Saa za gharama zawaponza maafisa FIFA

Saa za gharama zawaponza maafisa FIFA

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713


140918181027_parmigiani_fleurier_watch_624x351_parmigianifleurier.jpg
​

Shirikisho la soka la dunia FIFA, limewaambia viongozi wanaounda kamati ya utendaji na viongozi wengine wa juu wa shirikisho hilo kurejesha saa zipatazo 65 za gharama walizopokea kama zawadi kipindi cha kuelekea kombe la dunia huko Brazil mwaka huu.

FIFA imesema kitendo cha kurejesha saa hizo ni kutunza nidhamu.

Saa hizo zinakadiriwa kuwa na gharama ya dolla elfu ishirini na tano kila moja na zinatakiwa ziudishwe Octoba 24 ,mwaka huu.

Saa hizo za kumbukumbu ya Parmigiani ziligawiwa na shirikisho la soka la Brazili (CBF) wakati wa mkutano wa maandalizi wa FIFA uliofanyika mjini Sao Paulo.

FIFA imesema kuwa kanuni za maadili zinazuia viongozi kupokea zawadi ambazo zinathamani zaidi au zenye kuonesha ishara fulani.

Inasemekana kwamba saa hizo zitatolewa kwa taasisi zinazojitegemea na si sile zinazojali maslahi huko Brazili.

CHANZO:
BBC

 
Rais wa UEFA, Michael Platini amegoma kurudisha akidai kama FIFA waliona sio sawa wao kupewa hizo saa, wangezichukua mda huo huo walipokabidhiwa.

Huyu jamaa sijui kashaihonga hiyo saa?
 
Rais wa UEFA, Michael Platini amegoma kurudisha akidai kama FIFA waliona sio sawa wao kupewa hizo saa, wangezichukua mda huo huo walipokabidhiwa.

Huyu jamaa sijui kashaihonga hiyo saa?

Hahhahaha. ...ss si ilikua yake!! Awaambie tu imepotea wanunue wapeleke kwa jina lake!
 
Sasa inakuwaje unapewa zawadi halafu unarudisha kwa aliyekupa ndio mtindo gani huo
 
wajanja washapiga chezo hapo sio bure kwa kweli..
 
Back
Top Bottom