wake
5: Legacy: Pamoja na kuzongwa na shutuma kibao bado ana heshimika sana ambavyo yupo ndani ya CCM athubutu atoke hata tofautiana na Zitto kupambana na mfumo au Taasisi hata iwe chafu vipi inahitaji kujikana nafsi na ushindi wako utakuwa kwa asilimia 100 kama wewe utakuwa pure clean{Msafi Halisi} jambo ambalo lowassa hana na any trial ataishia kupata Aibu kuliko aliyoipata. kuna muda lazima ukubari kuwa kafara na kama anahitaji kuwa Rais wa hii nchi kwa watu wanaoona mbali mara 100 atumie kila mbinu aandae damu yake yani mtoto wake au mjukuu dreams zipo na inaweza kuwa accomplished hata baada ya vizazi shida ni ubinafsi tulionao Ingekuwa mimi ndo yeye ningeanza kumuandaa mwanangu tu
 
Hii namba 3 Kukubalika sana: Kwa ushawishi,Lowassa ndio amejitengenezea ushawishi mkubwa kuliko Mtanzania yeyote (Labda Dr.Slaa).

Mnajidanganya nyinyi pamoja na kumdanya Dr.Slaa.
 
Nitawashangaa sana vyama vya upinzani wote kwa ujumla wao. Viongozi na wafuasi wakimpokea kwa shangwe ndugu Edward Lowassa kwenye vyama vyao baada ya kushindwa kutwaa nafasi ya kuwania urais kupitia ticket ya CCM.

Kwani wapinzani Hao Hao ndio walioibua hoja ya wizi wa Richmond na EPA iliyopelekea kujiuzulu kwa huyu ndugu ambaye ni moja kwa moja amehusika.

Kwa kitendo cha kumpokea tu. Itadhihirishia umma kwamba hawana Nia thabiti ya kuongoza Hili taifa Bali wamejaa uchu wa madaraka.

Ni hayo tu.
 
Alisema haamini katika visasi

Ninachojua kwa Lowasa ni bingwa wa kupiga kimya
 
Lowassa atahama CCM na kwenda chama cha upinzani kwa sababu zifuatazo,

1. Afya yake: Lowassa anajua kuwa afya yake haipo imara sana kumfanya asogeze matumaini mbele ya kuwa rais.

2. Fedha: Lowassa ametumia pesa nyingi sana kwa ajili ya marafiki.Hatakubali kusalimu amri na kuwasaliti marafiki na wafadhili.Atagombea urais ili hata asipoupata,atapata wabunge kadhaa (marafiki) na hivyo kurejesha sehemu ya fadhila.

3. Kukubalika sana: Kwa ushawishi,Lowassa ndio amejitengenezea ushawishi mkubwa kuliko Mtanzania yeyote (Labda Dr.Slaa).

Ushawishi unatokana na rekodi ya utendaji kazi alipokuwa PM na kugawa pesa kwa makundi karibia yote.

4. Kulipa kisasi kwa Kikwete na CCM: Inasemekana kuwa Lowassa ndiye aliyemwingiza Kikwete ikulu kwa makubaliano maalum.Kikwete hajaonekana kumjali na kulipa fadhila,hivyo Lowassa anaona bora Kikwete na CCM yake wapate maumivu ya usaliti.

5. Uhakika wa kuiondoa CCM madarakani: Lowassa anakubalika na ana pesa.Anajua kabisa akiondoka ,CCM itabaki skeleton na hata kama yeye hatashinda urais,UKAWA watashinda tena kirahisi na hivyo kinga dhidi ya Kikwete na watu wake haitakuwepo na yeye atashiwishi(akiwa kama kiongozi mkuu wa upinzani) kushughulikiwa kwa Kikwete.

Kwa sababu hizi na zingine, simuoni Lowassa akiendelea kuimba iyena iyena.

Wakati Akijiandaa Kuhama CCM Kama Wewe Unavyomshabikia Na Kumtaka Afanye Hivyo Usisahau Pia Kumuuliza Je Anayakumbuka Ya Imran Kombe? CCM Yetu Ni Zaidi Ya CIA, MOSSAD, FSB/KGB Na Scotland Yard. Wewe Unadhani Kwanini Nakipenda Hiko Chama? Kimejaa MAFUNDI Watupu Na Moja Ya UFUNDI Kilichouonyesha Ni Kitendo Cha Kuwamaliza KIMAFIA Na KIJASUSI Akina Lowassa Na Mwezie Membe Bila Ya Hata Wao Kujua. Narudia Tena Kukuambia CCM Kumejaa MAFUNDI Watupu Na Wanaojua Michezo Yote Ya Hatari Na Ya Kibusara Unayoijua Wewe. Najua Wapo Watu Wengi Ningekupa Mifano Yao ILA Nimekutajia Tu Huyo Marehemu Brigadier General Imran Kombe Kwa Makusudi Na Nakutaka UTAFAKARI Kwa Kina Halafu Ukilipata Jibu Mfikirie Na Huyo Mpendwa Wako Unayemtetea Na Kumuonea Huruma a.k.a NIMEKATWA, NINA HASIRA Na UCHUNGU ( EL ).
 
Hii namba 3 Kukubalika sana: Kwa ushawishi,Lowassa ndio amejitengenezea ushawishi mkubwa kuliko Mtanzania yeyote (Labda Dr.Slaa).

Mnajidanganya nyinyi pamoja na kumdanya Dr.Slaa.
Hapa anayedanganywa ni Dr. Slaa au Lowassa?
 
Hii namba 3 Kukubalika sana: Kwa ushawishi,Lowassa ndio amejitengenezea ushawishi mkubwa kuliko Mtanzania yeyote (Labda Dr.Slaa).

Mnajidanganya nyinyi pamoja na kumdanya Dr.Slaa.
Vipi ile kete yenu ya dini utaitumiaje kwa John Pombe Magufuli?
 
Vipi ile kete yenu ya dini utaitumiaje kwa John Pombe Magufuli?
Hamna kete ya udini mnajiogopesha tu wenyewe, Magufuli mbona kijana wa JK unadhani ili limetokea bahati mbaya kazi ya kwanza ya Magufuli kaambiwa mchague Samia mara moja mgombea mwenza.

Nikuambie kitu CCM hata wamsimamishe Mzee Majuto bado atamtupa mbali Dr.Slaa.

Vipi UKAWA nasikia kila siku Mbowe na wenzake wanajifungua kutafuta mgombea lini mtamtangaza?
 
Watz ni watu wajinga sana. Sio watu wa kufikiria na wala kudadavua jambo,zaidi ya ushabiki.
Tuache ushabiki wa jambo hapa. Tuangalie mustakabali wa nchi. cCm au ukawa ndio nani? Wakati wao ndio wanategemea kupata kura yako kuingia ikulu?

Mawazo yangu juu ya kuhama kwa lowassa CCM mimi nathani ni brilliant. Watu wanamtaka lowasaa na je CCm watakuwa na lipi la kumpinga kama akiamua kuwa mgombea wa upinzani?
Ukawa wanaweza kumsafisha kilaini sana... Kumbuka watz wanataka mabadiliko. Kikwete pia ni wa kupelekwa mahakamani yeye na wenzake. Mwaga ugali na mwaga mboga.
 
aminiusiamini nakubaliana na wewe kwa namna moja au ingine.
CCM inaonekana ni chaka la kwenda kujifichia watu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Dawa GENTAMYCINE,Kwanza Lowassa sio mpendwa wangu tafadhali.Mimi najaribu kueleza possibilities.Mpendwa wangu kisiasa hapa Tz ni CHADEMA.Unafiri Lowassa hana mafundi? Kaulize kwanini fundi wa butiama alipekwa kutibiwa kwa mabepari na sio kwa wajamaa na pia uliza nini kilitokea.Kiufupi,huko kwenye mafundi ni wengi sana.
Wakati Akijiandaa Kuhama CCM Kama Wewe Unavyomshabikia Na Kumtaka Afanye Hivyo Usisahau Pia Kumuuliza Je Anayakumbuka Ya Imran Kombe? CCM Yetu Ni Zaidi Ya CIA, MOSSAD, FSB/KGB Na Scotland Yard. Wewe Unadhani Kwanini Nakipenda Hiko Chama? Kimejaa MAFUNDI Watupu Na Moja Ya UFUNDI Kilichouonyesha Ni Kitendo Cha Kuwamaliza KIMAFIA Na KIJASUSI Akina Lowassa Na Mwezie Membe Bila Ya Hata Wao Kujua. Narudia Tena Kukuambia CCM Kumejaa MAFUNDI Watupu Na Wanaojua Michezo Yote Ya Hatari Na Ya Kibusara Unayoijua Wewe. Najua Wapo Watu Wengi Ningekupa Mifano Yao ILA Nimekutajia Tu Huyo Marehemu Brigadier General Imran Kombe Kwa Makusudi Na Nakutaka UTAFAKARI Kwa Kina Halafu Ukilipata Jibu Mfikirie Na Huyo Mpendwa Wako Unayemtetea Na Kumuonea Huruma a.k.a NIMEKATWA, NINA HASIRA Na UCHUNGU ( EL ).
 
Hii namba 3 Kukubalika sana: Kwa ushawishi,Lowassa ndio amejitengenezea ushawishi mkubwa kuliko Mtanzania yeyote (Labda Dr.Slaa).

Mnajidanganya nyinyi pamoja na kumdanya Dr.Slaa.

mfia chama
 
salaam wana JF

sabab sita za lowasa kugombea urais kupitia upinzani

1.umri
umri wa Lowasa umeenda hawez tena subir miaka mingine 10

2.kukubalika
tunajua waliomkata lowasa ni kikundi tu cha watu wachahe wenye nguvu huko ccm
ila Wananchi wa kawaida wanamkubali sana lowasa

3.maono na vipaumbele (vision & priorities)
lowasa ana maono ya taifa la watu walio elimika ivo kaweka elimu kma kipaumbele chake contrary na mgombea wa ccm hana dira wala mwelekeo zaid ya ilani ambayo utekelezaji wake ni wa mwendo wa kobe huku waTZ tukiwa na shauku kubwa ya maendeleo ya kasi

4. ufedhuli wa wazi alifanyiwa
lowasa ana kila sabab ya ku fight back kwa uonevu wa wazi aliofanyiwa na vigogo ccm

5.kuimarisha upinzani
wanasema power without control is nothing
upinzani kwa hivi karibuni umekuwa na nguvu kubwa sana ya ushawish tatizo wamekosa central figure kuweza ku balance power
kma Lowasa anajitupa upinzan naona TZ yenye vyama vikubwa viwili kma ilivyo US na england

6.hana cha kupoteza
lowasa ana mengi ya kupoteza akiendelea baki CCM
heshima yake, had watu kma Nape nao wanampiga kibesi

kma wazungu wanavyo sema "you have zero chance of success unless you try"

ni vyema lowasa akajaribu gombea urais kupitia upinzani akataliwe na wananchi kuliko kukataliwa na kikundi kidogo cha wana CCm
 
Back
Top Bottom