Ili Tanzania tusiingie katika mkuMbo huo ni lazima tufanye mambo matatu katika kubadilisha katiba yetu.
(1) Tupunguze madaraka na mamlaka ya rais.
(2) Tuongeze uhuru na mamlaka za mahakama na bunge visiogope mamlaka ya rais.
(3) Tuongeze uhuru na mamlaka za tume ya utumishi serikalini na tume ya uchaguzi ziwe huru na ziwe na mamlaka mazito ya kushindana na yale ya raisi katika majukumu yake.