Rwanda yalalamikia Marekani kwa vikwazo

Rwanda yalalamikia Marekani kwa vikwazo

Luggy

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2012
Posts
3,737
Reaction score
3,320
[h=1]Rwanda yalalamikia Marekani kwa vikwazo[/h]

Jeshi la Rwanda limepuuzilia mbali hatua ya Marekani kuiwekea vikwazo kuhusiana na madai ya watoto kutumiwa kupigana kama wanajeshi katika vita ambavyo Rwanda inadaiwa kuunga mkono waasi wa M23 ndani ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Shirika la habari la AFP lilimemnukuu msemaji wa jeshi la Rwanda akisema kuwa sio haki kwa Rwanda kuadhibiwa kwa mambo ambayo hayafanyiki ndani ya mipaka yake wala kutekelezwa na jeshi la Rwanda

Joseph Nzabamwita alisema kuwa hatua ya kujumlisha Rwanda kuwa miongoni mwa nchi zinazotumia watoto kama wanajeshi haina misingi hata kidogo.

Umoja wa mataifa unatuhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 katika harakati zao dhidi ya serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo madai ambayo Rwanda imekana.
Mnamo siku ya Alhamisi naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani kuhusu maswala ya Afrika Linda Thomas-Greenfield alisema kuwa Marekani inatumia sheria ya kuwalinda watoto ya mwaka 2008 katika kuiwekea Rwanda vikwazo ili ikome kujihusisha na vita ndani ya DRC hususan katika kuwasajili watoto kama wanajeshi.
Kwa mujibu wa afisaa mkuu katika idara ya mambo ya nje alisema kuwa hatua hiyo itaifanya Rwanda kunyimwa msaada wa kijeshi katika mwaka 2014.
Nzabamwita alinukuliwa na AFP akisema kuwa Marekani inafahamu fika kuwa Rwanda haijawahi kuunga mkono utumiaji wa watoto kama wapiganaji na kuwa licha ya vikwazo hivyo Rwanda itaendelea kushirikiana na Marekani.
Kundi la waasi la M23 lilianzishwa na waliokuwa waasi wa Tutsi waliojiunga na jeshi la DRC chini ya mkataba wa amani wa mwaka 2009
Mwaka 2012 mwezi Aprili waasi wa M23 waliwageuka waliokuwa wanajeshi wenza na kuanza uasi Mashariki mwa nchi ambako kuna utajiri mkubwa wa madini.
 
Hofu yangu wanyaranda wasije wakadai walichongewa na jk.
 
wanashangaa nini laura nkunda si ndio alikua bingwa wa kutumia child soldier?
 
Aendae tezi na omo mwisho wake ngamani..
 
Rwanda yalalamikia Marekani kwa vikwazo

Jeshi la Rwanda limepuuzilia mbali hatua ya Marekani kuiwekea vikwazo kuhusiana na madai ya watoto kutumiwa kupigana kama wanajeshi katika vita ambavyo Rwanda inadaiwa kuunga mkono waasi wa M23 ndani ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Shirika la habari la AFP lilimemnukuu msemaji wa jeshi la Rwanda akisema kuwa sio haki kwa Rwanda kuadhibiwa kwa mambo ambayo hayafanyiki ndani ya mipaka yake wala kutekelezwa na jeshi la Rwanda

Joseph Nzabamwita alisema kuwa hatua ya kujumlisha Rwanda kuwa miongoni mwa nchi zinazotumia watoto kama wanajeshi haina misingi hata kidogo.

Umoja wa mataifa unatuhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 katika harakati zao dhidi ya serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo madai ambayo Rwanda imekana.
Mnamo siku ya Alhamisi naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani kuhusu maswala ya Afrika Linda Thomas-Greenfield alisema kuwa Marekani inatumia sheria ya kuwalinda watoto ya mwaka 2008 katika kuiwekea Rwanda vikwazo ili ikome kujihusisha na vita ndani ya DRC hususan katika kuwasajili watoto kama wanajeshi.
Kwa mujibu wa afisaa mkuu katika idara ya mambo ya nje alisema kuwa hatua hiyo itaifanya Rwanda kunyimwa msaada wa kijeshi katika mwaka 2014.
Nzabamwita alinukuliwa na AFP akisema kuwa Marekani inafahamu fika kuwa Rwanda haijawahi kuunga mkono utumiaji wa watoto kama wapiganaji na kuwa licha ya vikwazo hivyo Rwanda itaendelea kushirikiana na Marekani.
Kundi la waasi la M23 lilianzishwa na waliokuwa waasi wa Tutsi waliojiunga na jeshi la DRC chini ya mkataba wa amani wa mwaka 2009
Mwaka 2012 mwezi Aprili waasi wa M23 waliwageuka waliokuwa wanajeshi wenza na kuanza uasi Mashariki mwa nchi ambako kuna utajiri mkubwa wa madini.

Wanapiga kelele tu lakini kuna evidence za kutosha kuwatuhumu na kuwahukumu.
 
Msemo mzuri huu, fafanua.
Niliambiwa na rafiki zangu wa pwani/wavuvi kuwaTezi ni mbele ya jahazi,omo ni nyuma ya jahazi ngama ni katikati ya jahazi. Kwa wasafiri baharini hasa mabaharia huwa wanasema mtu ukimuona mara yupo mbele ya jahazi mara yupo nyuma ya jahazi ana kimbia kimbia tu bila utulivu lazima tu atakuja kupumzikia katikati ya jahazi ambako ndipo huwa kuna kibanda cha kula na kulala!
 
Kweli ila nadhani husemwa 'MWENDA TEZI NA OMO MSUBIRI NGAMANI'
 
kwelii lakini huwa wanawakusanya wale waibobo wanawaingiza jeshini.
 
Tighten the noose..! The truth will stand
 
Back
Top Bottom