Saashisha Mafuwe - Shime Wananchi wa Jimbo la Hai, Twendeni Tukajiandikishe

Saashisha Mafuwe - Shime Wananchi wa Jimbo la Hai, Twendeni Tukajiandikishe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,428

SAASHISHA MAFUWE ATOA SHIME KWA WANANCHI WA JIMBO LA HAI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA WA SERIKALI ZA MITAA

"Tunaenda kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatanguliwa na wananchi kujiandikisha, wakazi wa Kijiji, mtaa husika wanapaswa kwenda kwenye maeneo yao kwenye vituo kwa lengo la kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro

"Ni haki ya kikatiba ya kila mmoja ya kwenda kujiandikisha, ni haki ya kiraia na ni wajibu wetu kama Watanzania kama wananchi wa Jimbo la Hai kujitokeza kujiandikisha ili tuweze kupata nafasi ya kupiga kura kwa maana ya Mwenyekiti wa Kitongoji, Kijiji na Mtaa"

"Kumekuwa na sintofahamu kwa baadhi ya Wananchi kudhani kuwa ukiwa na Kitambulisho cha Mpiga Kura kuwa huna haja ya kwenda kujiandikisha, la hasha! Hili ni zoezi la Serikali za Mitaa ambalo kila mmoja unaenda kujiandikisha jina lako kwenye Daftari"

"Uandikishaji wa Daftari la sasa hatutatumia Kitambulisho cha Mpiga Kura ambacho tunacho wala Kitambulisho cha Uraia. Hili ni zoezi la kila mmoja wetu ili upate sifa ya kupiga kura kwenye eneo unaloishi"

"Hii ni nafasi ya kipekee inayompa mwananchi kupitia haki yake ya kikatiba kwenda kuchagua Kiongozi wa Serikali za Mitaa. Hapa unapata nafasi ya kuamua nani awe Mwenyekiti wa Kitongoji, Kijiji au Mtaa. Usipochukua hatua ya kujiandikisha tangu tarehe 11 - 20 Oktoba, 2024 utakuwa umepoteza haki ya kupiga kura na kupigiwa kura"

"Ili uweze kupiga kura na kupigiwa kura ni lazima uonekane kwenye Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa. Ni zoezi la muda mfupi sana, unaulizwa jina lako na taarifa chache kisha unaondoka, hakuna foleni"

"Nitoe Shime kwa wananchi wa Jimbo la Hai, sisi zaidi tuna kila sababu ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais, tumekuwa wanufaika wazuri wa Maendeleo yetu, kwenye miradi yote"

"Kama miaka 20 iliyopita Wilaya ya Hai ni kama tulienda rikizo. Leo Mheshimiwa Rais ametuletea miradi ya Barabara wakandarasi wapo wanaendelea na ujenzi. Tumefungua Barabara za Mitaa na Vijiji. Tuna Vituo 5 vipya vya Afya vimejengwa. Shule 6 mpya, Chuo Kikuu, huduma ya Maji, Skimu 5 za Umwagiliaji na mkandarasi ameshapatikana" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-10-18 at 09.36.46.mp4
    21.2 MB
Back
Top Bottom