Mada inahusu Viongozi kuheshimu ukomo Uongozi uliowekwa kikatiba ndiyo nikasema nijuavyo mimi ni TanZania tu hapa Afrika ndiyo inaheshimu mpaka sasa hivi ukomo wa Uongozi tuliojiwekea Kikatiba!
Hayo mengine uliyoandika kuhusu demokrasia ya Kenya au TanZania ni mada nyingine kabisa unaweza kuanzisha uzi halafu tukutane huko!
Kwani ni wapi uliona kiongozi Kenya akikiuka ukomo wa uongozi kulingana na katiba ya Kenya, fuatilia historia ya Kenya upate kujitaarifu. Nimesema sisi ndio tunafaa kuigwa maana tumefaulu kufanya ambayo kwa wenzetu ni ndoto.
Mambo gani hayo mliofanya ambayo ni ndoto kwa wengine? Kuuwana na kufukuzana kwa kuwa tu imetokea kuzaliwa sehemu ambayo siyo asili ya wazazi wako? Hiyo ndiyo unaita jambo la kuigwa na wengine?
Kila nchi ina ampungufu yake na mazuri pia, hata Tanzania ina mazuri na mabaya, hivyo usikomae na mabaya yetu tu. Kumbuka nyie kipindi cha uchaguzi huwa mnawanyofoa albino bila huruma, kitu ambacho sielewi vinahusiana vipi na demokrasia yenu.
Ukiweka pembeni mabaya kiasi unayoyaona kwetu, kuna mengine mengi mazuri ambayo bado ni ndoto kwa Watanzania. Kwa mfano tu, katiba mpya ambayo haijachakachuliwa ni jambo ambalo mnaota tu na hamjafanikiwa hata kukaribia.
Uongozi wenu bado upo kwenye chama kimoja na usanii mwingi, yaani rais wenu anachaguliwa na watu wachache wa CCM pale Dodoma, baada ya hapo mengine yote ni usanii mtupu. CCM wanawateua watu wachache kumchagua mtu mmoja miongoni mwa watangaza nia, halafu huyo mmoja anakua na uhakika wa kushinda urais. Nyie bado mbali sana.
Nchi nzima hakuna mtu anaefaa kuongoza wanyarwanda huu ni zaidi ya wazimu, wampe tu ufalme atawale milele
Demokrasia inatakiwa kuchukua mkondo wake. Haijalishi ameifanyia nini Rwanda.
Haijalishi? acha mizaha wewe
Rwanda na Burundi wanatakiwa wawekewe vikwazo na Tanzania:
Mzigo wa wakimbizi ni uzembe na tamaa za viongozi wao