RUVUMA: Mkuu wa Mkoa amsimamisha kazi Afisa Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amemsimamisha kazi afisa utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani humo PHILBERT MTWEVE kwa kosa kuwalipa mishahara watumishi hewa 8 na kuisababishia hasara serikali zadi ya milioni 27.

Kusimamishwa tu haotoshi. Vyombo vya dola vinatakiwa kula nae sahani moja
 
Kusimamishwa tu haotoshi. Vyombo vya dola vinatakiwa kula nae sahani moja
AMEMSIMAMISHA AU AMEAGIZA ASIMAMISHWE KAZI NA MAMLAKA YAKE YA NIDHAMU? MAANA YEYE HANA MAMLAKA YA KUSIMAMISHA KAZI WATUMISHI WA HALMASHAURI AMBAO KWA MUJIBU WA SHERIA NA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA 2002 NA 2003 AMBAZO KWAZO DED NDIYE MAMLAKA YA NIDHAMU. NAFIKIRI AMETOA MAAGIZO ASIMAMISHWE KAZI!!!
 
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amemsimamisha kazi afisa utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani humo PHILBERT MTWEVE kwa kosa kuwalipa mishahara watumishi hewa 8 na kuisababishia hasara serikali zadi ya milioni 27.

HAWA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WALIOSUBIRI TAMKO LA MAGHUFULI NA WALIKUWEPO KABLA MAGHUFULI HAJAWEPO MADARAKANI NAO NI MAJIPU YALIYOVIA. NINI MAANA YA MKUU WA MKOA AU WILAYA? SASA TUJIULIZE WALIKUWA WAKUU WA NINI?
 
Sina hakika kisheria kama mkuu wa wilaya ni mwajiri!!!!! DED afanye kazi gani!!!!
 
haya majipu, chunusi, vipele ni ving mno! hatuwezi kutumbua kimoja kimona tunahitani kujikwaruza ili vitumbuke kwa pamoja!
 
Back
Top Bottom