Gurta
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 2,233
- 532
Habarini,
Nimeona mahali makala inayojaribu kuangalia sababu zinazolekea mahusiano, hasa ya wakati huu tuliopo, yasivyodumu na jinsi inavyokuwa rahisi kwetu kuyavunja.
1. Hakuna utayari. Upweke tu ndio unaotuingiza mahusianoni, na tunajikuta tuko kwenye mahusiano na watu 'wasiotufaa'.
2. Hatuweki nafasi ya mapenzi (mahaba?). Ulimwengu na masaibu yake yanapelekea wengi wetu kuamua kuwa wapweke. Pia tumeondoa nafasi ya kutaka kuwa na wengine, tunajiingiza kwenye mambo wala yasiyo ya msingi kama internet, magemu ya video n.k.
3. Hatujui namna ya kuwasiliana. Tunaogopa 'kuwasiliana', hatuchukulii yale tunayoambiwa kwa uzuri wake badala yake yanatuumiza na kutufanya tuwe wenye wivu usio kuwa na maana.
4. Tunataka kutangatanga tu. Mapenzi yanahitaji kujuana kwa muda, lakini siku hizi tunafanya utalii tu na 'kuzurura'.
5. Tume'jikomboa' au kukombolewa kingono. Siku hizi hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya ngono (kufanya mapenzi) na mapenzi (mahaba?). One night stand, na madudu kama hayo ni kitu cha kawaida. Wakati mwingine hata baada ya kupata tunachokitaka, yakiwemo mapenzi, bado tunataka kufanya 'utembezi' na kuonja kwingine.