RWANDA: Kagame avunja Bunge

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427


Rais Paul Kagame wa Rwanda amevunja bunge la Rwanda kulingana na ibara ya 79 ya katiba ya nchi hiyo, kwa matayarisho ya uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa mwezi Septemba tarehe 2.

Tume ya uchaguzi sasa inatarajiwa kutangaza siku rasmi ya kuanza kampeni itakayo wahusisha wagombeaji 521 kuwania viti 80 katika bunge.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili Kennes Bwire amezungumza na mwandishi wetu wa Rwanda Sylivanus Karemera na kuanza kwa kumuuliza sababu za Rwanda kuandaa uchaguzi mwezi Septemba wakati kulikuwepo uchaguzi mkuu mwaka jana 2017

Chanzo: DW
 
Ok, wewe mleta uzi mbona umeacha hewani habari kuhusu kwa nini uchaguzi mwaka huu wakati ni mwaka jana ulifanyika. Tutafutie jibu la hilo swali la DW!
 
Mr slim ana vituko sana ,hivi yule muasi Kallixte Sankala aliye anzisha uasi amefikia wapi mbona sijasikia kateka hata kijiji?
 
Sinema za maziwa makuu zimeanza
hata Magu alisema atavunja Bunge
Ok, wewe mleta uzi mbona umeacha hewani habari kuhusu kwa nini uchaguzi mwaka huu wakati ni mwaka jana ulifanyika. Tutafutie jibu la hilo swali la DW!
Hio ndio democray ya Africa
Watu wa Rwanda washachoka na utawala wake wa kidikteta Paul Kagame, nafikiri keshasoma alama za nyakati....

Ndugu zangu naomba niwakosoe kidogo kwenye hili,
Natumaini hamtakasirika kwasababu nafanya hivi kwa ajili ya kuelimishana.


Mosi,
Katiba ya Rwanda ya mwaka 2003 pamoja na Marekebisho yake yanamruhusu Raisi wa Rwanda kufanya hivyo. Katiba inasema hivi :
"For elections purposes, the President of the Republic dissolves the Chamber of
Deputies at least thirty (30) days and not more than sixty (60) days before the end of
the parliamentary term."


Pili,
Raisi wa Rwanda anavunja Bunge kwasababu limeshafisha muda wake wa miaka 5 hivyo inabidi alivunje ili wajiandae na uchaguzi mwezi September. Hili hata Tanzania na kwingineko duniani hufanyika, ambapo Raisi hufungua Bunge na pia hulivunja. Hivyo huu uvunjaji siyo ule wa Raisi kulifukuza bunge kwasababu wameshindana nalo "Hapana"


Tatu,
Uchaguzi wa Raisi na wabunge nchini Rwanda ni tofauti na wa hapa nchini kwetu ambako kwenye Uchaguzi mkuu huwa tunachagua Madiwani, Wabunge na Raisi kwa pamoja. Rwanda Raisi alichaguliwa kivyake na wabunge nao wanachaguliwa kivyake. Hata Marekani wanatumia huu mfumo, ambapo Raisi anachaguliwa peke yake na wawakilishi nao peke yao.


NB: Hivyo tukisema chanzo ni udikteta tutakuwa tunamuonea Kagame wa watu bure tu
 
Nami baada ya kuisoma vzr katiba yao,nikaona yuko sahihi ,ahsante pia kwa kutukumbusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…