Mbatizaji Mkuu
Member
- Jul 19, 2020
- 39
- 128
Mapema Baada ya kuapa ndani ya Bunge la 12 Mjini Dodoma, Mbunge wa Hai Saashisha Mafuwe akihojiwa na chombo cha Habari cha Dar Mpya amenukuliwa akisema.
Jimbo la Hai lilikosa uwakilishi sahihi kwa zaidi ya miaka 15 na ndicho kilichomsukuma yeye kwenda kuchukua nafasi hiyo maana wananchi wa Hai walichoshwa na uwakilishi wa kiharakati ulikokuwa unalenga masuala binafsi na sio mahitaji ya WanaHai.
"Tulikuwa hatuna uwakilishi sahihi katika jimbo letu, nikaamua niende kugombea ili nitoe uwakilishi sahihi kutoka chama sahihi na kwa serikali sahihi.
Saashisha Mafuwe ameendelea kusema Watu wa Hai walikuwa na uchumi mzuri kabla ya kuingia kwa chama cha upinzani katika jimbo hilo hali iliyofanya kukosekana kwa kiungo kati ya wananchi na Serikali yao.
Saashisha ameng'ara sana kwenye kampeni zake kutokana na Sera yake ya kilimo na viwanda akijinasibu kufufua na kuuhuisha upya Kilimo cha mazao ya asili na mapya katika jimbo hilo ili kuujenga uchumi wa mtu mmojammmoja, Kwa upande wa vijana amedai atahakikisha mikipo yao kutoka taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi inawafikia ili wawekeze kwenye kilimo.
"Jimbo la Hai lina ukanda rafiki sana kwa kilimo cha aina zote, tuna mito mikubwa mitatu inayotiririsha maji Januari mpaka December ,tunayo mifereji ya Asili,Ardhi yenye rutuba hivyo tutafanya kilimo cha Biashara ili tupate faida kwajili ya kuujenga uchumi wa mtu mmojammoja"
Saashisha anasema watu wa hai wanasherekea ushindi wa Chama cha mapinduzi na Uapisho wake kwa kuwa lilikuwa ni hitaji lao la muda mrefu,Pia amesema uchaguzi katika jimbo la Hai ulikuwa huru na haki.
View attachment 1624608