Saa 48 ngumu kwa wachezaji Simba!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,439
Wakuu,

Kocha mkuu Benchika inasemekana amenyoosha rula. Rula yenyewe sio ombi ni maelekezo kwa viongozi!

Huyu anaweza kuwa kocha wa kwanza wa kigeni asiyeogopa mtu kwenye kazi yake. Aliletewa mtu ikabidi apitie mlango wa trial akamla kichwa fasta bila kuuliza aliyemleta

Inasemekana akitokea popote kambini ni kama Simba mwenye hasira ameingia na wachezaji wanamuogopa, hataki mchezo na mipango yake.

Sasa huko ametoa profile anataka washambuliaji wa aina gani na sio vinginevyo. Kuna majina vipenzi vya mashabiki yapo hati hati watu wanatafutana kuweka mambo sawa

Ila tutatoboa tu! Simba nguvu moja
 
Msimamo ndo unaofaa hakuna kuwaangalia watu machoni, ingawa wengine wanaogopa je akiwaacha baadhi ya wachezaji timu itakuja kupata chemistry mapema? Watu kama hawa ni kuwaaga tu kiroho paka

1.Saido ( umri umeenda )
2.Chama (nidhamu na umri)
3.Kramo ( mchezaji kamaliza msimu bila kucheza majeraha sugu
4.Bocco ( huyu umri na hana msaada tena)
5.Kennedy ( huyu yupo yupo tu)
6

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa, hatujazoea makocha wasioyumba na wenye misimamo ila itabidi tuzoee tu.
 
Kama ni ya kweli basi ngoja tuone, nijuavyo mimi BENCHKHA ni zile type za watu ambao wao wakilala wakiamka wanawaza kazi zao tu yaani yupo tayari ashinde ofisini siku tatu bila kukanyaga kwake, pia ni mtu wa misimamo mikali, anachojali yeye ni mafanikio full stop. ukimletea za kuleta anakuondoa au anakuachia kazi yako, pia ni mtu anayekwazika haraka yaani hasira zipo shingoni, ni mtu anayejali sana cv yake na mafanikio yake ni mtu asiyependa kelele wala kukosolewa mwisho kabisa ni mtu asiyeishi kwa kutegemea sifa za mashabiki yeye huamini ktk mipango yake. AKIMALIZANA NA WACHEZAJI ANAYEFUATA NI MANGUNGU NA TRY AGAIN tofauti na hapo atawaachia timu yenu kabla ya krismas
 
Chama na Ntibanzokiza hata asijiulize mara mbili
Muweke na onana...kiufupi wageni wa kubaki kwa upande wangu naona.
1.Ngoma
2.Kanute
3.Sarr(kwasababu ndo ameaajiriwa)
4.Inonga
5.Chemalone
6.Ayubu

Wa kupewa angalizo msimu uliobaki wawe
1.Phiri
2.Miqson
3.Kramo

Waliobaki piga panga tukianza na hawa
1.Onana
2. Saido
3.Baleke
4.Chama

Kwa wazawa

1.Bocco
2.Bocco
3.Bocco
4.Bocco
5.Bocco
6......
7......
 
Msimamo ndo unaofaa hakuna kuwaangalia watu machoni, ingawa wengine wanaogopa je akiwaacha baadhi ya wachezaji timu itakuja kupata chemistry mapema? Watu kama hawa ni kuwaaga tu kiroho paka

1.Saido ( umri umeenda )
2.Chama (nidhamu na umri)
3.Kramo ( mchezaji kamaliza msimu bila kucheza majeraha sugu
4.Bocco ( huyu umri na hana msaada tena)
5.Kennedy ( huyu yupo yupo tu)
6

Sent using Jamii Forums mobile app
ongezea;
Mwanuke
Hamis cha Urembo
Chilunda
Sarr

Ingiza kikosi cha I mara kwa mara;
Huseein Kazi.
Isra Mwenda.
Kabaraka.
Abel
 
Kama ni ya kweli basi ngoja tuone, nijuavyo mimi BENCHKHA ni zile type za watu ambao wao wakilala wakiamka wanawaza kazi zao tu yaani yupo tayari ashinde ofisini siku tatu bila kukanyaga kwake, pia ni mtu wa misimamo mikali, anachojali yeye ni mafanikio full stop. ukimletea za kuleta anakuondoa au anakuachia kazi yako, pia ni mtu anayekwazika haraka yaani hasira zipo shingoni, ni mtu anayejali sana cv yake na mafanikio yake ni mtu asiyependa kelele wala kukosolewa mwisho kabisa ni mtu asiyeishi kwa kutegemea sifa za mashabiki yeye huamini ktk mipango yake. AKIMALIZANA NA WACHEZAJI ANAYEFUATA NI MANGUNGU NA TRY AGAIN tofauti na hapo atawaachia timu yenu kabla ya krismas
Mkuu Mangungu na Try again hao kuwatoa pale ofisini ni ngumu labda uchome ofisi
 
Wakuu,

Kocha mkuu Benchika inasemekana amenyoosha rula. Rula yenyewe sio ombi ni maelekezo kwa viongozi!

Huyu anaweza kuwa kocha wa kwanza wa kigeni asiyeogopa mtu kwenye kazi yake. Aliletewa mtu ikabidi apitie mlango wa trial akamla kichwa fasta bila kuuliza aliyemleta

Inasemekana akitokea popote kambini ni kama Simba mwenye hasira ameingia na wachezaji wanamuogopa, hataki mchezo na mipango yake.

Sasa huko ametoa profile anataka washambuliaji wa aina gani na sio vinginevyo. Kuna majina vipenzi vya mashabiki yapo hati hati watu wanatafutana kuweka mambo sawa

Ila tutatoboa tu! Simba nguvu moja
Kama kocha hakubaliani na wachezaji nami nuunga mkono.

Hata akiwakataa asilimia 75 ya wachezaji waliopo ni sawa kabisa.

Timu haina morali,wachezaji hawajitumi,wengi wanajiona wana vipaji vya hali ya juu kumbe hakuna lolote.

Wanacheza kama vile hawali chakula,hawana kasi hata kama kuna gap la kukumbia
 
Msimamo ndo unaofaa hakuna kuwaangalia watu machoni, ingawa wengine wanaogopa je akiwaacha baadhi ya wachezaji timu itakuja kupata chemistry mapema? Watu kama hawa ni kuwaaga tu kiroho paka

1.Saido ( umri umeenda )
Mkimuacha huyu mtajuta
2.Chama (nidhamu na umri)
Nidhamu!? Anyways labda
3.Kramo ( mchezaji kamaliza msimu bila kucheza majeraha sugu
Sasa amesharudi na baada ya kurudi akaomba abadilishiwe jezi na uongozi umempa nyingine ma ile ya Kramo akapewa avae yule wa Majaribio matokeo yake na yeye ile jezi ikamtandika ma kuonekana kama tembele mbele ya meza yenye makuku, vitimoto na na mbuzi choma
4.Bocco ( huyu umri na hana msaada tena)
Mvumilieni kwa misimu miwili zaidi hadi hapo Aishi Manula atakapokuwa tayari.
 
Wakuu,

Kocha mkuu Benchika inasemekana amenyoosha rula. Rula yenyewe sio ombi ni maelekezo kwa viongozi!

Huyu anaweza kuwa kocha wa kwanza wa kigeni asiyeogopa mtu kwenye kazi yake. Aliletewa mtu ikabidi apitie mlango wa trial akamla kichwa fasta bila kuuliza aliyemleta

Inasemekana akitokea popote kambini ni kama Simba mwenye hasira ameingia na wachezaji wanamuogopa, hataki mchezo na mipango yake.

Sasa huko ametoa profile anataka washambuliaji wa aina gani na sio vinginevyo. Kuna majina vipenzi vya mashabiki yapo hati hati watu wanatafutana kuweka mambo sawa

Ila tutatoboa tu! Simba nguvu moja

Simba inapendwa ila haipendeki!

Mambo ya kifamilia haya, tuwaache mpambane sie twaenda zetu shamba!
 
Mkuu Mangungu na Try again hao kuwatia pale ofisini ni ngumu labda uchome ofisi
nimesema hivyo kwa sababu hata akifukuza hao akina ntibanzokiza ataletewa type hiyo hiyo ya wachezaji si unaona ingizo jipya BABACAR SARR unaweza kuniambia kaletwa na nani hapo simba?
 
Muweke na onana...kiufupi wageni wa kubaki kwa upande wangu naona.
1.Ngoma
2.Kanute
3.Sarr(kwasababu ndo ameaajiriwa)
4.Inonga
5.Chemalone
6.Ayubu

Wa kupewa angalizo msimu uliobaki wawe
1.Phiri
2.Miqson
3.Kramo

Waliobaki piga panga tukianza na hawa
1.Onana
2. Saido
3.Baleke
4.Chama

Kwa wazawa

1.Bocco
2.Bocco
3.Bocco
4.Bocco
5.Bocco
6......
7......
Onana unamjua visuri na unamjua unamuongelea nani?Onana ni mchezaji wa kimataifa nakushauri uachane na wivu na roho mbaya...
 
Back
Top Bottom