the great wizard
JF-Expert Member
- Dec 21, 2015
- 1,482
- 887
Kipigo cha mabao 4 kwa 0 toka kwa PSG kiliamsha hisia tofauti kwa mashabiki wa Barcelona.Wengi walifedheheshwa sana na kipigo hicho cha aibu.Swalu kubwa limekuja kuhusu uwezo wa kocha wa Barcelona Luis Enrique,je ana uwezo sahihi kuwa kocha wa Barcelona.Wengi wameonekana kutokukubaliana na uwezo wake.Ushindi wa dakika za lala salama dhidi ya Athletico Madrid ulitilia shaka kuhusu uwezo wa Enrique na japo mpira unadunda lakini kuna asilimia kubwa kwamba Barcelona wameshachungulia mlango wa kutoke UEFA.
Jorge Sampaoli kocha wa Sevilla amekuwa gumzo sana katika ligi ya Hispania.Uwezo wa Sampaoli umewashtua wengi kwani hadi sasa Sampaoli yuko katika mbio moja na Real Madrid na Barcelona wote wanataka ubingwa.Uwezo wake mkubwa umemfanya ahusishwe sana na kujiunga na klabu ya Barcelona.Miaka kadhaa iliyopita alitajwa miongoni mwa makocha watatu bora duniani.Sampaoli ni kama anaudai mpira kwa kuwa akiwa na miaka 19 tu alilizimika kuacha kucheza soka baada ya kuvunjwa miguu yote miwili.Kwanini Sampaoli na sii mwingine?
AINA YA MPIRA.Sampaoli anapenda kushambulia,ni aina ya kocha ambaye mara zote na timu zote anazofundisha huwa anashambulia tu.Toka enzi za “Dream Team” ambapo ni jina la timu ya Barcelona ililopewa kipindi inafundishwa na Johan Cryuf hadi hivi leo zama za Enrique,Barcelona hawakai nyuma wamekuwa timu ya kushambulia mwanzo mwisho.Mchezo wa kwanza wa Sampaoli La Liga ilikuwa dhidi ya Espanyol na waliwafunga bao 6 kwa 4,mechi hii ilikuwa ushahidi tosha wa aina ya mbinu za Sampaoli.Alipokuwa Chile alionekana kuwaunganisha Artulo Vidal,Edurdo Vargas na Alexis Sanchez kutengeneza kikosi ambacho kilionekana na safu ya ushambuliaji hatari sana kombe la dunia.Mfumo wake wa 3-4-3 ni kati ya mbinu inayowapa tabu sana wapinzani wake.Ni mtu sahihi kabisa kuwa kocha wa MSN.
UNYUMBULIKO WA MBINU.Moja kati ya matatizo makubwa ya Luis Enrique ni kukosa Plan B.Mara nyingi ambazo mbinu zake zinashikwa na wapinzani huwa anabaki kama mtu asiyejua ni nin afanye.Sampaoli amwonekana na mbinu mpya kila siku,kama umebahatika kuwaona Sevilla unaweza kushudia anavyomtumia Samir Nasri na Steven N’zonzi.Nasri amekuwa bora sana chini ya Sampaoli huku akicheza nafasi tofauti kutokana na Sampoli anavyotaka.Hatumii tu 3-4-3 bali michezo mikubwa mingi formation hii inaonekanaga kubadilika akicheza 4-3-3 na 4-4-2 pale inapohitajika.
IDEA MPYA ZA SOKA.Unaweza kumuona Lioneil Messi,amekuwa Messi yule yule wa mwaka 2014 akicheza vile vile habadiliki.Barcelona imekwama kimbinu na inahitaji mtu mpyaa kuwapa kitu kipya.Wanachofanya Barcelona leo ndio kilichofanywa miaka kadhaa iliyopita,sitaki kuamini kwamba kipindi chote hicho wapinzani wameshindwa kuona wanachofanya Barcelona.Ni jambo jema kwa timu kuamini katika philosophy yao ya soka,lakini kama philosophy yenu inashindwa kuwapa mutakacho kwanini ing’ang’aniwe?.Barcelona wanataka kuwa tishio tena duniani kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.Sii kwamba Barcelona wanashuka kiwango laa hasha bali wapinzani wanapanda kiwango.Mtu mpya anatakiwa kuja kuwarudisha walipokuwa na ni Jorge Sampaoli.