Rwaitama, sisi ambao tumo ndani ya 20% ya waliobaki ambao walikuwepo kabla ya uhuru, tukae tu kuiona Tanzania inavyopaa tusijitoe ubinadamu

Wimbo

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
783
525
Hakuna democrasia kwenye umaskini, si yeye tu Rwaitama peke yake hata nyombo vya nje vinapiga kelele kwa sababu hofu kupoteza uwezo wa kuendelea kutupigisha magoti, wanashangaa tumejitambua, ukiwa na njaa mwenye chakula akikwambia piga magoti utapiga tu utake usitake,

Anachokifanya Magufuli anatengeneza mazingira ya democrasia ya kweli ya uchumi anaposema ni watu siyo vitu, watu bila vitu/uchumi mzuri mtayumbishwa tu.

Mbona JK aliwapa kusema mtakalo mwishoni mkasema ni Raid wa kuzurura, dhaifu ameharibu uchumi, mnataka Rais mkali anayeweza kukemea rushwa na kujenga uchumi amepatikana Magufuli mnalalama tulizeni kichwa kinyolewe. Kumbukeni yaliyowapata Libya Leo wanatamani wajue tu hata mifupa ilikofukiwa ili waiombe radhi.

Rwaitama Mimi na wewe ambao tumo ndani ya 20% ya waliobaki ambao walikuwepo kabla uhuru, tukae tu kuiona TZ inavyopaa tusijitoe ubinadamu kwa kutetea matumbo yetu 60% ya population ambayo ni vijana inahitaji kuona Tanzania Mpya kwa miaka 58 Tanzania imeweza kuwa na mamilionea wasiozidi 10 Magufuli ameahidi katika kipindi chake azalishe mamilionea angalau 100 na inawezekana pale mnapokuwa na uwezo wakukusanya kodi ili kutengeneza nafasi kuzalisha ndani zaidi kuuza nje /kununua kidogo kutoka nje hata kwa mambo nyasiyo muhimu.
 
Wimbo,
Tangu aingie madarakani amezalisha mabilionia wangapi zaidi ya Makonda bilionia mtumishi wa serikali!

Ungelikuwa mfanyabiashara ungejua jinsi hali ya biashara inavyozidi kuwa mbaya kwa kukosa wanunuzi.

Tatizo lako ni kumtazama Lwaitama kichadema mtazamo ambao ni wa kijinga, wiki iliyopita mliwalaumu Chadema kwa kukodi ndege kwenda Mwanza kwenye sherehe lakini mkapongeza ATCL kuwabeba wanaccm bure toka Mwanza kuja Dar!

Kila siku nyie tu mko sahihi! Huyo mungu wenu aliyewaumba wanaccm yuko mbingu ipi!
 
Ni kweli Magu siyo malaika, lakini hata Mungu siyo justice, wengine wanaomba mvua wajenzi wa barabara wanaomba jua, yeye ambaye ni Mkamilifu wengine wanamlilia wangine wanamshangilia, kwani !! Badhite aliwa millionea si maskini tumepungua, watu wa ndani wakifanikiwa ni ushindi kuliko wageni wanaochuma na kupeleka kwingine wananyonya nguvu zetu tuondoe wivu wa kipuuzi.
 
Savimbi Jr,
Eebwana ee! Miaka minne kazalisha masikini milioni 2? Halafu ndio wanaita mkombozi wa wanyonge! Najaribu kuwaza jee ingekuwa zile nchi wananchi wanafuatilia kila kitu serikali inafanya, Rais anafanya, jee tungekuwa tuko hali gani? Zomea zomea angepona kweli?
 
Wimbo,
Mzee unajivuruga mwenyewe ni 20% yako, magufuli hawezi kuongeza idadi ya mamillionea kwenye nchi sana sana ameweza kufanya idadi ya masikini iongezeke, mfumuko wa bei (bidhaa sokoni imeongezeka kipindi hiki, deni la taifa limeongezeka, Unemployment rate imepanda maradufu, wazururaji wameongezeka mitaani, (sijui kama na wewe unawaona ?)), akiendelea kutawala nchi hii magufuli inakoelekea hapafai, wataalamu wa Uchumi wanasema Uchumi umesinyaa, wanzasiasa wanaotumwa na rais wanasema uchumi umekua !!, sina uhakika kama na wewe unfukuzia Uteuzi, kwa nini wazee nchi hii mnapenda kujitoa Ufahamu ?, sio kwamba mnamsaidia huyu rais bali mnampotosha
 
Mimi binafsi sioni Cha kujifunza kwa mzee huo kwa Yale anayoyakemea Sasa na kuyahubiri,

Sent using Jamii Forums mobile app
Hauwezi kujifunza kwa sababu lugha anayoiongea iko juu zaidi ya upeo wako wa kufikiri na kuelewa. Polepole kabla ya kuingia CCM alikuwa akiongea kwa upeo wa juu na ulimletea sifa, alipojiunga CCM ilibidi ajishushe ili wanaccm waweze kumuelewa na amepoteza umaarufu wake.
Kama unaweza kupongeza ATCL kubeba abiria toka Mwanza mpaka Dar bure! Tutajifunza nini toka kwako.
 
Wimbo,
Wewe kama uko kwenye rika la Lwaitama na mawazo yako ni huu mgando kuwa eti kuwa huru ni kutenda kama wakoloni basi wewe ni zezeta zee ambalo linachungulia kaburi bila matumaini. Hivi kuna mzee anayelinganisha uhuru na kujenga madaraja huku tukitekwa na kuuana na mateso lukuki kwa wenye mawazo mbadala? Shameeeeeeeeeeeee! Nyerere rudi ukute haya masalia ambayo ulishindwa kuyabadilisha!!!
 
Bishweko,
Umenena Mkuu, kwa hiyo huyu mleta mada pamoja na kujidai kwamba yeye ni mmoja wa watu wazima wachache waliobaki, kumbe inawezekana ameshindwa tu kumuelewa Rwaitama sio ?.
 
Ni kweli Magu siyo malaika, lakini hata Mungu siyo justice, wengine wanaomba mvua wajenzi wa barabara wanaomba jua, yeye ambaye ni Mkamilifu wengine wanamlilia wangine wanamshangilia, kwani !! Badhite aliwa millionea si maskini tumepungua, watu wa ndani wakifanikiwa ni ushindi kuliko wageni wanaochuma na kupeleka kwingine wananyonya nguvu zetu tuondoe wivu wa kipuuzi.
Tupe vyanzo vyake halali vya mapato vya ghafla kuwa tajiri, mbona wengine utajiri wao unachunguzwa na tunaona wanakamatwa hata kwa kuonewa? Bashite kafanya biashara gani ya kumtajirisha ghafla hivi hadi ujisifie uzalendo wa kifisadi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bishweko, a USA kati maRais 45 waliokwisha itawala hatuna profesor, wasomi wengi hawawezi utawala wanapoteza muda mwingi kufikilia kujumlisha na kutoa huku nchi ikiliwa mfano hata wateule maprofesor baadhi walichemka katika nafasi zao.
.
Rwaitama ni njaa tu anabembeleza mkate anaolipwa na DJ
 
Tupe vyanzo vyake halali vya mapato vya ghafla kuwa tajiri, mbona wengine utajiri wao unachunguzwa na tunaona wanakamatwa hata kwa kuonewa? Bashite kafanya biashara gani ya kumtajirisha ghafla hivi hadi ujisifie uzalendo wa kifisadi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante mkuu! muelimishe huyo hata Mobutu alipopora uchumi wa nchi yake na kujenga jumba lenye airstrip kijijini kwake watu walilalama sana. Waliambulia majibu kama ya huyo mchambuzi uchwara-- "Eti ni bora mimi Mobutu nitajirike katika Congo kuliko mzungu kujitarisha hapa Congo". Ona hali ya Congo DRC sasa!!!!
 
Wale wanaodhani manunuzi yanayofanyika ndiyo maendeleo uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, mkoloni alijenga reli, madaraja, meli kwenye ziwa Tanganyika na Victoria na elimu ya kiwango cha kimataifa lakini tukamuondoa kwa sababu ya kukosa demokrasia ambayo ilituacha waafrika tubaki masikini.
 
[QUOHayo ni mawazo yake na wewe toa yako sio kumtuhumu tatizo la Watanzania mtu akisema ukweli anaonekana hafai, miaka 58 tumeshindwa kuijenga Tanzania leo ndio tutarajie maajabu ,mahitaji ya Tanzania ni mengi sana itatuchukua miaka 58 mingine kupata Tanzania mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wimbo,
Mbona hujaeleza kitu hata kimoja alichokisema mzee mwenzio Lwaitama ambacho kimekuwashawasha hadi kuanza kumshambulia!!?
Kama wewe ni mzee unaleta blah blah hizi, hakika we ndiyo unazeeka vibaya! Pia uwezo wako wa kumuelewa Lwaitama ni mdogo! Nyie msubiri amri ya kwenda kupokea ndege tu basi, na kumsifia Jiwe.
 
Wale wanaodhani manunuzi yanayofanyika ndiyo maendeleo uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, mkoloni alijenga reli, madaraja, meli kwenye ziwa Tanganyika na Victoria na elimu ya kiwango cha kimataifa lakini tukamuondoa kwa sababu ya kukosa demokrasia ambayo ilituacha waafrika tubaki masikini.
Hayo ndiyo aliyochangia Rwaitama, mawazo ambayo hayategemewi kutolewa msomi mbobezi kama yeye, tushughulike na dhana ya mkoloni na ya Magu; mkoloni alijenga reli asafirishe mkonge mbao na pamba kulisha viwanda vyake ulaya, Magu anajenga reli tusafirishe kwa haraka mazao yetu kwenda sokoni na faida isomeshe watoto wetu, hizo ndege mnazipanda lakini bado mnabeza hivi kwa binadamu asiyenalengo la kujitoa ufahamu au tu kutokusifia jambo zuri analofanya hasimu wako ni suala la kujadili? Magu anastahili kupongezwa kajitahidi sana.
 
Hakuna democrasia kwenye umaskini, si yeye tu Rwaitama peke yake hata nyombo vya nje vinapiga kelele kwa sababu hofu kupoteza uwezo wa kuendelea kutupigisha magoti, wanashangaa tumejitambua, ukiwa na njaa mwenye chakula akikwambia piga magoti utapiga tu utake usitake,

Anachokifanya Magufuli anatengeneza mazingira ya democrasia ya kweli ya uchumi anaposema ni watu siyo vitu, watu bila vitu/uchumi mzuri mtayumbishwa tu.

Mbona JK aliwapa kusema mtakalo mwishoni mkasema ni Raid wa kuzurura, dhaifu ameharibu uchumi, mnataka Rais mkali anayeweza kukemea rushwa na kujenga uchumi amepatikana Magufuli mnalalama tulizeni kichwa kinyolewe. Kumbukeni yaliyowapata Libya Leo wanatamani wajue tu hata mifupa ilikofukiwa ili waiombe radhi.

Rwaitama Mimi na wewe ambao tumo ndani ya 20% ya waliobaki ambao walikuwepo kabla uhuru, tukae tu kuiona TZ inavyopaa tusijitoe ubinadamu kwa kutetea matumbo yetu 60% ya population ambayo ni vijana inahitaji kuona Tanzania Mpya kwa miaka 58 Tanzania imeweza kuwa na mamilionea wasiozidi 10 Magufuli ameahidi katika kipindi chake azalishe mamilionea angalau 100 na inawezekana pale mnapokuwa na uwezo wakukusanya kodi ili kutengeneza nafasi kuzalisha ndani zaidi kuuza nje /kununua kidogo kutoka nje hata kwa mambo nyasiyo muhimu.
Inawezekana ni Wewe hujamwelewa huyu Mzee. Lakini Mimi naamini kama kweli Mh.analitakia mema taifa.hili angetengeneza kwanza katiba itayo tuongoza sisi wote hata atakaye fuata atalaImika kuiishi.Lakini huu utaratibu wa kuongoza kwa kufuata Sheria za mtu anazo amka nazo ni hatari sana.Kumbuka huyo naye ni binadamu atapita Lakini Taifa lipo tu.Cha maana sana atujengee misingi iliyopo katika maandishi siyo huu mtindo tunaoenda nao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom