voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Hakuna "Hustler" bali wakenya wameingizwa mkenge!
Hii inatokana na nilichokiona na kuwasikia mawaziri wateule wa Serikali ya Ruto, mbele ya kamati ya bunge inayohusika na uthibitisho wa mawaziri hao(Vetting).
Nimetafakari sana kusikia kwamba Ukwasi walioutaja leo ambapo wamehojiwa Mawaziri watatu pekee.
Kwanza nianze na Rais Ruto pekee ambaye yuko kwenye orodha ya matajiri kumi wa Kenya akiwa na ukwasi wa 41 billions Kenya shillings.
Halafu makamu wake Richard Gachagua yeye anao ukwasi wa 800millios, Kenya shillings,pamoja na zile 200 millions Kenya shillings,ambazo zilikuwa zimetaifishwa na serikali anafikisha jumla ya ukwasi wa 1 bilion,Kenya shillings.
Leo hii Musalia Mudavadi ambae ni waziri mkuu mteule, Ametaja kuwa ukwasi wake ni 4.1bilions Kenya shillings.
Kuna mwanasheria mkuu mteule Justin Muturi ambae amesema ana ukwasi wa 700 millions, Kenya shillongs.
Mwingine aliefika leo mbele ya kamati hiyo ni Waziri wa Ulinzi mteule Hassan Dualle ambaye ametaja ukwasi wake kuwa ni 851 millions, Kenya shillings.
Kesho orodha itaendelea kwenye kamati hiyo.
MY Take!
Rutto aliweza kuwaaminisha walalahoi wa Kenya kuwa anatetea hustlers wa Kenya akijinasibu na lile toroli.
Lakini ukweli ni kwamba uchaguzi ule ulikuwa ni upinzani kati ya kambi mbili ambazo ni:
Ile ya watoto wa wanasiasa wenye majina katika historia ya Kenya kina Uhuru Kenyatta, Gideon Moi, Raila Odinga na wenzao wengine...
Dhidi ya kundi la waliowahi kuwa watumishi wa umma na kujitajirisha kupitia ufisadi mbalimbali, kulingana na nafasi walizowahi kuhudumu hapo awali, wakiongozwa na William Samoei Ruto, Musalia Mudavadi na Richard Gachagua na wenzao.
Kwa ukwasi huo hapo juu ni wazi kwamba wakenya wameruka matope na kukanyaga maji.
"Mwanasiasa akikwambia usiku umeingia, huku mkiwa ndani,vema utoke nje ukajiridhishe mwenyewe"
Alamsikhi.
View attachment 2390283View attachment 2390284